Ulianzaje kukaa gheto?

umetumia bei gan kuset huo mkito?
 
Kwanza kabisa niseme wadogo zangu ambao bado mnakula ugali wa shikamoo. Hakuna kama raha kumiliki ghetto lako aseee, usiogope maisha anza kujipanga mdogo mdogo. Nunua godoro lako na jiko lako la gesi inatosha sana kuanza maisha shida wengi wanataka aanze na geto lina kila kitu.

Anza taratibu vitu vingine vinakujaga taratibu, na hapo sasa utakua umeanza pata akili ya Maisha, usikubali ufikishe miaka 25 bado upo kwenu afu mtoto wa kiume. Kama unakaa home trust me wazazi wako lazma wawe na mashaka na wewe.

Mtoto wa kiume kapambane na maisha huna kazi tafuta kazi, ukipigwa na maisha rudi home wakuboost unasepa uanendelea na kupambana utatoboa tu mbna, hata wazazi watakuombea sana wataona wana kijana mpambanaji.

La mwisho usipange gheto ukiwa na mawazo ya kugongea mademu humo akili yako itakua hvohvo na usikubali kuingiza wanawake wasiojoelewa kwenye nyumba/ gheto lako. Kupanga geto ndo mwanzo wa maisha ya kujitegemea mpaka unajenga yako.

Next time nitaleta uzi maisha yangu ya gheto yalianzaje[emoji120]. Msikate tamaa madogo mtafika tu huku.
 
Broo hata kama utakosa Bando nipo tayari kukupatia vocha ya buku ili ushushe madini Hapa!!
 
Brother...Nakuomba hiyo next time iwe leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…