Mafian cartel
JF-Expert Member
- Nov 19, 2021
- 3,876
- 7,118
Hongera mkuuDah nikaona kama harakati za kutafuta mtaji nifungue biashara ili Nikae geto kama inakwama basi nikasema nisubiri sensa. Ikaja nikaaply vzr dah siku ya interview nikafika. Matokeo holla.
Wakuu nikalala ndani siku nzima stress.
Kuna mwana jirani akanipa pole akanipanga ya kuwa kuna eneo lao la familia ila yeye kapewa kipande anataka apande miti so kuna miti pori so nifanye kuchoma mkaa. Fresh nikapiga gunia saba hivi.
Hiyo ni mwezi wa nane mwishoni. Ikanibidi pia nirudi kijijini kuvuna mahindi yangu. Nikiwa kule bimkubwa anaona kijana jobless ikawa jau. Yaani watoto wote mimi sina issue. Unaweza fanya kazi siku tano then jmos ukaamua kupumzika ila siku hiyo utawakiwa kama mbwa.
Inauma aisee. Kuna bro angu akanitumia siku tangazo la kazi mahali fulani hvi. Nikaaply nikaitwa interview.
Baada aya week mbili niko Bush ninapiga kibarua cha kupiga ngano napigiwa simu na Hr ya kuwa nimepita. Imagine kati ya watu 400 nimepita. Tuliopita ni 70 na kitu.
Basi nikaripoti sign mkataba. Hivi jana ndio nimepanga geto la vyumba viwili na nimetengeneza mwenyewe my dream bed.
Nimefupisha stry kuonesha hamu ya vijana wanaomaliza vyuo na wengine pia wakiwa na hamu ya kujitegemea. Tuschague kazi ilimradi haikuvui utu. Displine mazee inahajika sana mpk tutakapopata makazi yetu ya kudumu.
Long live jf.
Jana ndio nimeingia rasmi kwenye getho langu rasmi.