Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

luchelele mzunguko,mnangani mzunguko[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ilinichukua muda sana kujua hiyo mzunguko Ina maana gani maana nilikuwa najua Kuna sehemu inaitwa mzunguko.
Kumbe hiyo mzunguko ni Ile inazunguka pale samaki.
Mi ndo nimejua sasa baada ya kusoma hapa 😂😂😂😂
 
Wakuu kampuni gani ya feni pangaboi ni nzuri na inadumu? Na bajet yake please maana haya mafeni ya chini naona kila mwaka nanunua jipya
 
WANA WA MAGHETTONI NIAJE !!!??

Jaribu kuwekeza kwenye engine (mashine) katika uzalishaji wako.

Hapa nazungumzia kwa sisi ambao tuko maghetto na hatuja ajiriwa yaani tunapambana tu wenyewe. Pia kwa wale ambao vichwa vyetu haviwezi biashara za kuuza bidhaa direct hasa za duka mfano kuuza duka au genge. Unajua sio wote tuna huo uwezo (mfano mm nikiwa na genge watoto watamaliza pipi zote na biscuits plus juice, maana napenda sana watoto wananiita anco wa mtaa)

Twende pamoja sasa maana siko viziri katika kuelezea, na nitakacho kieleza sio kigeni kabisa ila ni life experience yangu ya vitu nilivyofanya na ninavyoendelea kufanya hivyo napenda kushare vitu kidogo humu kuna watu vinaweza kuwasaidia kidogo, si unajua wana kupeana michongo.

Swali.
Je ni engine gani (mashine gani) ukiipata unaweza kutoboa maisha!!?????

Naamini ukifikiria hilo swali vizuri ndo utaanza kupata mwanga wa kile ninacho tamani kukuambia au kukuelezea. Fikiria kitu au kifaa cha kutendea kazi zako ambacho ukikipata unaweza kubadilisha maisha kimtindo kwa kukuongezea uzalishaji na kukuongezea kipato.

Nashauri kama kuna mishe unafanya ya uzalishaji na inakupa kipato (hasa uliyojiajiri mwenyewe) jaribu kuiwekezea kwenye mashine yake ikusaidie katika uzalishaji, inaweza kuku saidia kuongeza kipato.

Mifano iliyo hai.

1)kama ni mkulima mdogo ukiongeza pump ya kumwagilia na mashine ya kupalilia unaweza kuongeza kipato kimtindo maana bustani yako au shama lako litakua la kilimo mda wite mpaka kiangazi. Hivyo naamini uzalishaji utaongezeka. Nimepitia hii kipindi niko form 3 mzee alikua na mwanameka pump unakanyaga na miguu, ilisaidia kumwagilia nyanya kiangazi( Njombe-makambako). Saivi hazitumiki sana kwasababu zipo za petrol na diesel kwa wingi.

2) Kwa wavunja mawe.
Huku sasa ndio niliko jiwekeza mm. Kama unafanya kazi ya kuvunja mawe na kuuza basi nisikilize vizuri kwa sababu mm ndiko niliko na experience kubwa nimeipata hapo.
Ukiwa na compressor mashine ya kutobolea miamba itakusaidia sana tena sana kwenye shughuli nzima. Issue ni kua ina bei kubwa kidogo. Lkn kwenye uzalisha imenisaidia sana kuanzi milioni 8 na kuendelea.
View attachment 2422779View attachment 2422781View attachment 2422778View attachment 2422788

3). Kuponda kokoto.
Pia kama ww ni mpondaji wa kokoto unaweza kuongeza stone crusher katika kazi zako. Sio lazima liwe kubwa hada dogo la kuzalisha cubic metre 8 kwa siku linatosha sana kujipatia kipato. Tena unaweza kununua used mtaani kwa gharana nafuu (lkn likiwa spana mkononi sana utajuta).
View attachment 2422790View attachment 2422792View attachment 2422791

4). Chain saw ya kukatia miti. Kwa wale wanaoishi maeneo ya upasulishaji mbao wanajua hii kitu umuhimu wake. Bei yake nafikili ni kuanzia milioni 1.7 mpaka 2 na kuendelea. Hii unaweza kununua na ukampa kijana akakuletea mauzo yake au unaweza kukodisha. Ukimpa kijana kwa wiki anakuletea tsh. 70000 au 60000. ila kama ukiishika mwenyewe utapiga hela zaidi. ( ila sasa maisha ya pori yatakuhusu kwasababu hakuna miti mjini).View attachment 2422799

5) Kwa vijana waliopita garaje, air compressor za kujazia upepo kwenye magari na mashine ya ku-apply grease (grease pump) itakua ni option nzuri kwako. Unaweza kuweka nje ya sehemu unayofanyia kazi au ukaweka sehemu nzuri kwa biashara na ukaingiza shilingi miamia daily, sio mbaya sana kijana ukawa na kakitega uchumi pembeni. Hivyo vifaa unaweza ku afford kama mpambanaji haviuzwi ghali sana.
View attachment 2422806View attachment 2422807

6). Kama unaosha magari kwa mkono kwa nini usinunue jet washer (pressure washer). Kwanini usijaribu kununua jet washer uongeze uzalishaji wako na ufanisi wa kazi yako. View attachment 2422813View attachment 2422814

7). Kwa wanaofua nguo(Dobi). Unaweza kuongeza mashine ya kufulia nguo drycleaner itakayo kusaidia kufua nguo nyingi kwa wakati mmoja na kwa uhakika zaidi wateja wako wakafurahia kazi ya mikono yako. View attachment 2422819

Wadau, unajua kuna kazi ni za kawaida tu, lkn ukiziongezea uzalishaji kwa kutumia mashine husika unaweza kuongeza uzalishaji na kipato ukaishi viziri tu. Kuna mda mda mchawi anakua pesa ila kuna mda mchawi ni ww mwenyewe hujajiwekeza kwenye kazi yako mwenyewe. Basi tuanze kufikiria kuwekezea ipasavyo kwenye mishe tunazo fanya.
Asanteni sana, mtanisamehe kwa uandishi mbovu. Na nimeandika kwa experience yangu mwenyewe kupitia ideas za mtaani tu, so am very sorry if i offended you through this.
Pia nilitamani nimpate mwana jf mmoja humu ambae yupo ghetto na hajabanwa sana na michongo yake aje niliko tufundishane ideas mbalimbali. Atakaa kwangu kwa wiki moja au mbili hivi na nauli nitamtumia go and return. (kwa urafiki tu sina nia mbaya). Kwangu utajifunza biashara ya mawe na kokoto pia utajifunza matumizi ya explosives hada baruti na AMFO.

THANKS VERY MUCH (my names LUHANGA ATUKUZWE) from Makambako Njombe.
atukuzweluhanga@gmail.com
Facebook. Atukuzwe Luhanga
Phone. 0765135468.
Safi sana Mkuu izi ndo inshu za kujadili zinaleta motisha kwa sisi vijana tunapambania ndoto, Sio kupoteza mda tunajadili mada za kupiga Nyeto
 
Nyakati za ghetto ni za kupanda na kushuka, rightfully ukomae tuu, hakuna namna.
 
Nimekua nikiufuatilia huu uzi tangu nipo shule mpaka nimeajiliwa kwenye kampuni fulani hapa jijini Dar na ninaishi nyumbani lakini ni muda sasa wa kwenda kupanga ila changamoto kila chumba ninachopelekwa na madalali hakina sifa ninazozihitaji mimi yaani sijui wenzangu mnatumia mbinu gani ya kupata magheto makali
 
Ghetto hua kali kutokana na level ya uchumi wako, ko kupata ghetto ni vile tu kutokana na uchumi wako pia kutokana na mazingira, uswahili kuna maghetto ya bei chee lakini ni ya kawaida tu. Hivyo maghetto makali ni kawaida kua yana maeneo fulani lkn bei hua ni ghali pia.
 
Hii ni kwetu wanangu wa Maghetton!

Tusisahau kusave kila tunapopata mkwanja,hata kama umepata buku ten fanya saving walau ya buku sio mbaya. Jambo lingine na muhimu zaidi,ni kuwekeza katika kitu ambacho una ujuzi au ufahamu nacho kiundani,itapendeza zaidi kitu hicho kiwe kinagusa kwa namna moja au nyingine katika shughuli zako za kila siku.
Hapa namaanisha,mfano mimi msimamizi wa masuala ya mbao,basi mara moja moja nanunua miti kadhaa,au sometimes nanunua mbao kadhaa na kuziuza.
Kwa mfano ukiwa fundi katika workshop ya mtu,unaweza kununua hata MDF-Boards zako,au bawaba,handles,nob,n.k na kuwauzia baadhi ya mafundi wenzio.

Hivyo hivyo hata ukiwa dukani,kama bosi sio mkuda weka hata mzigo wako pale unapoona boss hajaleta mzigo kwasababu either kakwama au lah.
Muhimu ni pesa izunguke.

La mwisho na kubwa zaidi,usisahau kuwapa watu wenye uhitaji,toa msaada kwa watu wanaohitaji,mfano masikini,wazee,watoto yatima,n.k. Wakuu hii issue ya kutoa ni zaidi ya ndumba,milango mingi sana ya kimafanikio hufunguka. Mtu anaposhukuru kuna kitu kikubwa sana unapata. Mtumie hata Mshua, Mother au madogo chochote kile bila kujali uko katika hali gani.

NB: Pahala ambapo unaamka kila siku kwenda kusaka mkate wa kila siku ni pahala muhimu na nyeti sana.
So, Ghetto liheshimiwe,na si kila mtu anapaswa kulazwa ghetto kwako.

Tuendelee kupambana wanangu wa damu,JAH bless us![emoji109]
 
Yeah umenena vyema kabisa, hii ya kuweka vitu na kuwauzia umenipa darasa kubwa sana. Maana nafanya kazi ya drilling na blasting explosive hua tunanua ghalani, sijawahinkuwaza kununua vingi kuvisave kwa ajili ya kuuza nikipata kazi.
 
Shukrani sana ndugu.
Mkuu,katika shughuli zetu hizi za kila siku kuna chances kadhaa ambazo tukizitumia vyema hatukosi hata pesa ya kupaulia[emoji28].
 
Yeah umenena vyema kabisa, hii ya kuweka vitu na kuwauzia umenipa darasa kubwa sana. Maana nafanya kazi ya drilling na blasting explosive hua tunanua ghalani, sijawahinkuwaza kununua vingi kuvisave kwa ajili ya kuuza nikipata kazi.
Mfano wewe waweza kununua vingi na kuwauzia wahitaji,si lazima wao waende kuvitafuta mbali au wewe ukavisake kipindi unafanya hiyo kazi. Waweza kuwa nazo hizo materials muda wowote kisha kuziuza wakati zinahitajika,na baadae inaweza kuwa biashara yako nyingine kubwa tu.
 
Ado ado washkaji nimevunja kibubu hapa nimechoka sina hata mia mazee,nimejilipua lakini fresh hela inatafutwa
IMG_20221124_142659_061.jpg
 
Back
Top Bottom