Ulaji huu wa mafuta ni kawaida?

Ulaji huu wa mafuta ni kawaida?

Kama unaishi Dsm, 5w40 au 10w40 inakuhusu. 5w30 inaweza isiwe ideal saana kwa Dsm na mikoa mingine yenye joto kali, maana kuna vipindi joto linazidi nyuzi 35, japo ni vigumu saana kushuka zaidi ya nyuzi 10
Oil ipi recomended kwa mikoa yenye baridi kama Arusha?
 
Binafsi huwa natumia Total quartz 9000 5w 30..kuna ujazo wa lita 1 na lita 4.
Hapa nilipo lita 1 nanunua 15000/- lita4 55000/-

Castrol sina uzoefu na bei zake lakini ni oil bora pia kama ilivyo total.
Aisee ni kua makini maduka mengine ni wezi balaa,kuna maduka hapa mjini wanauza hio 5w30 lita 4 kwa 60,000 lkn kuna maduka ya wahindi wanauza lita 1 ya 5w30 kwa 35,000 maana yake lita 4 hapo unaongelea kwny 140,000.
 
Tanzania tuna tatizo kubwa la mafundi....Mafundi wetu hawapendi kusoma au hata kugoogle info ambazo zitasaidia kukuza ujuzi wao..

Unakuta gari ndogo chini ya cc 1500 injini teknolojia ya kisasa fundi anakuambia weka oil namba 50... hapo lazima ukione kwenye fuel consumption.

5w 30 ni viscosity recommended kwa gari nyingi sana za teknolojia ya kisasa..

5w 30 ina uwezo wa kuhimili baridi kali sana na joto kali sana...pia inamudu masafa marefu.

Kuna hili suala la mafundi kusema gari ikishatembea 150k km, eti tumia 20w 50....hii elimu sijui wameipata wapi.

Binafsi nina nissani kwenye user manual yake wamerecommend 5w30 na hakuna mahali wameandika mileage ikifika 150k nitumie 20w50.

Mafundi wajisomee wasije wakafanya watanzania wayachukue magari yao.
Wakumbuke engine zinebadilika sana...siku hizi hakuna tena carburator...kuna VVTi, EFI n.k
Nadhani hio 20w40 mafundi wakibongo nchi nzima ndio wanaijua,ukisema unabadilisha tu oil jibu la kwanza la fundi ni hio 20w40.
 
Aisee ni kua makini maduka mengine ni wezi balaa,kuna maduka hapa mjini wanauza hio 5w30 lita 4 kwa 60,000 lkn kuna maduka ya wahindi wanauza lita 1 ya 5w30 kwa 35,000 maana yake lita 4 hapo unaongelea kwny 140,000.
Kwa uhakika aidi nunua kwenye petrol station za total....huko hakuna usanii
 
Nadhani hio 20w40 mafundi wakibongo nchi nzima ndio wanaijua,ukisema unabadilisha tu oil jibu la kwanza la fundi ni hio 20w40.
Ndiyo mafundi wetu hawataki kupanua maarifa[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kinachokumaliza ni hiyo 20w-50 ndio mana consumption iko juu... ukitaka kuamini weka castro 5w-30 utaona tofauti mimi nilifanya makosa hayohayo nilimwaga oil iliokuja na gari nikajichanganya nikaweka 20w-50 lita sita engine ya V6 ndani ya siku moja tu nilianza kuona gari imekuwa nzito na mafuta yanakwenda haswa nikaingia hasara nikaimwaga na kubadili hadi filter nikaweka castro 5w-30 recommended aisee raha sana gari nyepesi sana mafuta kiduchu nasafiri mkoani safi na ni km 10000 ila kwasasa nimeshafagia km 6000 nataka next week nitoe niweke mpya
5w-20 zinapatikana??
 
5w-20 zinapatikana??
Unaweza kupata japo uwezekano mdogo. Sababu haifai kwa mazingira ya kwetu. Mikoa mingi ukiangalia asubuhi joto linaanzia nyuzi 20 kuendelea. So hiyo oil haifai kwa mazingira hayo. Ndio maana hata waagizaji wa oil wanaojua specs hawawezi kuileta.
 
Binafsi huwa natumia Total quartz 9000 5w 30..kuna ujazo wa lita 1 na lita 4.
Hapa nilipo lita 1 nanunua 15000/- lita4 55000/-

Castrol sina uzoefu na bei zake lakini ni oil bora pia kama ilivyo total.
Gari yako aina gani na ina cc ngapi
 
Mambo vip? Lete mrejesho
Nimeshauriana na fundi niiache oil iliyopo kwakuwa toka nimeweka haijafika km 1000.japo nimepewa maelezo tofauti,na mafundi na wauza oil tofauti.
Service ikifika nitabadili na kuweka hiyo 5w30.nitaleta mrejesho
 
Back
Top Bottom