Uliambiwa nini ukiwa Mtoto lakini baada ya kukua ukagundua ni Uongo?

Uliambiwa nini ukiwa Mtoto lakini baada ya kukua ukagundua ni Uongo?

Nilidanganywa vingi...
Nilikuwa napenda sana kulia lia hovyo pengine kitu kidogp nalia,niliambiwa nkilia usiku ni kuita wachawi na wataondoka na sauti yangu nitakuwa bubu. Nikaacha habari za kujiliza Liza na madeko

Kingine kula muhindi unaambiwa njoo nikuwekee njia ya kwenda kwenu (wanamtaka origin yako huko)
Nimetengenezewa njia hatari,usiombe umkute mtengeneza njia ni mlafi mbona utajuta anapiga nusu hindi badala ya njia mbili tu loh
 
Mama alinambia hivi "nilikununua hospital, niliona watt weeengi ila nilipofika kwako tuu,ukanichekeaaa nami nikafurahi na kukuchekea pia,nikakuchua ukawa mwanagu mzuuuri hadi Leo"... Looh niliamini eti nimenunuliwa hospital mpaka nipokuja kujua hahahhaha so funny

Ukimchungulia MTU mzima unapofuka macho[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] n.k
Ha ha ha ha ha bila shaka na wewe umeshanunua watoto kadhaa mkuu
 
Mama alikuwa akimpata mdogo wangu alikuwa ananidanganya kuwa ameenda kumnunua sokoni!.....Hadi nafika la saba nilikuwa nafikiri kuwa watoto huwa wananunuliwa sokoni!!
 
Kuvunja ungo inamaanisha hivohivo kuchukua ungo na kuuvunja
 
Uncle wangu alinidanganya kiwiliwili cha kumbikumbi kimejaa usaha, imeniathiri hadi leo hii sili kumbikumbi!
 
[emoji736] Nilidanganywa ukikalia kinu kinakunasia makalioni

[emoji736] Nilidanganywa kama umelala chini mwenzio akikuruka huwezi refuka utakua mfupi hivyo hivyo

[emoji736] Nilidanganywa ukinyoosha kidole makabulini kinakauka hadi uking’ate

[emoji736]Nilidanganywa uking’oa jino ukalitupa chini pale kwenye pengo pataota jiwe

[emoji736] Nilidanganywa mwenzio akikung’ata pakaa mavi ya kuku ataoza meno

[emoji736] Nilidanganywa ukikojoa porini au sehem sio rasmi temea mate kwani nyoka akilamba ule mkojo dudu itavimba

[emoji736]Nilidanganywa ukila sukari nyingi kwenye chai unapata kisukari


[emoji324]Nahisi ni mimi pekee ndio nitakua nilidanganywa vingi sana nilipo kua mtoto.

Nashukuru sikuwahi kudanganywa juu ya uzaliwaji wa watoto maana nilikua mtata sana ktk hayo mambo haha
 
Back
Top Bottom