Ulianzaje kukaa gheto?

luchelele mzunguko,mnangani mzunguko[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ilinichukua muda sana kujua hiyo mzunguko Ina maana gani maana nilikuwa najua Kuna sehemu inaitwa mzunguko.
Kumbe hiyo mzunguko ni Ile inazunguka pale samaki.
Mi ndo nimejua sasa baada ya kusoma hapa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Wakuu kampuni gani ya feni pangaboi ni nzuri na inadumu? Na bajet yake please maana haya mafeni ya chini naona kila mwaka nanunua jipya
 
Safi sana Mkuu izi ndo inshu za kujadili zinaleta motisha kwa sisi vijana tunapambania ndoto, Sio kupoteza mda tunajadili mada za kupiga Nyeto
 
Nyakati za ghetto ni za kupanda na kushuka, rightfully ukomae tuu, hakuna namna.
 
Nimekua nikiufuatilia huu uzi tangu nipo shule mpaka nimeajiliwa kwenye kampuni fulani hapa jijini Dar na ninaishi nyumbani lakini ni muda sasa wa kwenda kupanga ila changamoto kila chumba ninachopelekwa na madalali hakina sifa ninazozihitaji mimi yaani sijui wenzangu mnatumia mbinu gani ya kupata magheto makali
 
Ghetto hua kali kutokana na level ya uchumi wako, ko kupata ghetto ni vile tu kutokana na uchumi wako pia kutokana na mazingira, uswahili kuna maghetto ya bei chee lakini ni ya kawaida tu. Hivyo maghetto makali ni kawaida kua yana maeneo fulani lkn bei hua ni ghali pia.
 
Hii ni kwetu wanangu wa Maghetton!

Tusisahau kusave kila tunapopata mkwanja,hata kama umepata buku ten fanya saving walau ya buku sio mbaya. Jambo lingine na muhimu zaidi,ni kuwekeza katika kitu ambacho una ujuzi au ufahamu nacho kiundani,itapendeza zaidi kitu hicho kiwe kinagusa kwa namna moja au nyingine katika shughuli zako za kila siku.
Hapa namaanisha,mfano mimi msimamizi wa masuala ya mbao,basi mara moja moja nanunua miti kadhaa,au sometimes nanunua mbao kadhaa na kuziuza.
Kwa mfano ukiwa fundi katika workshop ya mtu,unaweza kununua hata MDF-Boards zako,au bawaba,handles,nob,n.k na kuwauzia baadhi ya mafundi wenzio.

Hivyo hivyo hata ukiwa dukani,kama bosi sio mkuda weka hata mzigo wako pale unapoona boss hajaleta mzigo kwasababu either kakwama au lah.
Muhimu ni pesa izunguke.

La mwisho na kubwa zaidi,usisahau kuwapa watu wenye uhitaji,toa msaada kwa watu wanaohitaji,mfano masikini,wazee,watoto yatima,n.k. Wakuu hii issue ya kutoa ni zaidi ya ndumba,milango mingi sana ya kimafanikio hufunguka. Mtu anaposhukuru kuna kitu kikubwa sana unapata. Mtumie hata Mshua, Mother au madogo chochote kile bila kujali uko katika hali gani.


NB: Pahala ambapo unaamka kila siku kwenda kusaka mkate wa kila siku ni pahala muhimu na nyeti sana.
So, Ghetto liheshimiwe,na si kila mtu anapaswa kulazwa ghetto kwako.

Tuendelee kupambana wanangu wa damu,JAH bless us![emoji109]
 
Yeah umenena vyema kabisa, hii ya kuweka vitu na kuwauzia umenipa darasa kubwa sana. Maana nafanya kazi ya drilling na blasting explosive hua tunanua ghalani, sijawahinkuwaza kununua vingi kuvisave kwa ajili ya kuuza nikipata kazi.
 
Yeah umenena vyema kabisa, hii ya kuweka vitu na kuwauzia umenipa darasa kubwa sana. Maana nafanya kazi ya drilling na blasting explosive hua tunanua ghalani, sijawahinkuwaza kununua vingi kuvisave kwa ajili ya kuuza nikipata kazi.
Shukrani sana ndugu.
Mkuu,katika shughuli zetu hizi za kila siku kuna chances kadhaa ambazo tukizitumia vyema hatukosi hata pesa ya kupaulia[emoji28].
 
Yeah umenena vyema kabisa, hii ya kuweka vitu na kuwauzia umenipa darasa kubwa sana. Maana nafanya kazi ya drilling na blasting explosive hua tunanua ghalani, sijawahinkuwaza kununua vingi kuvisave kwa ajili ya kuuza nikipata kazi.
Mfano wewe waweza kununua vingi na kuwauzia wahitaji,si lazima wao waende kuvitafuta mbali au wewe ukavisake kipindi unafanya hiyo kazi. Waweza kuwa nazo hizo materials muda wowote kisha kuziuza wakati zinahitajika,na baadae inaweza kuwa biashara yako nyingine kubwa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…