Maundumula
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 7,553
- 3,081
Afadhali ya Trump akiingia Biden na mtazamo wao wa kushoto haya mambo yakipelekwa white house ndio tutajuta.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nani aliyesema Tanzania ni kisiwa? Closed minds ni nyie mliolishwa kasumba kwamba hatuwezi kufanya chochote cha maana bila kuwategemea wazungu!Closed minds. TZ siyo kisiwa.
EU wameshayumba kiuchumi ni kama mbwa koko iliwafanikiwe kwasasa wanatuhitaji kuliko tunavyowahitaji,kama tunakusanya mapato ya 1.3Tril nini 70Bil wanayobweka fedha ya covid 19 safari hii wamegonga mwamba.European Union sio watu wa kukurupuka,wako slow lakini salama,hasa nchi za Afrika.
Hawataishabikia Tanzania kuvunja utawala wa Demokrasia lakini hawataiadhibu kama ilivyoadhibiwa Zimbabwe kwakuwa maslahi yaliwahusu wazungu wakulima wakipigiwa upatu na Uingereza.
Lakini utawala bora sio Demokrasia tu, kuna kudhibiti ufisadi, kukusanya kodi na kusimamia miradi kwa ufasaha. Kwa hayo mazuri ya Serikali ya Magafuli inaweza isichukuliwe hatua yoyote ya kuikwaza lakini wakiendelea kumshawishi afungue milango zaidi ya demokrasia.
Wazungu wa EU wanachojali Tanzania tokea enzi za Mwalimu Nyerere ni ikiwa amani itatoweka,lakini mengine ni subsidiary tu.
Mkuu hata Mugabe alianza vizuri sana akaja kumalizia vibaya,Shida ya Afrika ni wakubwa kujichukulia mali za umma pale wakisha kaa madarakani.
Tuseme tu ni viongozi wachache katika bara letu wanaoweza kutenganisha mali yake binafsi na mali ya umma akina Thomas Sankara, akina Edward Sokoine.
Ulaya na Marekekani wakibana na Marekani wakatumia influence yao kwenye mashirika kama Benki ya dunia, nchi hii miradi mingi itakwama na hata hiyo SGR na ujenzi wa Bwawa la Umeme vyote vinaweza kuathirika ikiwemo kukwama kabisa kwa miradi hiyo.
Hata kama fedha za hii miradi hazitoki Ulaya na Marekani, bado naamini support kubwa ya hawa tunaowaita mabeberu ndio inawezesha serikali kugharamia hiyo miradi kwa kuiongezea serikali uwezo wa kifedha kugharamia hiyo miradi sambamba na mambo mengine ya muhimu kama afya,maji,umeme.
Vile vile Benki ya Dunia-moja ya taasisi za fedha za kimataifa inayotukopesha- wametuwezsha kukamilisha miradi mingi ambayo CCM wanaitumia kujisifu: Ubungo interchange, soko la Ndugai kule Dodoma, Stendi ya kisasa Dodoma, n.k.
Kwakweli tuache kiburi na tuwe na shukurani kwani bila hawa watu tusingiweza kufanya baadhi ya mambo ambayo leo hii tunajisifu kuyafanya na zaidi tuache Kejeli za kuita hawa watu mabeberu ikiwa hata huduma za msingi kama elimu, afya na maji zinatushinda kuzitekeleza bila support yao.
Funguweni akili mgando hizo na muache kuwasujudu wazungu nao ni watu Kama nyie tu tofauti rangi tu.