Ukitaka usiwe mvivu wa kuosha vyombo baada ya kupika fanya hivi ÷
Kwanza; usiwe na vyombo vingi ghetto, uwe na vichache vya muhimu tu.
Pili; ukiwa unapika kila chombo ambacho hakina matumizi baada ya kumaliza kazi yake hakikisha unakiosha au unakisuuza na kuirudisha mahali pake.
Mpaka unamaliza kupika utajikuta huna chombo hata kimoja kichafu isipokuwa ulivyopikia na utakavyotumia wakati wa kula. Hivi haviwezi kukutia uvivu kuosha maana ni vichache.
Kwanini nasema uwe na vyombo vichache, kwanza siyo hulka mwanaume ghetto kwake kuwe na vyombo vingi vya kupikia hii ni kazi ya wanawake.
Ukiwa na vyombo vingi vitakufanya uwe unatumia tumia tu maana unavyo vingi na unaona uvivu wa kuosho vichafu.
Sasa hii itakukusanyia vyombo vingi vichafu na vitakutia uvivu wa kuosha na hutapika, bajeti yako utaivuruga kwenda kula nje wakati kila kitu unacho ndani.
Wengine husema kwa kuwa yupo dada wa jirani au mwenye nyumba nitamuita aje anioshee, kosa la kiufundi hapa unafanya. Utaoa/kuozeshwa kabla ya muda wako.
Kuoa/kuolewa huwa siyo umri bali ni utayari wa mtu kwamba anaingia kwenye majukumu haya. Usiige kila mtu ana akili zake jinsi ya kuishi kwenye ndoa.
Kuna vijana tulianza wote maisha wakawahi kuoa, mwaka juzi nakutana nao wanasema bora wasingeoa mapema wanasema angalau sasa hivi ndio wangeoa ili wawe wamejijenga zaidi kimaisha.
Wanaume wengi huamua kuoa mapema baada ya kuchoshwa na kuosha vyombo na kupika, Tumia hiyo njia kwanza,chakula cha kujipikia ni bora na ni afya zaidi kuliko cha nje.