Uliambiwa nini ukiwa Mtoto lakini baada ya kukua ukagundua ni Uongo?

Uliambiwa nini ukiwa Mtoto lakini baada ya kukua ukagundua ni Uongo?

Nilidanganywa yafuatayo:
1. Tanzania ni nchi masikini
2. Wanaume wa Dar ndiyo wanaume wa kweli
3. Mwanamke akila kichwa cha mbuzi na samaki hawezi zaa
4. Mwanamme ukila chakula kwenye chungu unakosa nguvu za kiume kama wanaume wa Dar.
 
Mimi nilidanganywa ukikutana na mtu mwenye albinism basi jitemee mate ndani ya nguo ulio ivaa nguo ya juu t-shirt usipo fanya hivyo......
 
Nilidanganywa kua nikikojoa niteme mate nilipokojolea, kama sikutema mchawi akipita Mama atakatika maziwa.

Mpaka leo natema nilipo kojolea..
 
Ndugu mkikojoa sehemu moja,Ziwa la mama linavimba.



Kila MTU anavaa pichu had MMASAI
 
Nilidanganywa nisipo oga usiku shetani ana pembe kichwani na ulimi wa moto atakuja kunilamba mwili mzima asubuhi nitaamka msafi kwa kulambwa huko.

Kumbe uongo uchafu unaishia kwenye shuka nilikuwa siachi kuoga usiku hata iwe vipi [emoji28][emoji28][emoji28]

Niliambiwa nisipopiga mswaki mara tatu chakula kinachotakiwa kutoka kama kinyesi kinarudi mdomoni ndio nitanuka mdomo kama kinyesi hadi leo nashindwa kuacha kupiga mswaki mara mbili

Ya mwisho kali ni kuwa baba na
Mama wanalala chumbani peke yao na wanajifingia mlango kwa sababu wanakazi ya kuhesabu pesa nyingi sana ili majambazi wasiwaone. Kumbe wana kazi ya kuongeza familia [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom