SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na madai kuwa ulaji wa ugali hudumaza akili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?

02692B18-05FE-4851-857F-7A5DA6E174CD.jpeg
 
Tunachokijua
Ugali ni chakula kinachotumika sana Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa utafiti wa Onu Okpa et al (2019), “Sub-Saharan African Maize-Based Foods - Processing Practices, Challenges and Opportunities” mahindi huchangia 30% ya nishati za vyakula wanavyotumia watu wa ukanda huu kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti huu, kila mtu anayepatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara hutumia wastani wa kati ya gramu 52-450 za mahindi kwa siku. Ni chanzo kikuu cha ugali unaotumika kila siku kwenye nchi hizi. Kwa Tanzania, 64% ya wananchi wake hula chakula hiki walau mara 5-7 kwa wiki.

Takwimu hizi zinaonesha kuwa ugali ni chakula kinachotumika sana, pengine kuliko aina nyingine za vyakula. Baadhi ya watu huutengeneza kwa kutumia unga wa mhogo, mtama, ulezi pamoja na aina zingine za nafaka.

Bila kujali tofauti ndogo za mgawanyiko wa virutubisho, nafaka zote husifika kwa kuwa na kiasi kikubwa cha nishati na wanga, pia kiasi kidogo cha madini na vitamini muhimu kwa afya.

Kuhusishwa na udumavu wa akili
Kitaalamu, udumavu wa akili husababishwa mambo mengi ikiwemo baadhi ya changamoto za kijenetiki mfano Down’s syndrome, kukosa hewa ya kutosha wakati wa kuzaliwa, maambukizi makali ya homa ya uti wa mgongo, utapiamlo, matumizi ya baadhi ya madawa na pombe wakati wa ujauzito pamoja na sababu zingine siziso wazi sana.

Kwa kurejea mgawanyiko wa virutubusho vinavyopatikana kwenye nafaka zinazotumika kutengenezea ugali, hakuna uhusiano wa moja kwa moja unaoweza kutajwa, au pia kuhusishwa na kusababisha udumavu wa akili kwa watu. Virutubisho na madini yake havina athari hasi kwenye afya ya ubongo.

Pia, JamiiForums imezungumza na wataalamu wa lishe ambao wamethibitisha kuwa chakula hiki ni salama, hakiwezi kusababisha madhara tajwa.

Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayana ukweli uliojengwa kwa hoja za kisayansi. Ni uzushi usio na uthibitisho wa tafiti au takwimu.
1727993405658.png


ugali umetulea na kutukuza tulio wengi lakini imefika wakati lazima tuweke mambo wazi, tufikirie nje ya box tuachane na ile misemo "la msingi shibe ipatikane ili tuendelee kuishi"

.................................

vyakula vilivyojitosheleza unaweza kula bila mboga mfano wali, ndizi, Pilau, mkate, maandazi, chips, chapari, viazi, n.k, Ugali ni Chakula cha ajabu huwezi kula bila mboga wala kunywea chai.

Ni chakula maarufu zaidi kwenye sehemu za mateso kama jela, watoto wasiojitambua wanalishwa kinguvu ni kinyume na nature.

Mahindi yaliletwa Africa kutoka Ulaya mwaka wa 700, ni chakula kizuri kinapokuwa bado kibichi mfano kuandaa mahindi yaliyochomwa, kuchemsha, kande za mahindi mabichi, n.k. Shida ya ugali ni kusubiri mpaka mahindi yakauke.

mahindi sio utamaduni wa mwafrika yaliletwa na wakoloni kutokea ulaya, Chakula chetu cha asili ni mtama, ndizi, ulezi, magimbi uwele, mihogo.

hapo zamani mahindi yalipoletwa kutoka ulaya, babu zetu walizoeshwa kula ugali kwa maksudi ili kuwakandamiza uwezo wa kufikiri na kuwaongezea nguvu za kufanya kazi mashambani, Mtu anaweza kuwa genius anaekula ugali lakini ilibidi awe mara 4 zaidi bila ugali.

Ushahidi / Proof kwa hapa nchini ukifuatilia makabila yanayotoa vichwa (Wakerewe, Wachaga, Wahaya, Wanyakyusa waliokulia vijijini) utagundua hawali sana ugali, na bado sio uwezo wao kamili kwasababu siku mbili au tatu za wiki wanafinya matonge ya ugali.

Ni kweli Mboga za majani na samaki huongeza akili lakini kosa linalofanywaa ni kuvila kwa ugali, huu ugali unayeyusha / ku dilute virutubisho.

Ushauri wa bure kabisa, Muweke mbali mtoto na ugali ili kumsaidia kutunza uwezo wa akili zake, ugali unadumaza zaidi akili utotoni hadi balehe kipindi ambacho ubongo unapanuka.
 
Ni Chakula cha ajabu huwezi kula bila mboga, vyakula vingine kama wali, ndizi, mkate, maandazi, chips, chapari, viazi unaweza kula bila mboga, Why ugali ?

Niliwahi kusikia hapo zamani ugali kilikiwa chakula cha watumwa kwa maksudi ili kukandamiza uwezo wa kufikiri na maharage huleta usingizi, ni dawa ya kumfanya mtu asifikie maximum potential ya uwezo kufikiri, Kwa hapa nchini ukifuatilia sehem zimazotoa vichwa utagundua hawali sana ugali
Mimi nisipokula ugali week huwa nahisi kuhaha na nitautafuta kokote unakopatikana niukule kwanza.

Ugali huwa ni mtamu sana licha ya kwamba hauliki bila mboga ila utamu wake huwezi kuuona kama unakula kwasababu hauna machaguo mengine ya vyakula kwa maana huo ndio unakopatikana kutokana na budget yako, hapo lazima ukuchoshe.

Na hapo kwenye kula na mboga au bila mboga nadhani inaweza kumake sense ila ni kama inakuja halafu inakataa kwa maana ugali unatokana na mahindi au muhogo sasa ukiangalia mahindi ni kwamba yanauwezo wakutoa vyakula vingi ambavyo mtu anaweza kula bila mboga na the same kwa mihogo.

Kwahiyo maybe kinachofanya ugali ushindwe kuliwa bila mboga ni zile hatua za uandaaji wake Kwahiyo inawezekana kama kungekua na namna tofauti ya kuuandaa ugali basi ungeweza kuliwa bila mboga, kwa maana ugali hauwekwi chumvi hauwekwi mavuta hauwekwi nyanya wala kitunguu wala nazi wala chochote kile kama vyakula vingine vinavyoliwa bila mboga ila wenyewe ni maji na unga tu shwaaaaaaaa unakitoa kituuuuuu 😆😆😆

Ugali uheshimiwe guys.
 
Hapa Kuna ulakini flani, nchi karibu zote hawali ugali, ila huku ukila ugali unaonekana wa asili,


Kwa tuliosoma shule za kibishi, mkishakunywa uji saa 4 vipindi vinavyofata ilikua kama kukamilisha ratiba tu, watu wamechoka kama wamekula visungura
 
Hapa Kuna ulakini flani, nchi karibu zote hawali ugali, ila huku ukila ugali unaonekana wa asili,


Kwa tuliosoma shule za kibishi, mkishakunywa uji saa 4 vipindi vinavyofata ilikua kama kukamilisha ratiba tu, watu wamechoka kama wamekula visungura
True story kabisa mkuu, hii kitu kuna namna inapunguza na kudidimiza uwezo wa kufikiri.
Uji wake ni jau vile vile huko mashuleni boarding hizi za kayumba ni mwendo wa kulala kwenye pindi la mathe baada ya kupiga porenga ni msala sana hii kitu.

Hallelujah!!!
 
Mwenye shibe hawezi kumkumbuka mwenye njaa

ugali ni kama chakula cha kiutamaduni, neno duni naomba liheshimiwe

wengi tumeshazoea kula ugali ili kupoza njaa na kuamini ni lishe yenye kuleta ukakamavu hayo mambo ya faida na hasara tuwaachie wanasayansi na watafiti
ipo nchi inaongoza kwa kulima mahindi lakini mazao yake wanalisha ng'ombe
 
Ugali sio chakula ni basi tu limekosekana jina sahihi kuwakilisha hayo mauji uji.

Ukishaona msosi official wa jela ni ugali, ndio hapo ambapo unatakiwa ujifikirie mara mbili kujiuliza ugali ni nini na umefata nini jela.

Kumbuka jela ni sehemu ya mateso, kila chochote kinachofanyika kule ni kwa ajili ya kuwa sehemu ya hayo mateso.

Sera ya jela ni kuwa hawawezi kukupa chochote ambacho kitakufanya wewe ujisikie raha.

Sasa ugali kama ni chakula, umefikaje kule?

Kuna namna ambayo ugali unatumika kama instrument of torture sema bado watu hawajastukia tu.
 
View attachment 3114645

Ni Chakula cha ajabu huwezi kula bila mboga wala kunywea chai.

vyakula vilivyojitosheleza unaweza kula bila mboga mfano wali, ndizi, mkate, maandazi, chips, chapari, viazi, n.k, ni

hapo zamani watumwa walilishwa ugali kwa maksudi ili kuwakandamiza uwezo wa kufikiri, ni dawa iliyotumika kupunguza uwezo wa kufikiria (Thinking capacity), Mfano mdogo usiopingika ni kwa hapa nchini ukifuatilia sehem zinazotoa vichwa utagundua hawali sana ugali, lakini bado sio uwezo wao kamili kwasababu kuna baadhi ya siku wanafinya matonge ya ugali.

Ushauri wa bure kabisa, ukitaka kumuongezea mtoto uwezo wa akili usije usimzoeshe ugali, kiwe chakula cha kufanyia mazoezi namna ya kula ili ugenini asitie aibu.
Au sio :AYOOO: :AYOOO:
 
Ugali sio chakula ni basi tu limekosekana jina sahihi kuwakilisha hayo mauji uji.

Ukishaona msosi official wa jela ni ugali, ndio hapo ambapo unatakiwa ujifikirie mara mbili kujiuliza ugali ni nini na umefata nini jela.

Kumbuka jela ni sehemu ya mateso, kila chochote kinachofanyika kule ni kwa ajili ya kuwa sehemu ya hayo mateso.

Sera ya jela ni kuwa hawawezi kukupa chochote ambacho kitakufanya wewe ujisikie raha.

Sasa ugali kama ni chakula, umefikaje kule?

Kuna namna ambayo ugali unatumika kama instrument of torture sema bado watu hawajastukia tu.
Kwa mbali ugali wa unga uliokobolewa unapunguza madhara, unakutana na mtu anakula DONA !! unga ambao haujakobolewa umechanganywa na PUMBA.
 
Ugali wa mahindi hutokana na mahindi yaliyokomaa au kukauka sana na kisha kusagwa na kusonga unga wake kwenye maji ya moto. Tukumbuke kuwa mahindi mabichi ambayo huchomwa au kubanikwa nayo ni ugali ambao hauhitaji mboga!

Faida ya ugalli ni kuupa mwili nguvu kama ilivyo kwa vyakula vingine vya wanga, si kujaza tumbo tu.

Aidha, kiini cha njano cha punje au mbegu za mahindi hutoa mafuta; na baadhi ya mashina ya mahindi mabichi ni miwa mitamu kabla ya kukomaa kuwa mabua. Tuyape heshima mahindi!
 
Back
Top Bottom