Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 4,951
- 19,766
Myself nachoshwa na hizi ngenga za kidini, yaani nachukizwa na kitu chochote kinachotengeneza matabaka.
Leo hii ukichunguza Kwa umakini unagundua hizi dini zinachangia pakubwa kuleta utengano kwenye jamii kuliko kuunganisha.
Watu wengi tunachekeana usoni tu lakini nafsi zetu zinajipendelea kulingana na matabaka tuliyojiwekeq.
Kwa sisi tunaoishi uswahilini mahali ambako ndipo watu wamekaririshwa hizi habari za kidini utagundua mengi.
Ni rahisi kusikia Kwa muislam ndiye mtu msafi kimwili zaidi kuliko mkristo.
Ni rahisi mkristo kumsema vibaya muislam kwamba ni mchawi anafuga majini,kitu ambacho ni sumu tunapanda Kwa watoto wetu
Ni vigumu Kwa muislam Kula au kunywa kwenye nyumba ya mkristo eti anakula vitu vichafu na haramu yaani nguruwe.
Lakini pia muislam humuona mwanaume mkristo kama mzinifu tu kwani wao wanaamini mke mmoja hatoshi.
Hizi mambo zinaenda direct Kwa watoto wetu na kuzidi kuipanda sumu ambayo itakuja kuleta mabalaa yasiyowezekana .
Jana katika maadhimisho ya sikukuu ya pasaka umetoka waraka kutoka TEC ukionesha kudai kitu wanachokiita haki.
Kwa upande wa Baraza la kiislam BAKWATA wapo kimya ,siku nyingi hawajatoa waraka wowote kuhusu yanayoendelea nchini.
Hili kinaweza kuamsha hisia Kwa watu wa upande fulani.
Lakini pia maoni na hisia za watanzania wengi naona maoni yamepokelewa kiutofauti harufu ya udini imekamata Kwa asilimia nyingi Sana.
Waislamu wengi (siyo wote) wanahisi hizi ni chuki za wakristo dhidi ya uislamu kwani hawa maaskofu ,anapotokea raisi mkristo kutoka huwa hawaongei wala kutoa maonyo yeyote hata kama viongozi wanakosea.
Mimi nimalize Kwa kusema nakubali mno serikali iliyopo madarakani,lakini najaribu kusisitiza uwepo wa HAKI.maana haki huinua taifa.
Tuna UHURU na AMANI ambayo tumedumu nayo Kwa miaka mingi isifike mahali tukafanya jambo litakalo haribu mfumo mzima wa maisha ya watanzania.
Tusidharau au kuruhusu viashiria kama hivi ni hatari Kwa maslahi na ustawi Kwa taifa.
Tusiidharau nguvu ya UMMA.
ogopa siku watu wakiungana hata kama ulikuwa unawamudu wakiwa mmoja mmoja siku wataangusha miliki yako