Ulaji huu wa mafuta ni kawaida?

Kama unaishi Dsm, 5w40 au 10w40 inakuhusu. 5w30 inaweza isiwe ideal saana kwa Dsm na mikoa mingine yenye joto kali, maana kuna vipindi joto linazidi nyuzi 35, japo ni vigumu saana kushuka zaidi ya nyuzi 10
Oil ipi recomended kwa mikoa yenye baridi kama Arusha?
 
Binafsi huwa natumia Total quartz 9000 5w 30..kuna ujazo wa lita 1 na lita 4.
Hapa nilipo lita 1 nanunua 15000/- lita4 55000/-

Castrol sina uzoefu na bei zake lakini ni oil bora pia kama ilivyo total.
Aisee ni kua makini maduka mengine ni wezi balaa,kuna maduka hapa mjini wanauza hio 5w30 lita 4 kwa 60,000 lkn kuna maduka ya wahindi wanauza lita 1 ya 5w30 kwa 35,000 maana yake lita 4 hapo unaongelea kwny 140,000.
 
Nadhani hio 20w40 mafundi wakibongo nchi nzima ndio wanaijua,ukisema unabadilisha tu oil jibu la kwanza la fundi ni hio 20w40.
 
Kwa uhakika aidi nunua kwenye petrol station za total....huko hakuna usanii
 
Nadhani hio 20w40 mafundi wakibongo nchi nzima ndio wanaijua,ukisema unabadilisha tu oil jibu la kwanza la fundi ni hio 20w40.
Ndiyo mafundi wetu hawataki kupanua maarifa[emoji23][emoji23][emoji23]
 
5w-20 zinapatikana??
 
5w-20 zinapatikana??
Unaweza kupata japo uwezekano mdogo. Sababu haifai kwa mazingira ya kwetu. Mikoa mingi ukiangalia asubuhi joto linaanzia nyuzi 20 kuendelea. So hiyo oil haifai kwa mazingira hayo. Ndio maana hata waagizaji wa oil wanaojua specs hawawezi kuileta.
 
Binafsi huwa natumia Total quartz 9000 5w 30..kuna ujazo wa lita 1 na lita 4.
Hapa nilipo lita 1 nanunua 15000/- lita4 55000/-

Castrol sina uzoefu na bei zake lakini ni oil bora pia kama ilivyo total.
Gari yako aina gani na ina cc ngapi
 
Mambo vip? Lete mrejesho
Nimeshauriana na fundi niiache oil iliyopo kwakuwa toka nimeweka haijafika km 1000.japo nimepewa maelezo tofauti,na mafundi na wauza oil tofauti.
Service ikifika nitabadili na kuweka hiyo 5w30.nitaleta mrejesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…