Uchaguzi 2020 Ule mtaji wa 'vijana hawapigi kura' safari hii haupo

Uchaguzi 2020 Ule mtaji wa 'vijana hawapigi kura' safari hii haupo

Wakina mama wajasiliamali, bodaboda JPM alisha wakampata mapemasana 2016 wakati anaingia madarakani.
 
CCM wamekuwa wakitumia kasoro ndogondogo miongoni mwa wapiga kura kama mtaji wa kisiasa.

Kwa miaka na chaguzi kadha, imekuwa ikiaminika kuwa vyama vya upinzani vinapendwa na kujaza vijana katika mikutano yao lakini vijana hawa hawapigi kura pale muda wa kufanya hivyo unapowadia.

Dhana hii imetumika miaka na miaka lakini mwaka huu haifui dafu. wazee au watu wazima wa mwaka huu, ambao ccm imekuwa ikijivunia kuwa ndo wapigakura wake ndo kina sisi hapa. yaani wale vijana wa 1995, 2000, 2005, 2010 na hata 2015 ndo sisi hapa tushakuwa watu wazima na sasa CCM hawana pa kujificha tena. upinzani tunaenda kuupa kura. wazee wetu miaka 60, 70+ ni wachache na tushawaambia watulie tarehe 28 tuna jambo letu.

CCM wamepaniki. zile kauli za makamu wa rais kuwa hata tukipigia kura ccm lazima iunde Serikali ni dhahir kuwa wameshajua aina ya wapigakura wa safari hii.

Watoto wa shule wanaowajaza kwenye mikutano yao ni watoto wetu. wanawajaza ujinga mchana tunawatoa ujinga jioni. ccm isitegemee mtaji wowote wa kisiasa kutoka kwa watoto wetu. wanapoteza muda.

Kwa hiyo vijana wenzangu tuendeni tarehe 28 tukafanye yetu.

Kwa upinzani mwaka huu, ushindi ni saa 4 asubuhi.
Na kadi za kupiga kura tunazo
 
ukitaka kucheka waulize hao vijana kama walijiandikisha, hata wale waliojiandikisha walikuwa wanatafuta vitambulisho vya kusajili laini za simu na sasa hivi hawajuhi vitambulisho vyao vilipo! Hata kuhakiki niliowaona wanahakikiwa walikuwa akina mama na wazee...upinzani sijuhi ni kwa kutojua au ile staili yao ya zimamoto kwanini hawakuwahimiza wanachama wao kuhakiki taarifa zao!
 
Hata mm nilipokuwa kijana nilikuwa nashabikia upinzani ila kadiri nilivyokuwa nazeeka nilitambua Nchi hii sio ya kuwapa Wapinzani kwani nikuturudisha kwenye ukoloni wa kizungu.Na pia kadiri mtu anavyokuwa anajitambua, hao unaosema walikuwa vijana ndo sisi tutakipa chama cha Mapinduzi kiongoze Nchi kwa misingi ya Ujamaa na kujitegemea
Dogo, bado unaota ujamaa..!! uko sayari gani? Huenda uko dunia ya wafu. Msalimie Mwl. Nyerere na Kwame Nkrumah[emoji1787]
 
Back
Top Bottom