SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na madai kuwa ulaji wa ugali hudumaza akili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?

02692B18-05FE-4851-857F-7A5DA6E174CD.jpeg
 
Tunachokijua
Ugali ni chakula kinachotumika sana Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa utafiti wa Onu Okpa et al (2019), “Sub-Saharan African Maize-Based Foods - Processing Practices, Challenges and Opportunities” mahindi huchangia 30% ya nishati za vyakula wanavyotumia watu wa ukanda huu kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti huu, kila mtu anayepatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara hutumia wastani wa kati ya gramu 52-450 za mahindi kwa siku. Ni chanzo kikuu cha ugali unaotumika kila siku kwenye nchi hizi. Kwa Tanzania, 64% ya wananchi wake hula chakula hiki walau mara 5-7 kwa wiki.

Takwimu hizi zinaonesha kuwa ugali ni chakula kinachotumika sana, pengine kuliko aina nyingine za vyakula. Baadhi ya watu huutengeneza kwa kutumia unga wa mhogo, mtama, ulezi pamoja na aina zingine za nafaka.

Bila kujali tofauti ndogo za mgawanyiko wa virutubisho, nafaka zote husifika kwa kuwa na kiasi kikubwa cha nishati na wanga, pia kiasi kidogo cha madini na vitamini muhimu kwa afya.

Kuhusishwa na udumavu wa akili
Kitaalamu, udumavu wa akili husababishwa mambo mengi ikiwemo baadhi ya changamoto za kijenetiki mfano Down’s syndrome, kukosa hewa ya kutosha wakati wa kuzaliwa, maambukizi makali ya homa ya uti wa mgongo, utapiamlo, matumizi ya baadhi ya madawa na pombe wakati wa ujauzito pamoja na sababu zingine siziso wazi sana.

Kwa kurejea mgawanyiko wa virutubusho vinavyopatikana kwenye nafaka zinazotumika kutengenezea ugali, hakuna uhusiano wa moja kwa moja unaoweza kutajwa, au pia kuhusishwa na kusababisha udumavu wa akili kwa watu. Virutubisho na madini yake havina athari hasi kwenye afya ya ubongo.

Pia, JamiiForums imezungumza na wataalamu wa lishe ambao wamethibitisha kuwa chakula hiki ni salama, hakiwezi kusababisha madhara tajwa.

Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayana ukweli uliojengwa kwa hoja za kisayansi. Ni uzushi usio na uthibitisho wa tafiti au takwimu.
Ugali ni chakula cha wanyama kama farasi..hivi unawezaje kula chakula kama kile
 
The term “maize” is derived from the ancient word mahiz from the Taino language — a now extinct Arawakan language — of the indigenous people of pre-Columbian America. Columbus and other explorers took maize back to Europe with them and it spread across the trade routes of Europe, Africa and Asia in the 1500s and 1600s.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fala wewe, kwahiyo mtu anayekula vitumbua hali mchele!?,unga wa ugali si unatokana na mahindi!?, Kwahiyo unga wa mahindi una matatizo, ila mahindi hayana shida!?,hivi jamii forums imevamiwa na watoto siku hizi!??
Ha ha ha ni hatari sheikh. Inashangaza
 
Kwani makuli wapo Tz peke yake?
Nchi ambayo kwa mwaka hayafiki makontena 1mil

Nigeria hawali ugali ila wana miili mikubwa
Nigeria awali ugali? Au kwa vile wanaita Jina tofauti? Humu jukwaani wapotoshani mmekuwa wengi Sana.
 
Na ukisoma historia zinadia kuwa kabla ya wakoloni kuja Afrika, Afrika haikuwa na utamaduni wa kula ugali.

Kwa hiyo ujio wa wakaloni ndio mwanzo wa ugali.

Kabla ya wakoloni Afrika ilikuwa na wazee timamu sana kwenye kichwa ila hayo yote yalikuja ku change ghafla baada ya ugali kuwasili.

Ukifanya tafakuri ya kina utaona wakoloni walitumia ugali kama bio weapon ya kuwadhoofisha wazee wetu kiakili.

Na sehemu wakoloni waliyokuja kumaliza mchezo kwa kuwavuruga akili mazima wazee wetu ni pale walipoingia porini kutafuta majani yanayoteleza na kuyapa jina la mlenda na kufanya hiyo ndio combinations bora ya mlo wa ugali.

Baada ya hapo ndio tumefikia hapa tulipo kila mtu amepoteana, tumekata ringi hatuna dira.

And sometimes if we're being honest, we gotta admit to speak the truth, that the world is better off without us.
Sidhani kama ulikuwepo kipindi hicho
Ila inaonekana hata hujui historia uliyofunzwa darasani

Colonialists did not introduce ugali in Africa.

Ugali ni chakula ambacho ni utamaduni wa mataifa mengi Afrika,
mfano :
-Tanzania na kenya tunaita UGALI
-Uganda wanaita POSHO
-Zambia na malawi wanaita NSHIMA
-Zimbabwe wanaita SADZA
-South Africa wanaita PAP
-Nigeria wanaita TUWO
-senegal wanaita COUSCOUS
-sudani wanaita KISRA

hii ni kuonyesha tu namna gani chakula hiki ni tamaduni ya Afrika

Kwahio chakula hiki hakitumiki sana EUROPE au Marekani sababu kubwa si tamaduni yao
Ila ukienda katika migahawa yao UGALI unaweza kuukuta na baadhi ya wazungu wanatumia na wanapenda sana

Nenda CHINA ukikuta wanakula NYOKA, Dim Sum,Peking Duck,Xiao Long Bao na Kung Pao Chicken

Nenda MAREKANI ukikuta wanakula Hamburgers,Hot Dogs,frybread, cornbread na succotash

Mlivo na akili mbovu pamoja na mtoa mada mtasema wanakula Sumu kama ambavyo mmejazana ujinga nyie na kuona UGALI ni sumu

Hatukatai Wakoloni wamechangia kwa kubwa kwenye vyakula vya africa lakini ugali Afrika ulikua enzi na enzi hayupo anaejua historia yake kwa sasa

Ila mkoloni amekuta ugali ndio chakula kikuu na ndio tamaduni yetu labda tu mtu akizungumzia Ugali ujue hatuzungumzii tu mahindi pekee, hapo kuna mihogo, mtama, viazi na ulezi na nk. vyote hivo vilikuwepo kabla ya mkoloni

(Sasa kama vyote hivo havikuepo na vililetwa na mkoloni ina maana walikua wanakula mchanga au [emoji23][emoji23][emoji23] kazi kweli kweli kwenye bongo zenu hahahah )

Mwanzo wakoloni walipoweka food crops cultivation hakukuwa na maana huku hakukuwa na huo ukulima bali ulikua unafanyika locally
Na baada ya kuona hayana faida katika uchumi wao wakabadilisha kwenda kwenye cash crops

Sasa huo mlenda unaosema waafrika wamefundishwa na wazungu hebu tuambie ulikuwepo wakati wanafundisha au umesoma wapi historia hio?
 
#Bring back our Ugali. Ugali ndio chakula kikuu ukanda wa Afrika ya kati. Ugali unaliwa sambamba na chakula kingine kinachoitwa mboga. Mboga inaweza kuwa ni majani malaini yaliyochemshwa na kuungwa vizuri au mchuzi wa nyama. Ugali hushibisha vema kuliko chakula kingine. Ugali ndio chakula kikubwa, popular food
 
Sidhani kama ulikuwepo kipindi hicho
Ila inaonekana hata hujui historia uliyofunzwa darasani

Colonialists did not introduce ugali in Africa.

Ugali ni chakula ambacho ni utamaduni wa mataifa mengi Afrika,
mfano :
-Tanzania na kenya tunaita UGALI
-Uganda wanaita POSHO
-Zambia na malawi wanaita NSHIMA
-Zimbabwe wanaita SADZA
-South Africa wanaita PAP
-Nigeria wanaita TUWO
-senegal wanaita COUSCOUS
-sudani wanaita KISRA

hii ni kuonyesha tu namna gani chakula hiki ni tamaduni ya Afrika

Kwahio chakula hiki hakitumiki sana EUROPE au Marekani sababu kubwa si tamaduni yao
Ila ukienda katika migahawa yao UGALI unaweza kuukuta na baadhi ya wazungu wanatumia na wanapenda sana

Nenda CHINA ukikuta wanakula NYOKA, Dim Sum,Peking Duck,Xiao Long Bao na Kung Pao Chicken

Nenda MAREKANI ukikuta wanakula Hamburgers,Hot Dogs,frybread, cornbread na succotash

Mlivo na akili mbovu pamoja na mtoa mada mtasema wanakula Sumu kama ambavyo mmejazana ujinga nyie na kuona UGALI ni sumu

Hatukatai Wakoloni wamechangia kwa kubwa kwenye vyakula vya africa lakini ugali Afrika ulikua enzi na enzi hayupo anaejua historia yake kwa sasa

Ila mkoloni amekuta ugali ndio chakula kikuu na ndio tamaduni yetu labda tu mtu akizungumzia Ugali ujue hatuzungumzii tu mahindi pekee, hapo kuna mihogo, mtama, viazi na ulezi na nk. vyote hivo vilikuwepo kabla ya mkoloni

(Sasa kama vyote hivo havikuepo na vililetwa na mkoloni ina maana walikua wanakula mchanga au [emoji23][emoji23][emoji23] kazi kweli kweli kwenye bongo zenu hahahah )

Mwanzo wakoloni walipoweka food crops cultivation hakukuwa na maana huku hakukuwa na huo ukulima bali ulikua unafanyika locally
Na baada ya kuona hayana faida katika uchumi wao wakabadilisha kwenda kwenye cash crops

Sasa huo mlenda unaosema waafrika wamefundishwa na wazungu hebu tuambie ulikuwepo wakati wanafundisha au umesoma wapi historia hio?
Historia inaonesha kabla ya karne ya 7 Africa hakukuwa na mahindi.

Labda huo ugali ulikuwa ni wa ngano au ulezi ila mahindi asili yake sio Africa.
 
Usifananishe ugali na vitu vya kijinga!
Ugali nyama choma na kachumbali pilipili kwa mbaaali we!! Ni hatari....!!
 
Wadau nawasabahi.

Umewahi kujiuliza ugali unaliwa sana na Watu wa aina gani? Utafiti mdogo nilioufanya sehemu nyingi iwe mitaa kwa Mama Lishe kwenye MAPUB au mabaa idadi kubwa ya Watu Wanakula UGALI ni Watu wa kiwango na Kipato cha CHINI. Tembelea Mikoani mpaka Vijijini UGALI ndio chakula kikuu kwa Watu Waishio huko.

Mfano wa Pili Mashuleni Hospital Magereza na Mahabusu za Polisi UGALI ndio Chakula kikuu na Wote wanakula UGALI ktk sehemu hizo ni Watu Wasio na UWEZO hivyo lazima TIKUBALI kuwa KULA UGALI dalili Kubwa ya UMASIKINI.
 
Wadau nawasabahi.Umewahi kujiuliza UGALI unaliwa sana na Watu wa aina gani?Utafiti mdogo nilioufanya sehemu nyingi iwe mitaa kwa Mama Lishe kwenye MAPUB au mabaa idadi kubwa ya Watu Wanakula UGALI ni Watu wa kiwango na Kipato cha CHINI.Tembelea Mikoani mpaka Vijijini UGALI ndio chakula kikuu kwa Watu Waishio huko.
Mfano wa Pili Mashuleni Hospital Magereza na Mahabusu za Polisi UGALI ndio Chakula kikuu na Wote wanakula UGALI ktk sehemu hizo ni Watu Wasio na UWEZO hivyo lazima TIKUBALI kuwa KULA UGALI dalili Kubwa ya UMASIKINI
JE kula chips?? Nadhan wewe ni kizazi kipya, acha watu wale chakul wanachokipenda
 
Back
Top Bottom