dah kama masihara vile, nilikua na kama 200K hivi, nikachomoka hadi maskani fulani hivi kuna madalali kibao yani...."oya nataka ghetto kali liwe la nje, wapangaji wawe wachache na kuwe na toi la ndani ili nikiingia na pisi kali mambo yasiwe mengi." nikaongea kwa sauti ya mamlaka.
kuna mwana mmoja akanitonya kwa dalali mmoja hivi kibonge maneno meengi, "ghetto lipo kaka ila chumba kidogo sanaaa, kuna toi la ndani, chumba ni cha nje ila wapangaji wapo wengi, hata kama sasa hivi unalitaka twende ukalicheki" dalali akanisanukia.
tukadandia boda hadi kwenye ghetto, nikalipia 3months na nikam-clear dalali, bado sijahamia coz kuna shemeji yenu namsubiri tukalizindue ghetto.