Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Inaendelea sehemu ya pili.........
KUELEKEA KUISHI GETO MTAANI

Nilirudi home nikiwa na vyombo vyote kama nilivosema ila hamu ya kuhama home ilikuwa iko high sana. Nikicheki kamataji kangu mkononi nina kama kani hivi mfukoni.

Nilikuwa na wazo la biashara kwamba nikipata mtaji nifungue biashara ili kama ikatokea ikawa vzr basi nitafute getho. Biashara ingeweza kulipa bills.

Wazo la business ni kama laki sita mkononi nina laki. Nikamuomba mzee anipe eneo nichome mkaa. Wakuu nilichoma mkaa kwa tabu hivohvo ilikuwa ni mwaka jana nikapata gunia 20. Nikapata laki 2 na tisini hivi.
Nikaiweka ndani.
Hee kijijini si nilikuwa na shamba nililima kiangazi na hapo ni Januari ndio nimetoa mkaa. Bi mkubwa akanambia nitume ya kupalilia na mbolea kama 50 elfu hv jumla.
Hela ikaanza kupungua na Ambition pia. Si nikaanza kutumia nilivokuwa sina akili. Ikabaki kama laki hivi. Nikaamua ninunue kifaa kimoja cha gharama ambacho kiko ndani ya lile wazo la biashara then nitafute mishe nifanye niongezee mtaji maana eneo lingine la mkaa likawa halipo.


So ikaja wazo kwamba kuna kazi za. Anuani za makazi kwamba nikipata basi hela yote nasukumia huko. Kwani hiyo kazi ya anuani za makazi nilipata nafasi. NIKAKOSA KUCHAGULIWA. !!

Hiyo ni mwezi wq tatu mwaka huu
Apo ndio mwisho?
 
Inaendelea sehemu ya pili.........
KUELEKEA KUISHI GETO MTAANI

Nilirudi home nikiwa na vyombo vyote kama nilivosema ila hamu ya kuhama home ilikuwa iko high sana. Nikicheki kamataji kangu mkononi nina kama kani hivi mfukoni.

Nilikuwa na wazo la biashara kwamba nikipata mtaji nifungue biashara ili kama ikatokea ikawa vzr basi nitafute getho. Biashara ingeweza kulipa bills.

Wazo la business ni kama laki sita mkononi nina laki. Nikamuomba mzee anipe eneo nichome mkaa. Wakuu nilichoma mkaa kwa tabu hivohvo ilikuwa ni mwaka jana nikapata gunia 20. Nikapata laki 2 na tisini hivi.
Nikaiweka ndani.
Hee kijijini si nilikuwa na shamba nililima kiangazi na hapo ni Januari ndio nimetoa mkaa. Bi mkubwa akanambia nitume ya kupalilia na mbolea kama 50 elfu hv jumla.
Hela ikaanza kupungua na Ambition pia. Si nikaanza kutumia nilivokuwa sina akili. Ikabaki kama laki hivi. Nikaamua ninunue kifaa kimoja cha gharama ambacho kiko ndani ya lile wazo la biashara then nitafute mishe nifanye niongezee mtaji maana eneo lingine la mkaa likawa halipo.


So ikaja wazo kwamba kuna kazi za. Anuani za makazi kwamba nikipata basi hela yote nasukumia huko. Kwani hiyo kazi ya anuani za makazi nilipata nafasi. NIKAKOSA KUCHAGULIWA. !!

Hiyo ni mwezi wq tatu mwaka huu
Naweka kituo nitarudi
 
Ukitaka usiwe mvivu wa kuosha vyombo baada ya kupika fanya hivi ÷

Kwanza; usiwe na vyombo vingi ghetto, uwe na vichache vya muhimu tu.

Pili; ukiwa unapika kila chombo ambacho hakina matumizi baada ya kumaliza kazi yake hakikisha unakiosha au unakisuuza na kuirudisha mahali pake.

Mpaka unamaliza kupika utajikuta huna chombo hata kimoja kichafu isipokuwa ulivyopikia na utakavyotumia wakati wa kula. Hivi haviwezi kukutia uvivu kuosha maana ni vichache.

Kwanini nasema uwe na vyombo vichache, kwanza siyo hulka mwanaume ghetto kwake kuwe na vyombo vingi vya kupikia hii ni kazi ya wanawake.

Ukiwa na vyombo vingi vitakufanya uwe unatumia tumia tu maana unavyo vingi na unaona uvivu wa kuosho vichafu.

Sasa hii itakukusanyia vyombo vingi vichafu na vitakutia uvivu wa kuosha na hutapika, bajeti yako utaivuruga kwenda kula nje wakati kila kitu unacho ndani.

Wengine husema kwa kuwa yupo dada wa jirani au mwenye nyumba nitamuita aje anioshee, kosa la kiufundi hapa unafanya. Utaoa/kuozeshwa kabla ya muda wako.

Kuoa/kuolewa huwa siyo umri bali ni utayari wa mtu kwamba anaingia kwenye majukumu haya. Usiige kila mtu ana akili zake jinsi ya kuishi kwenye ndoa.

Kuna vijana tulianza wote maisha wakawahi kuoa, mwaka juzi nakutana nao wanasema bora wasingeoa mapema wanasema angalau sasa hivi ndio wangeoa ili wawe wamejijenga zaidi kimaisha.

Wanaume wengi huamua kuoa mapema baada ya kuchoshwa na kuosha vyombo na kupika, Tumia hiyo njia kwanza,chakula cha kujipikia ni bora na ni afya zaidi kuliko cha nje.
Mkuu una madini mengi sana, shukrani kwa ushauri wako.
 
KUISHI GETO. (A) CHUONI.

Wasalam, awali niliahidi kuwaletea stori yangu kuhusu kuhamia getho.
Nikiwa chuo naanza wakati huo nikajipanga ya kuwa nikihitimu tu basi nikajitegemee. Huu uzi niliujua nikiwa second year.

Hivyo nikaanza nunua asset za ndani yaani vyombo ambavyo nitasafirisha hadi home nilikotaka kuanzisha makazi pale nikihitimu. So nilikuwa makini sana kuvitunza ili vifike home vikiwa bull bull.

Home na mkoa nilikokuwa chuo ni km kama 1000 hivi.

Nikawa nikipata boom nanunua vyombo. Kitanda sikununua kwani kule kwetu mbao na vitanda ni bei cheee. Mwaka wa kwanza nilinunua tu godoro kitanda nilikikuta. Mwaka wa tatu nilipohamia palikuwa na kila kitu. Godoro langu nililonunua kwa mama muhindi mitaa ya uhuru pale mwanza super banco kwa Sh laki moja na elfu tano nikaliweka stoo jipya jipya tu.

Nikajifunza heshima ya pesa na jinsi ya kujiheshimu mimi kama mimi.
Maisha ya geto kichuo chuo sio pwa. Bora ukose bundle lakini uhakika wa msosi uwepo.
Nilikuwa nikitoka likizo kwenda chuo basi nabeba nafaka yoyote ile kufanikisha mamisosi.

Afu nilikuwa na hii tabia. Mtaani si hakutabiriki nikaamua kila likizo ile ya kuingia mwaka mwingine nikirudi home basi asilimia 80 ya nguo nilikuwa naacha nguo zangu home. Nikirudi chuo nitanunua nyingine. Lengo lilikuwa nikirud mtaani nisiwe na stress za mavazi kwa mwanzoni. Nibaki kuwaza yale mahitaji mengine muhimu mawili ya binadamu yaani chakula (food), getho(shelter). Clothes yaani (milozi) hapa nikawa nimesolve. Nawafundisha nini akati mwalimu wako wa historia alikufundisha kuhusu mahitaji muhimu ya binadamu. Ahhh mikono inauma kutype ila haina noma.

Yaani bajeti ya msosi na matumizi mengine nilikuwa napiga kabla ya kusign boom na nikisha sign hiyo bajeti inapigwa review kali kufanyiwa uhakiki. Kila nilichonunua sikuwa najutia. Pesa ya boom tamu na me utamu ulizidi kwani nilinunulia kila kitu stahiki. .

Kiukweli nilipata shida miezi miwili ya first year ila baada ya hapo sijawahi kukosa uhakika wa kula.
Basi baada ya kuua UE na kumaliza mazaga ya research kwa mwaka wa mwisho basi nikawa nipangilie naondokaje.

Uzuri me sikuwaga na aibu nikawaambia wanahostel oya anayetaka kuniachia vijiko au kitu chochote kizuri asitupe. Basi nilipewa mivyombo hatari jumlisha na vyangu.
Nikanunua shangazi kaja panga mavyombo vizuri sikuacha kitu hadi upawa na miiko.

Idea ya kutouza chchte nilipewa na bro angu hv kwao ni wa kishua hatari. Unajua wakishua basi alikuwa ndio yule. Ila jamaa kila kitu alirudi nacho kwao. Yeye alipakiza mizigo kwenye gari tupu la mizigo linalorudi kwao. Huyu jamaa alini inspire sana. Mzee wake alimnunulia mazaga ya geto ya milioni moja na nusu lakini hakuuza hata kimoja. Alirudisha kwao. Alilipia usafiri elfu 80 tu toka huko hadi nyanda za juu kusini.

Nb: Kwa mwanachuo yeyote anayesoma hapa namshauri usiuze hiyo gesi hiyo bakuli hiyo meza na hako kakitanda. Mtaani ni kwingine kabisa. Ni aheri uingie mtaani uanze kuwa na mawazo ya ufanye mishe gani au uhamie wapi. Sio unawaza kitanda godoro utapata wapi. Unaanza kuwaza nitaanzaje hata ndoo sina. Maksai mkubwa wewe ukute hata gesi yaki ya oryx ya kilo hamsini ulimgawia kimanzi chako cha first year. Acheni kuigana huko chuo pumbavu zenu. Yaani fika mtaani ili hata ikatokea umepata elfu 30 unahama hapo kwa baba ako. Hama hapo kwenu wazazi wakumiss we mbwa. Wanachuo wengi ni watoto wa maskini ukweli mchungu. Mwenyewe nilikuwa chuo najua kila kitu.

TUENDELEE
Nilifunga mizigo vzr ilikuwa mingi ila kwa kuwa nilijiandaa taratibu haikunipa shida. Nilifikiria nipakize na mimi nijae kwny fuso nikaona so bora nichukue basi.
Mizigo nililipia elfu 18 huwezi amini ilikuwa mizito ila nilipanga vzr aise. Yaani ile nimeifikisha nyumbani kwa wazazi hata siamini.

Nikamuonesha mzee mizigo yangu nikawa namtolea vyombo ajue. [emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mzee nikamfungulia shangazi lile. vipawa na miiko yangu miwili ilikuwa chini kabisa. Basi mzee kuiona alicheka sana akasema hadi upawa. Ila akasema safi ni bora kuliko kuuza.
Kisaikolojia nikaona tu mzee kajua huyu mbwa hana siku nyingi hapa home.

*****

Ninakuja siyo mida wakuu itaendelea.....

.

Sema unatoka mbeya na ulikua unasoma SAUT na ulikua unaishi Kati ya Nyamalango,sweya,masha au nganza

Katika vyuo wanafunzi wana enjoy maisha basi ni wanafunzi wa SAUT mbali na tabu za masomo mengi chuoni ila nje ya chuo maisha ni matam SAUT aisee na yanakuruhusu kujijenga kimaisha
 
Baada ya uzi huu kunihamasisha hatimae na mimi nimehama home na hapa nimeandaa kitu cha chapati mayai
PXL_20221204_192740042.NIGHT_1.jpg
PXL_20221205_162734828.jpg
 
Back
Top Bottom