Ulevi Unaninyima Amani. Ninaomba Msaada wenu

Kwani nyie wenzetu hizo pombe mnakunywaje?
 
Ukiona unahangaika kuacha pombe maana yake nguvu ya Mungu inakuondoa ktk hilo janga la ulevi... Ni jambo si rahisi kwasababu shetani pia anataka uendelee kuwa mtumwa wa pombe...
Anza kufanya ibada mida ambayo huwa unapenda kunywa fanya ibada au soma maandiko ya Mungu... Epuka kuitwa au kuwa karibu na watu walevi wanaokushawishi...
Haitakuwa rahisi ila Mungu ni mwema soon utashuhudia ukuu wa Mungu...
Ktk yote usijutie maisha ukayaona mabaya, hayo ni mambo ya kawaida ktk maisha hutokea cha msingi focus ktk kujijenga upya kiafya kiakili na kiuchumi...
Kuna watu walikuwa walevi leo ni viongozi wakubwa tu wakuheshimika cha muhimu ni kukubali kubadirika
 
Kunywa nyingi kabisa
ukipata pesa kunywa tena
ukifukuzwa kazi ukipata kazi nyingine nenda umelewa
ukifika toroka kazini nenda kalewe
ukitoka kazini kalewe yani wewe kunywa mpaka pombe zikuogope zenyewe hapo utaacha
Nao ni ushauri, lakini siwezi nikaufanyia kazi.
 
Pole sana ndugu, ushauri wangu ni kwamba

Tazama video hapo chini Uielewe vizuri kisha

Kila siku iendayo kwa Mungu, hakikisha umeamka saa 1030AM(kumi unusu alfajiri) ufanye mazoezi .
Usinywe pombe kila unapojiskia, anza kunywa pombe ukiwa unajipongeza/motive baada ya kufanikisha/ kukamilisha jambo fulani, mf umefanikiwa kununua TV, umefaulu mtihani nk


View: https://youtu.be/-w8n9UOiBxE?si=T6FNM-svwpPJQCCA
 
Kwa kuwa ni ngumu kuacha kwa mara moja Anza kupunguza idadi ya chupa za Pombe.

Halafu punguza marafiki wanaokunywa sana pombe.

Kuwa busy na shughuli zako.

Punguza matumizi ya simu.

Kunywa Maji Mengi.

Penda sana kunywa nyumbani wakati mwingine.

Hama mahali ulipozoeleka hamia sehemu mpya.

Zungumza na marafiki wapya wenye mtizamo tofauti.

Soma vitabu.
 
Wote walioamua kuipa pombe uwezo na nguvu ya kuamua mda na wakati wa kuwapumzishia akili, wapo nyumba za rehabilitation

Usiruhusu kunywa pombe kama sehemu ya kupunguza mawazo au kutaftia amani, ukifanya ivo jua umeishaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Shida ya waTz ni

Ukiamua inawezekana
Amua uache
Nenda kanisani katubu dhambi

Chief, nenda kwa Afisa Ustawi yeyote wa eneo lako mwambie kwamba una addiction na pombe na unahitaji kwenda rehab.

Atakupa ushauri yeye kwanza kisha atakuunganisha na watu wanaofanya hizo kazi kama sehemu ya maisha yao.
 
Naomba msaada wenu wote ili niweze kushinda vita hii dhidi ya pombe. Ninatafuta ushauri juu ya jinsi ya kuacha
Mlevi unaandika vizuri hivi wewe sio mlevi, ungeandika kilevilevi ningekuelewa ila hivi ulivyoandika wewe sio mlevi kabisa wewe mnywaji
 
Mpe Yesu maisha yako, yeye anao uwezo wa kuondoa kiu ya pombe iliyopo ndani yako.
 
Kitu Cha kwanza, badirisha marafiki. Jitahidi uwe na marafiki wasiokunywa pombe. Kisha Anza kuutafuta usu wa Mungu. Mimi hizi mbinu zilinisaidia sana kipindi nalewa nikiwa Karagwe.
 
Mau ya muwa ulochanua ni tiba unayachemsha kama n mengi au kama upatikanaji wake n mdogo basi unayaanika unasaga Sasa ule unga wake unakuwa unautia kwa chakula, mboga, maji au chochote unachokula au kunywa
 
Ushauri wa hovyo. Unamtaka aruke tope akanyage kinyesi
Huo ushauri ndio utafanya kazi!
Tabia hubadilishwa kwa tabia

Ni ufinyu wako wa uelewa tu unakupelekea kudhani labda uraibu unaweza tibika kirahisi kwa kuiizuia au michezo!!…..


Toa uo utoko kichwani
 
Change ur circle and people you hang out with

Maintain this formula

PPT
People
Place
Things

P -don't hang out with alcoholic people

Place - don't go club , bar , and so on

Things - punguza aina ya vyakula vinavyochochea wewe kutumia pombe pia punguza mawazo yanayochochea wewe kutumia pombe.

Unaweza jaribu hizo mbinu then ukaona how it is work.

Pia replacement -mfano ikiwa unapata shida kuacha pombe anza na kupunguza idadi

Mfano ulikuwa unakunywa bia 5 anza kunywa 03 baadae mbili na baadae 1

Hizi mbinu zote zinaweza kukusaidia au zisikusaidie kutoka na wewe umeamua kujiona wapi.
 
Jambo la kwanza mtegemee Mungu. Pili acha marafiki wote mara moja, tatu nenda kwa wataalam wa afya ya akili. Nne kunywa vimiminika tofauti wakati unahisi kiu, kama maji, maziwa tangawizi na mchai chai. Tano soma vitabu vya kiroho au Biblia ama Quran kulingana na Imani yako. Sita usikose ibada kama ni Jumapili, au msabato jumamosi au ijumaa kama ni muislam. Saba na mwisho lala usingizi wa kutosha zaidi ya 8 hours.
 
Me naweza amua kuacha pombe hata miaka miwili na nikaweza
 
Pole sana mkuu
Wapige chin marafik wanao kupa pombe
Nenda kanisan omba mungu utapata Aman
Pendelea kufanya vitu vinavyo kupa furaha
Tafuta marafik watakao kupa ushaur mzur
Kingine mtafute mwana saikolojia
Utakuwa sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…