Ulianzaje kukaa gheto?

Nimeishia katikati next time jitaidi kuandika vziri
 
Kero za nyumbani ni nyingi Sana, ukizingatia Umri wa miaka 25 Ni mtu mzima na ungependa kuwa na maamuzi yako. Lakini ukikaa nyumbani unakuwa mtumwa, Utaambiwa fanya hiki, fanya kile, Nenda kule au Kalete hiki, Simamia kazi fulani nk

Wakati mwingine lawama wakirudi nyumbani, mbona hiki hakipo Kama inavyotakiwa.

Changamoto nyingine nyumbni wanakuchukulia wewe Kama Mtoto asiye jitambua, Hana ratiba, ni Kama robot anasubiri instruction,
Ndio maana ukiamka wanakupa timetable yao na majukumu ambayo unapaswa kuyatekeleza.

Wakati mwingine unaamka na ratiba zako, lakini zinakuwa zinaingiliwa na ratiba za hapo nyumbani walizokupangia, Sio zako.

Nyumbani panakera Sio kidogo.
Uhuru hakuna. Sio uhuru wa kuita Mademu peke ake hata wakufanya maamuzi yako.

Nje ya nyumbani uko huru Sana.
Changamoto zipo pia!!! Kama huna mishe zinazoeleweka! Jipange vizuri tu, Uingie mtaani unavijihera Mengine yatajiset polepole.
 
Dogo usirudie kuandika hivi ukiwa jf..uandishi huo peleka facebook au magroup yenu ya whatsapp.
 
Malizia story hii mzee baba
 
[emoji119][emoji119][emoji122][emoji122]
 
Sawa mkuu kheri ya wewe uliyenishauri. Kuliko kuchekwa tu alafu ujui wapi umekosea. Alafu sijajua shida inakuja wapi . au nilicho kiandika hakisomeki ?
Vizuri! Umeshajirekebisha kwenye yale ma "X X X X" yako... bado una tatizo la "H" "I" na "A".

Unasoma shule gani?
 
Nilipanga gheto nkalipa kodi ya miezi miwili nlikuwa sina godoro mwenye nyumba akinisaidia godoro, nikaanzia kulala chini. Ila saiv gheto limejaa
Nipo kwenye process za kumalizia nyumba yangu
dah mkuu m mwenyewe nlipanga gheto nikachukua chumba na sebule, halafu siku ya kuhamia nikahamia na godoro, sofa la watu wawili ,pasi ya umeme na subwoofer.

Kila nikipita sebulen ikawa inanipa hasira ya kutafuta, sasa hv nmefanikiwa kuwa na kila kitu.
 
Ukitaka kuishi geto kwa ambae uko nyumban na hauna kazi ila una vicent kidogo na umedhamiria kuishi geto..ONDOKA home nenda katafute geto mkoa mwingine kabisa na huo uliopo..panga room ya bei ndogo utakayokutana nayo mbele yako..

Nakumbuka nilianza ishi kwenye room ya 15,000 kwa mwezi,kilichoniokoa kale ka chumba kalikua n kastoo ka mwenye nyumba so kalikua kadunchu sana ila kako ndani ya Bonge moja la MJENGO ukiniona naingia getini unaeza hisi naishi mle ndani kumbe naenda stoo kwangu...ni unaeka godoro la 3*6 na ndoo mbili tu hamna nafasi hata ya kupita ukiingia ndani ni unapanda juu ya godoro tu.

Nilisugua benchi pale,kodi ikawa inanishinda ila nikawa najitahidi nalipa hata ya mwezi mwezi sijawahi rudi home tangu nitoke..saivi naishi Kwangu asee nyumbani kbsa sipaiti geto tena japo nipo peke angu.
 
safi sana...japo siwashauri watu wanaoanza maisha kuanza kwa style hiiii...nawambiaga waanze na Chumba cha chini kbsa haijalishi una sh ngapi mkononi kwakua unaanza maisha tena ni maisha yako peke ako Nawambiaga waanze na chumba hata kama kipo cha 5000 kwa mwezi aende...

ukishazoea maisha ya geto ukajua changamoto,ukawa na uhakika wa kipato chako..ndio kinachofata ni Kuishi kwenye ndoto zako,unafanya kama ulivyofanya wewe sasa.
 
siku hizi kama una geto unatuonyesha Funguo halafu tunaangalia ni aina gani ya Funguo..
 
Mimi nina 23 years now, nimeanza kuishi geto nikiwa na miaka 19, baada ya kupote ada ya chuo million 2 na nusu ila saiv maisha yanaenda vzr tu namshukuru Mungu kwa kupoteza hela nilikimbia kipigo cha mzeee baba
watu waloanza kuishi geto mapema/maisha ya kujitegemea mapema huwa nawaona kama WAHENGA hua wanajua vitu vingi sana...tena ukute yule alokaa maisha ya changanyikeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…