Uliambiwa nini ukiwa Mtoto lakini baada ya kukua ukagundua ni Uongo?

Uliambiwa nini ukiwa Mtoto lakini baada ya kukua ukagundua ni Uongo?

hao wachawi wenye uwezo mkubwa waende Bank wakaibe pesa kichawi. Kwanini wanashindwa.?
uchawi ni mambo ya kiroho! Na mchawi hamind sana pesa... Hata hvo hata bank nazan kuna mkono wa uchawi au kinga dhidi ya uchawi
 
uchawi ni mambo ya kiroho! Na mchawi hamind sana pesa... Hata hvo hata bank nazan kuna mkono wa uchawi au kinga dhidi ya uchawi

kama bank wanajenga kwa uchawi na kafara kwanini wanaweka ulinzi na ma camera? Kwanini wasitumie uchawi kulinda mali zao?

Dhana ya kuamini uchawi upo ni mambo ya kufikirika zaidi na sio uhalisia,kwa mfano ni vigumu sana kwa daktari kuamini kwamba mtu anaweza akaugua kwa sababu ya kulogwa, vilevile ni vigumu accountant akaamini biashara yake haiendi vizuri kwa sababu ya uchawi.

Ila daktari anaeamini uchawi anaweza kuamini biashara yake ya duka la dawa haitoki kwa sababu ya uchawi, na accountanta anaeamini uchawi anaweza akaamini mtu anaweza kuugua kwa sababu ya kulogwa.
 
Wanatumia ulinzi na camera kwa niaba ya wezi wa kawaida, alaf bank ni vitu vya kistaarabu, lakin uchawi loo...
 
Nilipokuwa namaliza LA saba, in 90s, jamii ilituaminisha kuwa sie LY(tunaohitimu) ndio tumemaliza kila kitu, sasa, tu relaxy!laiti tungeambiwa kwamba hata kuifikia hatua ya, elimu bado sana, maaana mpaka nilipotoka UDSM ndio niliamini nimemaliza, hatua ya kwanza, ya elimu,
Kibaya ambacho bado jamii inaendelea kuwaambia vijana kuwa, wasome ili waje waajiliwe, kwenye nchi yenye uchumi mbovu kama hii!
 
Uki ng'oa Jino lazima ulitupe juu ya bati.

Usipo tupa halioti.
Sie tuliambiwa lazima ukalitupe uvunguni mwa kitanda tena ukiwa umeinama ulilushe kupitia katikati ya miguu,na huku unaimba wimbo kumwambia panya alichukue akupe jipya!
 
Tuliambiwa soma kwanza, huko mbeleni utalala mpaka uchoke. Ila naona kila nikisogea huko mbeleni ndiyo masaa ya kulala yanapungua zaidi.
[emoji16][emoji16]

Mimi nilijisemea nikimaliza chuo nitalala sana. Saiv bora hata ya chuo nilikua naweza kudoji vipindi nikaenda kulala
 
Back
Top Bottom