Tanzania tuna tatizo kubwa la mafundi....Mafundi wetu hawapendi kusoma au hata kugoogle info ambazo zitasaidia kukuza ujuzi wao..
Unakuta gari ndogo chini ya cc 1500 injini teknolojia ya kisasa fundi anakuambia weka oil namba 50... hapo lazima ukione kwenye fuel consumption.
5w 30 ni viscosity recommended kwa gari nyingi sana za teknolojia ya kisasa..
5w 30 ina uwezo wa kuhimili baridi kali sana na joto kali sana...pia inamudu masafa marefu.
Kuna hili suala la mafundi kusema gari ikishatembea 150k km, eti tumia 20w 50....hii elimu sijui wameipata wapi.
Binafsi nina nissani kwenye user manual yake wamerecommend 5w30 na hakuna mahali wameandika mileage ikifika 150k nitumie 20w50.
Mafundi wajisomee wasije wakafanya watanzania wayachukue magari yao.
Wakumbuke engine zinebadilika sana...siku hizi hakuna tena carburator...kuna VVTi, EFI n.k