SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na madai kuwa ulaji wa ugali hudumaza akili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?

02692B18-05FE-4851-857F-7A5DA6E174CD.jpeg
 
Tunachokijua
Ugali ni chakula kinachotumika sana Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa utafiti wa Onu Okpa et al (2019), “Sub-Saharan African Maize-Based Foods - Processing Practices, Challenges and Opportunities” mahindi huchangia 30% ya nishati za vyakula wanavyotumia watu wa ukanda huu kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti huu, kila mtu anayepatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara hutumia wastani wa kati ya gramu 52-450 za mahindi kwa siku. Ni chanzo kikuu cha ugali unaotumika kila siku kwenye nchi hizi. Kwa Tanzania, 64% ya wananchi wake hula chakula hiki walau mara 5-7 kwa wiki.

Takwimu hizi zinaonesha kuwa ugali ni chakula kinachotumika sana, pengine kuliko aina nyingine za vyakula. Baadhi ya watu huutengeneza kwa kutumia unga wa mhogo, mtama, ulezi pamoja na aina zingine za nafaka.

Bila kujali tofauti ndogo za mgawanyiko wa virutubisho, nafaka zote husifika kwa kuwa na kiasi kikubwa cha nishati na wanga, pia kiasi kidogo cha madini na vitamini muhimu kwa afya.

Kuhusishwa na udumavu wa akili
Kitaalamu, udumavu wa akili husababishwa mambo mengi ikiwemo baadhi ya changamoto za kijenetiki mfano Down’s syndrome, kukosa hewa ya kutosha wakati wa kuzaliwa, maambukizi makali ya homa ya uti wa mgongo, utapiamlo, matumizi ya baadhi ya madawa na pombe wakati wa ujauzito pamoja na sababu zingine siziso wazi sana.

Kwa kurejea mgawanyiko wa virutubusho vinavyopatikana kwenye nafaka zinazotumika kutengenezea ugali, hakuna uhusiano wa moja kwa moja unaoweza kutajwa, au pia kuhusishwa na kusababisha udumavu wa akili kwa watu. Virutubisho na madini yake havina athari hasi kwenye afya ya ubongo.

Pia, JamiiForums imezungumza na wataalamu wa lishe ambao wamethibitisha kuwa chakula hiki ni salama, hakiwezi kusababisha madhara tajwa.

Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayana ukweli uliojengwa kwa hoja za kisayansi. Ni uzushi usio na uthibitisho wa tafiti au takwimu.
Kitu kibaya zaidi ni kwamba watu wengi wanakula ugali mweupe, unaotokana na mahindi yaliyokobolewa.

Kukoboa mahindi kunaondoa protini.

Ugali unakuwa na wanga tu.

Ugali wenye virutubisho ni wa unga wa dona. Unga wa mahindi yasiyokobolewa.
 
#Bring back our Ugali, Ugali ndio chakula kinachoshibisha vizuri. Ugali kwa mboga, maziwa safi sana. Ugali una nishati nyingi
 
Jamii Forums ilikuwa sehemu ya kukuta mijadala yenye akili, lakini recently imegeuka kijiwe cha wajinga wajuaji wanaosema wanachojisika instinctively kama wanyama bila ya critical and logical self judgment and analysis. Na hiyo sababu ni wajinga in the first place.

Najisikia kupoteza braincells kila navyosoma hizi comments. It's pathetic kujua watanzania ni wajinga kiasi hichi.

Sasa naelewa kwanini hata baada ya zaidi ya miaka 60 ya uhuru, Tanzania bado ni 3rd World Country. A country made up of retards.
 
Mbona naonaga wanigeria wana ugali fulani hivi mweusi
Ugali ni chakula kizuri sana. Tena mimi nazungumzia ugali wa mtama, uwele, ulezi na dona. Hata majuu siku hizi wengi wanakula mikate ''mweusi'' au brown. Haian tofauti na ugali wa mtama.
 
Wadau nawasabahi.

Umewahi kujiuliza ugali unaliwa sana na Watu wa aina gani? Utafiti mdogo nilioufanya sehemu nyingi iwe mitaa kwa Mama Lishe kwenye MAPUB au mabaa idadi kubwa ya Watu Wanakula UGALI ni Watu wa kiwango na Kipato cha CHINI. Tembelea Mikoani mpaka Vijijini UGALI ndio chakula kikuu kwa Watu Waishio huko.

Mfano wa Pili Mashuleni Hospital Magereza na Mahabusu za Polisi UGALI ndio Chakula kikuu na Wote wanakula UGALI ktk sehemu hizo ni Watu Wasio na UWEZO hivyo lazima TIKUBALI kuwa KULA UGALI dalili Kubwa ya UMASIKINI.
Acha kuandika pumba wewe. Ugali hauna mahusiano yoyote na Umasikini. Bali ni Culture Food. Ni kama Tambi ukienda Asia.
Na ugali unaliwa sana na watu wa hali ya chini sababu mostly ni chakula rahisi kuandaa na cheap vilevile.

Wewe unataka watu wale nini Tanzania? Ukilinganisha na uchumi mbovu tulionao?

Najua hauwezi kujibu hayo maswali sababu you're a fuking idiot.
 
Ni kweli kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe fala ni mjinga kinyama, kichwa kimejaa tope lakini bado unaendelea kutema pumba kwa kujiamini kabisa. Na hawa wapuuzi wanaokubaliana na huu uzi wako uliojaa kamasi wananifamya nihoji umri, elimu na uwezo wa akili walionao.

Inashangaza sana kuona wajinga wanajiami kupitiliza, Dunning Krugger Effect is real na wewe ni real life evidence.

Fuking pathetic.
 
Wadau nawasabahi.

Umewahi kujiuliza ugali unaliwa sana na Watu wa aina gani? Utafiti mdogo nilioufanya sehemu nyingi iwe mitaa kwa Mama Lishe kwenye MAPUB au mabaa idadi kubwa ya Watu Wanakula UGALI ni Watu wa kiwango na Kipato cha CHINI. Tembelea Mikoani mpaka Vijijini UGALI ndio chakula kikuu kwa Watu Waishio huko.

Mfano wa Pili Mashuleni Hospital Magereza na Mahabusu za Polisi UGALI ndio Chakula kikuu na Wote wanakula UGALI ktk sehemu hizo ni Watu Wasio na UWEZO hivyo lazima TIKUBALI kuwa KULA UGALI dalili Kubwa ya UMASIKINI.
Weee jamaa inaonekana hujaenda shule! Na kama ulienda hukukombolewa kifikra na wala hukupata maarifa. Tatizo sio neno "ugali". Ugali ni nini? Unaweza kuwa ugali wa ulezi, mtama, mahindi, n.k. Kwa wengi wetu tumezoea ugali wa mahindi. Ugali wa mahindi umejaa wanga. Kazi ya wanga ni kuupa mwili nguvu. Virutubisho vya kuongezea kwenye wanga vinapatikana kwenye mboga utakayotumia. Mwisho wa siku ukila ugali na mboga kama dagaa, nyama, mbogamboga unakuwa umeongeza protini na kufanya balanced diet! Acha kubeza ugali! Ugali ndo chakula kikuu cha watanzania na ndicho kilichotukuza! Acha dharau!
 
Madhara ya kula ugali moja wapo ni kutukana ovyo hata watu usiowajua

Badilisha mlo
Kula viazi,ngano, mihogo
Kwanini ufakamie hayo madawa ya kulevya yaitwayo ugali

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani katika yote niliyoandika, this is your fuking defense? Hiyo inabadili vipi ukweli wa nilichoandika?
 
Wewe fala ni mjinga kinyama, kichwa kimejaa tope lakini bado unaendelea kutema pumba kwa kujiamini kabisa. Na hawa wapuuzi wanaokubaliana na huu uzi wako uliojaa kamasi wananifamya nihoji umri, elimu na uwezo wa akili walionao.

Inashangaza sana kuona wajinga wanajiami kupitiliza, Dunning Krugger Effect is real na wewe ni real life evidence.

Fuking pathetic.
Ugali tu
Hadi unatukana kwa kiingereza
Acha ugali japo akili yako iwe kama ya binadamu wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wengi wanaamini ugali ndio chakula pekee cha kuupa mwili nguvu na afya njema lakini si kweli

Ugali ni mlo hatari ni kama sumu ndio maana hata wanyama wachoyo kama mbwa, nguruwe, paka, nk. Hawana akili lakini katu huwakuti wakila ugali maana ni chakula kisicho na nutrients zozote mwilini.

Hapa Tanzania jamii na makabila makabila makubwa hatupendelei ugali mfano sisi watu wa mkoa wa Kagera, Moshi(wachaga) na Mbeya hawali ugali lakini Tanzama mikoa duni kama Dodoma, Singida, Lindi, na watu wa Pwani wala ugali

Wenzetu wamataifa mengine wana afya afya na wala hawajui ugali ni nini Tazama wenzetu kutoka west Africa hawali maugali kama Watanganyika wana body zimejengeka.

Waganda, Wakenya, Wanyarwandwa hawali ugali. Mtu ukila ugali kwanza unalewa kama umepiga jibapa la Konyagi masaa mawili, ukila ugali wa Mara digestion ni ngumu mwilini chakula hakushuki hupati choo siku mbili, sasa hicho chakula au uchafu tu.

Wazungu na warabu wako vizuri kiafya wala hawayajui maugali ni nini wao wanajilia ngano, wali, nyama na maziwa, sisi Watanganyika kutwa usiku tunakula maugali na milenda kama tumerogwa

Madhara ya ugali kwa watu wetu, tumekosa washiriki wazuri kwenye michezo yani leo umpeleke Kibwana amkabe Sadio Mane AFCON haiwezekani.

Watoto hawana akili mashuleni wapo tu wamechoka yaani wamelewa chakali shuleni hawaewi kisa kula maugali.

Miili kama midogo kama digidigi unakuta mwanaume Dar anavamiwa na panya road anajificha kisa kula maugali

Sipendi ugali nakushauri usije ukala haya sumu ya akili na mwili ugali ni sumu kali

Nikiwa Rais nitapiga marufuku ugali

#kataa ugali Mtanganyika
Lete data za kisayansi ndugu, ugali una Carbohydrates, hii ni class ya chakula na ni nutrition unayoipata hata kwa kula wali, ndizi, au vyakula vya ngano.
 
Lete data za kisayansi ndugu, ugali una Carbohydrates, hii ni class ya chakula na ni nutrition unayoipata hata kwa kula wali, ndizi, au vyakula vya ngano.
Vitu vingine haviandikwi kirahisi kwenye vitabu

Sio kila maarifa unayapata vitabuni
Nimejitoa kama nabii kuwapeni siri zilizojificha, wewe unalazimisha nikuletee kurasa za vitabuni

Ugali unadumaza mwili, fikra, na ni sumu kali

Ni ngumu sisi waafrica kuwaza mapinduzi ya kisayansi katika kilimo, teknolojia n.k sisi tutawaza ushirikina, miujiza na ujinga mwingi

Haya yote sababu ya lishe duni iliyoletwa na wazungu iitwayo ugali hasa wa mahindi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
What is Fufu mkuu?? Tatizo ni kuwa umeridhika kushea sabuni ya kuogea na mume wa dada yako....
 
Back
Top Bottom