Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Hata ikiwa hivyo kama huna maneno mengi mbona unaishi tu. Tatizo la nyumba za hivyo kunakuwa na uswahili.

Sipendi sehemu ambazo watu hufungulia subwoofers Kama wanashindana.

Hapa nilipo unaweza hisi hakuna binadamu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sasa ndo penyewee.
 
Sikuwahi kukaa ghetto maana niliacha udom nikaenda college afya na chakula kilikuwa hapo hapo na vyumba vilikuwa apoapo sikukaa MDA marefu nilipata kazi Duuuuh nilitafutana nilikuwa na demu lakin tuliachana ndan ya week Tu baada ya kupata kazi Kwa ajili ya ubize wa kazi, mahali nilipopata kazi mwanamke wa kuowa sioni. Saiv natafuta mfanya kazi wa ndani mdogomdogo wa kike Ila nitamwambia nimeowa mke yupo mkoa mwingine kikazi Ila atakuja MDA wowote
 
Wasiopenda pika wengi wao hawajui pika
Hapo umenena yaan najua kupika ugali tu. Hivyo vingine aiseee ni jau tupu. Home nilikua na dada 3. Nilikua nakula tu na kuchota maji, kupika sikuwahi.
Nina mwaka wa 2 cjawahi kupika chochote ghetto, hata chai tu. Ni mwendo wa kubadilisha migahawa tu.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Sikuwahi kukaa ghetto maana niliacha udom nikaenda college afya na chakula kilikuwa hapo hapo na vyumba vilikuwa apoapo sikukaa MDA marefu nilipata kazi Duuuuh nilitafutana nilikuwa na demu lakin tuliachana ndan ya week Tu baada ya kupata kazi Kwa ajili ya ubize wa kazi, mahali nilipopata kazi mwanamke wa kuowa sioni. Saiv natafuta mfanya kazi wa ndani mdogomdogo wa kike Ila nitamwambia nimeowa mke yupo mkoa mwingine kikazi Ila atakuja MDA wowote
Unaweza kumla kizembe usipolua makini.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Hapo umenena yaan najua kupika ugali tu. Hivyo vingine aiseee ni jau tupu. Home nilikua na dada 3. Nilikua nakula tu na kuchota maji, kupika sikuwahi.
Nina mwaka wa 2 cjawahi kupika chochote ghetto, hata chai tu. Ni mwendo wa kubadilisha migahawa tu.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
Jifunze pika, vyakula vya mahotel, migahawa mingi viko kibiashara kuliko kiafya
 
Afu kuna hii nimesahau kusimulia hapo juu.

Ilikuwa hivi mwezi Juni kuna mwana alikua na getho zuri Town centre bei kitonga akawa anahama anahamia kwake basi akasema anipasie.
Nikafuata ushauri humu ya kwamba unaweza panga afu huku uko unakaa home unajivuta na kununua au kuweka vitu mdogomdogo. Basi nikajikusanya nikapata kodi ya miezi mitatu. Nikalipa. Hapo nasubiri mishe fulani itiki then nisepe home nihamie kwa hilo getho nililolilipia..
Hee si mishe ikabuma nikazidi kujipa moyo. Mwezi wa kwanza, wa pili hadi wa tatu unakata sijawah hata peleka chochote wala nilale.
Mwezi wa tatu yaani ule mwez kodi ndio inaisha mwenye nyumba yuko Dar akanipigia akanambia Sparta mbn kumbe hujahamia miezi yote hiyo. Nikamdanganya nikamuambia ya kuwa mzee niko porini tunapasua mbao so niko camp sijapata muda wa kuja Town.
Akanambia ya kuwa kuna watu wanamsumbua wanakitaka chumba dah kama veep nikurdishie kodi ya mwezi mmoja. Nikasema sawa kishingo upande.
😂😂😭😭
Nikacheka wee na kulia kwa pamoja.
Ukiona mtu kahamia full getho mpe heshima yake kwa kweli.

Elfu sitini yangu ikaenda bure na sijawahi kumuambia mtu dadeki.



Lakini hii leo nimeweza hamia rasmi na uwezo wa kulipa bills na korokocho nyingine ninao.
Sasa inatakiwa nitafute muda niitengeneze kabati langu la nguo na style hii hapa.
 
7f389bbc757f57ad879547d5fbde9afa.jpg
 
Hama.

Kuna mtaa huwa napita kuna vyumba kama 30 kila mtu anapiga wimbo wake
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], hapa kwetu hakuna huo mtindo, tupo wastaarabu na tulio elimika.
 
KUISHI GETO. (A) CHUONI.

Wasalam, awali niliahidi kuwaletea stori yangu kuhusu kuhamia getho.
Nikiwa chuo naanza wakati huo nikajipanga ya kuwa nikihitimu tu basi nikajitegemee. Huu uzi niliujua nikiwa second year.

Hivyo nikaanza nunua asset za ndani yaani vyombo ambavyo nitasafirisha hadi home nilikotaka kuanzisha makazi pale nikihitimu. So nilikuwa makini sana kuvitunza ili vifike home vikiwa bull bull.

Home na mkoa nilikokuwa chuo ni km kama 1000 hivi.

Nikawa nikipata boom nanunua vyombo. Kitanda sikununua kwani kule kwetu mbao na vitanda ni bei cheee. Mwaka wa kwanza nilinunua tu godoro kitanda nilikikuta. Mwaka wa tatu nilipohamia palikuwa na kila kitu. Godoro langu nililonunua kwa mama muhindi mitaa ya uhuru pale mwanza super banco kwa Sh laki moja na elfu tano nikaliweka stoo jipya jipya tu.

Nikajifunza heshima ya pesa na jinsi ya kujiheshimu mimi kama mimi.
Maisha ya geto kichuo chuo sio pwa. Bora ukose bundle lakini uhakika wa msosi uwepo.
Nilikuwa nikitoka likizo kwenda chuo basi nabeba nafaka yoyote ile kufanikisha mamisosi.

Afu nilikuwa na hii tabia. Mtaani si hakutabiriki nikaamua kila likizo ile ya kuingia mwaka mwingine nikirudi home basi asilimia 80 ya nguo nilikuwa naacha nguo zangu home. Nikirudi chuo nitanunua nyingine. Lengo lilikuwa nikirud mtaani nisiwe na stress za mavazi kwa mwanzoni. Nibaki kuwaza yale mahitaji mengine muhimu mawili ya binadamu yaani chakula (food), getho(shelter). Clothes yaani (milozi) hapa nikawa nimesolve. Nawafundisha nini akati mwalimu wako wa historia alikufundisha kuhusu mahitaji muhimu ya binadamu. Ahhh mikono inauma kutype ila haina noma.

Yaani bajeti ya msosi na matumizi mengine nilikuwa napiga kabla ya kusign boom na nikisha sign hiyo bajeti inapigwa review kali kufanyiwa uhakiki. Kila nilichonunua sikuwa najutia. Pesa ya boom tamu na me utamu ulizidi kwani nilinunulia kila kitu stahiki. .

Kiukweli nilipata shida miezi miwili ya first year ila baada ya hapo sijawahi kukosa uhakika wa kula.
Basi baada ya kuua UE na kumaliza mazaga ya research kwa mwaka wa mwisho basi nikawa nipangilie naondokaje.

Uzuri me sikuwaga na aibu nikawaambia wanahostel oya anayetaka kuniachia vijiko au kitu chochote kizuri asitupe. Basi nilipewa mivyombo hatari jumlisha na vyangu.
Nikanunua shangazi kaja panga mavyombo vizuri sikuacha kitu hadi upawa na miiko.

Idea ya kutouza chchte nilipewa na bro angu hv kwao ni wa kishua hatari. Unajua wakishua basi alikuwa ndio yule. Ila jamaa kila kitu alirudi nacho kwao. Yeye alipakiza mizigo kwenye gari tupu la mizigo linalorudi kwao. Huyu jamaa alini inspire sana. Mzee wake alimnunulia mazaga ya geto ya milioni moja na nusu lakini hakuuza hata kimoja. Alirudisha kwao. Alilipia usafiri elfu 80 tu toka huko hadi nyanda za juu kusini.

Nb: Kwa mwanachuo yeyote anayesoma hapa namshauri usiuze hiyo gesi hiyo bakuli hiyo meza na hako kakitanda. Mtaani ni kwingine kabisa. Ni aheri uingie mtaani uanze kuwa na mawazo ya ufanye mishe gani au uhamie wapi. Sio unawaza kitanda godoro utapata wapi. Unaanza kuwaza nitaanzaje hata ndoo sina. Maksai mkubwa wewe ukute hata gesi yaki ya oryx ya kilo hamsini ulimgawia kimanzi chako cha first year. Acheni kuigana huko chuo pumbavu zenu. Yaani fika mtaani ili hata ikatokea umepata elfu 30 unahama hapo kwa baba ako. Hama hapo kwenu wazazi wakumiss we mbwa. Wanachuo wengi ni watoto wa maskini ukweli mchungu. Mwenyewe nilikuwa chuo najua kila kitu.

TUENDELEE
Nilifunga mizigo vzr ilikuwa mingi ila kwa kuwa nilijiandaa taratibu haikunipa shida. Nilifikiria nipakize na mimi nijae kwny fuso nikaona so bora nichukue basi.
Mizigo nililipia elfu 18 huwezi amini ilikuwa mizito ila nilipanga vzr aise. Yaani ile nimeifikisha nyumbani kwa wazazi hata siamini.

Nikamuonesha mzee mizigo yangu nikawa namtolea vyombo ajue. [emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mzee nikamfungulia shangazi lile. vipawa na miiko yangu miwili ilikuwa chini kabisa. Basi mzee kuiona alicheka sana akasema hadi upawa. Ila akasema safi ni bora kuliko kuuza.
Kisaikolojia nikaona tu mzee kajua huyu mbwa hana siku nyingi hapa home.

*****

Ninakuja siyo mida wakuu itaendelea.....

.
[emoji23] mkuu naona umeamua kuwakanya vijana katkat ya uzi
 
Back
Top Bottom