WANA WA MAGHETTONI NIAJE !!!??
Jaribu kuwekeza kwenye engine (mashine) katika uzalishaji wako.
Hapa nazungumzia kwa sisi ambao tuko maghetto na hatuja ajiriwa yaani tunapambana tu wenyewe. Pia kwa wale ambao vichwa vyetu haviwezi biashara za kuuza bidhaa direct hasa za duka mfano kuuza duka au genge. Unajua sio wote tuna huo uwezo (mfano mm nikiwa na genge watoto watamaliza pipi zote na biscuits plus juice, maana napenda sana watoto wananiita anco wa mtaa)
Twende pamoja sasa maana siko viziri katika kuelezea, na nitakacho kieleza sio kigeni kabisa ila ni life experience yangu ya vitu nilivyofanya na ninavyoendelea kufanya hivyo napenda kushare vitu kidogo humu kuna watu vinaweza kuwasaidia kidogo, si unajua wana kupeana michongo.
Swali.
Je ni engine gani (mashine gani) ukiipata unaweza kutoboa maisha!!?????
Naamini ukifikiria hilo swali vizuri ndo utaanza kupata mwanga wa kile ninacho tamani kukuambia au kukuelezea. Fikiria kitu au kifaa cha kutendea kazi zako ambacho ukikipata unaweza kubadilisha maisha kimtindo kwa kukuongezea uzalishaji na kukuongezea kipato.
Nashauri kama kuna mishe unafanya ya uzalishaji na inakupa kipato (hasa uliyojiajiri mwenyewe) jaribu kuiwekezea kwenye mashine yake ikusaidie katika uzalishaji, inaweza kuku saidia kuongeza kipato.
Mifano iliyo hai.
1)kama ni mkulima mdogo ukiongeza pump ya kumwagilia na mashine ya kupalilia unaweza kuongeza kipato kimtindo maana bustani yako au shama lako litakua la kilimo mda wite mpaka kiangazi. Hivyo naamini uzalishaji utaongezeka. Nimepitia hii kipindi niko form 3 mzee alikua na mwanameka pump unakanyaga na miguu, ilisaidia kumwagilia nyanya kiangazi( Njombe-makambako). Saivi hazitumiki sana kwasababu zipo za petrol na diesel kwa wingi.
2) Kwa wavunja mawe.
Huku sasa ndio niliko jiwekeza mm. Kama unafanya kazi ya kuvunja mawe na kuuza basi nisikilize vizuri kwa sababu mm ndiko niliko na experience kubwa nimeipata hapo.
Ukiwa na compressor mashine ya kutobolea miamba itakusaidia sana tena sana kwenye shughuli nzima. Issue ni kua ina bei kubwa kidogo. Lkn kwenye uzalisha imenisaidia sana kuanzi milioni 8 na kuendelea.
View attachment 2422779View attachment 2422781View attachment 2422778View attachment 2422788
3). Kuponda kokoto.
Pia kama ww ni mpondaji wa kokoto unaweza kuongeza stone crusher katika kazi zako. Sio lazima liwe kubwa hada dogo la kuzalisha cubic metre 8 kwa siku linatosha sana kujipatia kipato. Tena unaweza kununua used mtaani kwa gharana nafuu (lkn likiwa spana mkononi sana utajuta).
View attachment 2422790View attachment 2422792View attachment 2422791
4). Chain saw ya kukatia miti. Kwa wale wanaoishi maeneo ya upasulishaji mbao wanajua hii kitu umuhimu wake. Bei yake nafikili ni kuanzia milioni 1.7 mpaka 2 na kuendelea. Hii unaweza kununua na ukampa kijana akakuletea mauzo yake au unaweza kukodisha. Ukimpa kijana kwa wiki anakuletea tsh. 70000 au 60000. ila kama ukiishika mwenyewe utapiga hela zaidi. ( ila sasa maisha ya pori yatakuhusu kwasababu hakuna miti mjini).
View attachment 2422799
5) Kwa vijana waliopita garaje, air compressor za kujazia upepo kwenye magari na mashine ya ku-apply grease (grease pump) itakua ni option nzuri kwako. Unaweza kuweka nje ya sehemu unayofanyia kazi au ukaweka sehemu nzuri kwa biashara na ukaingiza shilingi miamia daily, sio mbaya sana kijana ukawa na kakitega uchumi pembeni. Hivyo vifaa unaweza ku afford kama mpambanaji haviuzwi ghali sana.
View attachment 2422806View attachment 2422807
6). Kama unaosha magari kwa mkono kwa nini usinunue jet washer (pressure washer). Kwanini usijaribu kununua jet washer uongeze uzalishaji wako na ufanisi wa kazi yako.
View attachment 2422813View attachment 2422814
7). Kwa wanaofua nguo(Dobi). Unaweza kuongeza mashine ya kufulia nguo drycleaner itakayo kusaidia kufua nguo nyingi kwa wakati mmoja na kwa uhakika zaidi wateja wako wakafurahia kazi ya mikono yako.
View attachment 2422819
Wadau, unajua kuna kazi ni za kawaida tu, lkn ukiziongezea uzalishaji kwa kutumia mashine husika unaweza kuongeza uzalishaji na kipato ukaishi viziri tu. Kuna mda mda mchawi anakua pesa ila kuna mda mchawi ni ww mwenyewe hujajiwekeza kwenye kazi yako mwenyewe. Basi tuanze kufikiria kuwekezea ipasavyo kwenye mishe tunazo fanya.
Asanteni sana, mtanisamehe kwa uandishi mbovu. Na nimeandika kwa experience yangu mwenyewe kupitia ideas za mtaani tu, so am very sorry if i offended you through this.
Pia nilitamani nimpate mwana jf mmoja humu ambae yupo ghetto na hajabanwa sana na michongo yake aje niliko tufundishane ideas mbalimbali. Atakaa kwangu kwa wiki moja au mbili hivi na nauli nitamtumia go and return. (kwa urafiki tu sina nia mbaya). Kwangu utajifunza biashara ya mawe na kokoto pia utajifunza matumizi ya explosives hada baruti na AMFO.
THANKS VERY MUCH (my names LUHANGA ATUKUZWE) from Makambako Njombe.
atukuzweluhanga@gmail.com
Facebook. Atukuzwe Luhanga
Phone. 0765135468.