SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.


ugali umetulea na kutukuza tulio wengi lakini imefika wakati lazima tuweke mambo wazi, tufikirie nje ya box tuachane na ile misemo "la msingi shibe ipatikane ili tuendelee kuishi"

.................................

vyakula vilivyojitosheleza unaweza kula bila mboga mfano wali, ndizi, Pilau, mkate, maandazi, chips, chapari, viazi, n.k, Ugali ni Chakula cha ajabu huwezi kula bila mboga wala kunywea chai.

Ni chakula maarufu zaidi kwenye sehemu za mateso kama jela, watoto wasiojitambua wanalishwa kinguvu ni kinyume na nature.

Mahindi yaliletwa Africa kutoka Ulaya mwaka wa 700, ni chakula kizuri kinapokuwa bado kibichi mfano kuandaa mahindi yaliyochomwa, kuchemsha, kande za mahindi mabichi, n.k. Shida ya ugali ni kusubiri mpaka mahindi yakauke.

mahindi sio utamaduni wa mwafrika yaliletwa na wakoloni kutokea ulaya, Chakula chetu cha asili ni mtama, ndizi, ulezi, magimbi uwele, mihogo.

hapo zamani mahindi yalipoletwa kutoka ulaya, babu zetu walizoeshwa kula ugali kwa maksudi ili kuwakandamiza uwezo wa kufikiri na kuwaongezea nguvu za kufanya kazi mashambani, Mtu anaweza kuwa genius anaekula ugali lakini ilibidi awe mara 4 zaidi bila ugali.

Ushahidi / Proof kwa hapa nchini ukifuatilia makabila yanayotoa vichwa (Wakerewe, Wachaga, Wahaya, Wanyakyusa waliokulia vijijini) utagundua hawali sana ugali, na bado sio uwezo wao kamili kwasababu siku mbili au tatu za wiki wanafinya matonge ya ugali.

Ni kweli Mboga za majani na samaki huongeza akili lakini kosa linalofanywaa ni kuvila kwa ugali, huu ugali unayeyusha / ku dilute virutubisho.

Ushauri wa bure kabisa, Muweke mbali mtoto na ugali ili kumsaidia kutunza uwezo wa akili zake, ugali unadumaza zaidi akili utotoni hadi balehe kipindi ambacho ubongo unapanuka.
 
Mimi nisipokula ugali week huwa nahisi kuhaha na nitautafuta kokote unakopatikana niukule kwanza.

Ugali huwa ni mtamu sana licha ya kwamba hauliki bila mboga ila utamu wake huwezi kuuona kama unakula kwasababu hauna machaguo mengine ya vyakula kwa maana huo ndio unakopatikana kutokana na budget yako, hapo lazima ukuchoshe.

Na hapo kwenye kula na mboga au bila mboga nadhani inaweza kumake sense ila ni kama inakuja halafu inakataa kwa maana ugali unatokana na mahindi au muhogo sasa ukiangalia mahindi ni kwamba yanauwezo wakutoa vyakula vingi ambavyo mtu anaweza kula bila mboga na the same kwa mihogo.

Kwahiyo maybe kinachofanya ugali ushindwe kuliwa bila mboga ni zile hatua za uandaaji wake Kwahiyo inawezekana kama kungekua na namna tofauti ya kuuandaa ugali basi ungeweza kuliwa bila mboga, kwa maana ugali hauwekwi chumvi hauwekwi mavuta hauwekwi nyanya wala kitunguu wala nazi wala chochote kile kama vyakula vingine vinavyoliwa bila mboga ila wenyewe ni maji na unga tu shwaaaaaaaa unakitoa kituuuuuu 😆😆😆

Ugali uheshimiwe guys.
 
Hapa Kuna ulakini flani, nchi karibu zote hawali ugali, ila huku ukila ugali unaonekana wa asili,


Kwa tuliosoma shule za kibishi, mkishakunywa uji saa 4 vipindi vinavyofata ilikua kama kukamilisha ratiba tu, watu wamechoka kama wamekula visungura
 
Hapa Kuna ulakini flani, nchi karibu zote hawali ugali, ila huku ukila ugali unaonekana wa asili,


Kwa tuliosoma shule za kibishi, mkishakunywa uji saa 4 vipindi vinavyofata ilikua kama kukamilisha ratiba tu, watu wamechoka kama wamekula visungura
True story kabisa mkuu, hii kitu kuna namna inapunguza na kudidimiza uwezo wa kufikiri.
Uji wake ni jau vile vile huko mashuleni boarding hizi za kayumba ni mwendo wa kulala kwenye pindi la mathe baada ya kupiga porenga ni msala sana hii kitu.

Hallelujah!!!
 
Mwenye shibe hawezi kumkumbuka mwenye njaa

ugali ni kama chakula cha kiutamaduni, neno duni naomba liheshimiwe

wengi tumeshazoea kula ugali ili kupoza njaa na kuamini ni lishe yenye kuleta ukakamavu hayo mambo ya faida na hasara tuwaachie wanasayansi na watafiti
ipo nchi inaongoza kwa kulima mahindi lakini mazao yake wanalisha ng'ombe
 
Ugali sio chakula ni basi tu limekosekana jina sahihi kuwakilisha hayo mauji uji.

Ukishaona msosi official wa jela ni ugali, ndio hapo ambapo unatakiwa ujifikirie mara mbili kujiuliza ugali ni nini na umefata nini jela.

Kumbuka jela ni sehemu ya mateso, kila chochote kinachofanyika kule ni kwa ajili ya kuwa sehemu ya hayo mateso.

Sera ya jela ni kuwa hawawezi kukupa chochote ambacho kitakufanya wewe ujisikie raha.

Sasa ugali kama ni chakula, umefikaje kule?

Kuna namna ambayo ugali unatumika kama instrument of torture sema bado watu hawajastukia tu.
 
Au sio
 
Kwa mbali ugali wa unga uliokobolewa unapunguza madhara, unakutana na mtu anakula DONA !! unga ambao haujakobolewa umechanganywa na PUMBA.
 
Ugali wa mahindi hutokana na mahindi yaliyokomaa au kukauka sana na kisha kusagwa na kusonga unga wake kwenye maji ya moto. Tukumbuke kuwa mahindi mabichi ambayo huchomwa au kubanikwa nayo ni ugali ambao hauhitaji mboga!

Faida ya ugalli ni kuupa mwili nguvu kama ilivyo kwa vyakula vingine vya wanga, si kujaza tumbo tu.

Aidha, kiini cha njano cha punje au mbegu za mahindi hutoa mafuta; na baadhi ya mashina ya mahindi mabichi ni miwa mitamu kabla ya kukomaa kuwa mabua. Tuyape heshima mahindi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…