mapipando
JF-Expert Member
- Jun 8, 2015
- 2,922
- 3,559
Habari wanajamvi,
Kumekuwa na desturi ya watoto kudanganywa aidha na watu wazima ama na watoto wenzao kwa malengo tofauti tofauti. Mfano kuogopeshwa tu au kutotakiwa kufanya jambo fulani.
Mimi nilidanganywa kuwa
1. Eti kama mvua inanyesha halafu ukawa unakimbia basi maji yote ya bahari yatakuja na kujaa mahala pote kiasi kwamba nyumba zitasombwa.(Dar)
2. Wanajeshi ama polisi wa kike kazi yao ni kuwapikia wanajeshi ama polisi wa kiume.
3. Mwanaume ukila chakula kwenye chungu ama sufuria utachelewa kuoa ama hutooa kabisa
Wewe ulidanganywa nini?