Uliambiwa nini ukiwa Mtoto lakini baada ya kukua ukagundua ni Uongo?

Uliambiwa nini ukiwa Mtoto lakini baada ya kukua ukagundua ni Uongo?

Uncle wangu alinidanganya kiwiliwili cha kumbikumbi kimejaa usaha, imeniathiri hadi leo hii sili kumbikumbi!
Dah hadi nimejawa na mate halafu pa kuyatema sina duh (bad image)
 
Nikidanganywa acacia watatulipa kishika uchumba trillion 400,nimepata akili kumbe ulikuwa ni uongo
 
Mama yangu alinidanganya eti Mtoto anazaliwa kupitia kwenye Dole gumba .
 
Ulikuwa unaonekana mwehu mno ndyo maana ulidanganywa ivyo
 
[emoji736] Nilidanganywa ukikalia kinu kinakunasia makalioni

[emoji736] Nilidanganywa kama umelala chini mwenzio akikuruka huwezi refuka utakua mfupi hivyo hivyo

[emoji736] Nilidanganywa ukinyoosha kidole makabulini kinakauka hadi uking’ate

[emoji736]Nilidanganywa uking’oa jino ukalitupa chini pale kwenye pengo pataota jiwe

[emoji736] Nilidanganywa mwenzio akikung’ata pakaa mavi ya kuku ataoza meno

[emoji736] Nilidanganywa ukikojoa porini au sehem sio rasmi temea mate kwani nyoka akilamba ule mkojo dudu itavimba

[emoji736]Nilidanganywa ukila sukari nyingi kwenye chai unapata kisukari


[emoji324]Nahisi ni mimi pekee ndio nitakua nilidanganywa vingi sana nilipo kua mtoto.

Nashukuru sikuwahi kudanganywa juu ya uzaliwaji wa watoto maana nilikua mtata sana ktk hayo mambo haha
Wote tumedanganywa vingi mkuu,na vingi vinafanana fanana...teh
 
Nilidanganywa eti ukinyoshea kidole upinde wa mvua unakumeza, ukilala chali wakati inanyesha mvua ya radi inakupasua tumbo
 
Back
Top Bottom