1st time nasoma hii thread nilikua nakaa kwa bro baada ya kumaliza chuo (2018),nilikua intern kwenye moja ya processing plants huko Geita.
2019 mwishoni bro akawa anavuta jiko hivo kwa kunionea huruma akaniachia baadhi ya vitu kama kitanda na sofa moja la watu wawil na tv 24",ila asikwambie mtu unapiga intern hulipwi cha maana zaidi ya nauli na kuambulia kula hapo kazini,mambo yakawa tight kinoma kodi ikaanza kupiga chenga,nikiwaza kurudisha mpira kwa kipa naona jau,nikaamua kupambana hivo kwa msaada wa bro(kumpiga vizinga vya hapa na pale)
Mungu mkubwa 2021 mwanzoni nikawa nimeitiwa kijinafasi cha kujishkuza kwenye moja ya machimbo mikoa ya kusini,hapo ni mimi na kibegi changu cha mgongonj shuka la kimasai la kujifunika,PC yangu na simu nokia kitochi maana hata Samsung niliotoka nayo chuo nilishauza kwa wakati huo kupunguza ukali wa msoto.
Hapo machimboni nilikua naishi kibishi sana,unalala sehemu wanaziita matanda (watu wa migodinj wanaelewa),nimeweka turubai na kuzungushia kibanda mianzi,afu godoro la sufi nilinunua Nachingwea town Tsh 15k.Sikuwahi hata siku moja kujikweza na kujionaa labda m ni graduate nna ki degree,sasa katika kufahimana na watu,nikaanza kupata deals za kuchenjua (ndio taaluma yangu) kwenye processing plant kama mkemia.Hela ya kwanza ya maana kupata nikapanga chumba Nachingwea mjini,nikanunua smart ili nirudi mjini maana mambo nowadays yako digitalized,godoro na mkeka na kiredio cha bluetooth life likaanza.
View attachment 2280060
Kupitia hio nafasi hapo machimboni niliweza pia kujuana na watu wengi sana na kupitia hao watu nikafanikiwa kupata kazi (yenye maslahi mazuri kwa upande wangu) na kwa sasa walau nauona mwanga,nipo ghetto napambania kombe taratibu,weekends kama hivi unashinda unacheza games plus movies maana msimu wa football ndo umeishia hivo.
NB:Kukata tamaa na kurudisha mpira kwa kipa haipaswi kua option yako no 1.Jah Bl