Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Wakuu mambo vipi, Leo naomba tufanye kushare kila mtu jinsi alivyo chomoka Nyumbani kwao..Hii itatoa hamasa kwa wale waliokua nyumbani na kuogopa kuhama na kuanza kujitegemea.

Janga hili linawakumba wana vyuo wengi,unakuta mtu anamalza chuo akiwa labda ana 25 then anarud nyumbani ,mbaya zaid anasubir kazi..alaf kazi zenyew haijulkani utapata lini.

Hii inapelekea wana wengi kua na fear ya kuchomoka home...Kiukwel hali ya kukaa hom inakata sana..Mzee unakuta anachomoka anakuachia mikazi flani hivi howcome.

Ukija upande wa MMU ndio mambo yanakua sio mambo...mtoto anataka aje kukusalmia unaona soo kwasababu upo nyumbani..inakata sana hii

Tukija kwenye maisha ya kujituma tu..sometime unakosa hamasa ya kupambana kwasababu ugali wa bure,unalala bure,kila kitu bure..hii inakua ngumu kuwaza kwa mapana ili kuanza kukamilisha dream zako..

Pia inakata sana..pale wanao unakuta wapo na mageto yao..lakin wewe kwako ni tofauti.

Sasa naomba kila mmoja aseme alichomokaje home na kuanza kukomaa na maisha..Achilia changamoto zake kikubwa hapa ni kusepa kwa maza..

Mimi binafsi geto nilianza kukaa soon nilivyoingia chuo,,,nakumbuka nilipata room ya elf 50 nikaanza nayo kibish,nikanunua bed ya 150, 5 kwa 6,nikatafuta feni tu ya elf 35..si unajua joto la dar..nikaingia k.koo nikavuta subwoofer ya elf 75 tu...geto bila mziki sio geto ni choo,kujichek mfukoni boom likawa lishakata...basi nikaendelea kuishi geto hadi namalza chuo geto likawa limesheheni tu.

sasa baada ya kumalza chuo. Ndio nikarudi hom..ujinga niliofanya ni kurud hom na baadhi ya vitu niliviuza...Kasheshe ndio ipo saiz..wakuu hom akili inalala,,vibe yote hakuna ,hapa ndio najichanga nichomoke tena nirud geto nianze kupambana..hop ndan ya huu mwaka nitakua nishasepa hom kwa mara nyingine.

Sasa share kitu basi nawewe..

Nini lilikusukuma usepe home?
Kitu gani kilikupa mzuka wa kuanza kukaa geto?
Vipi ulianza kukaa geto ukiwa na kazi au kibishi tu?
Maisha yalkuaje since day one?
Je ulienjoy uamuzi wako wa kusepa home?
ulianza kununa vitu gani vya msingi na kuanza kuishi geto
Una lipi la kuwaambia wana walioko home hadi leo wakiogopa kukaa geto kisa hawana ajira bado?

Karibuni wakuu..

View attachment 878774
daa umefanya uzembe kama wangu,nikiwa shule nilikua nakaa na manzi tukanunua kila kitu kwa malengo baada ya shule tuanze maisha.

akiba tukiwa na m.1 na laki 6, uoga kitu cha ajabu sana nikaona ntafanya nini nikala kona kurudi home nikamuachia manzi kila kitu. alinililia sana nirudi ila ule uoga haukuwa wa nchi hii

now nimepanga ila najilaumu sana kumkimbia yule manzi kwa uoga wa maisha mji wa watu
Hahahaha ulifanya makosa Sana mkuu [emoji848] kukimbia na pesa mliyomake ulimuachia yote aseee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilipoanza kuishi mwenyewe mkoa tofauti na nyumbani walinipa kitanda godoro na vitu vingine nikakataa, nilienda na begi langu tu kufika nikanunua godoro langu nikaanza kupiga nyama chini, nimenunua vitu vyangu Sasa ni mwendo mdundo tu, sikuwahi tegemea kuwa ipo siku nitaweza ishi mwenyewe nilishazoea nyumbani kila kitu free, at least nami nimepata Cha kusimulia wanangu loh, nimejifunza ku budget leaving on my own mwanzo ilikuwa ngumu, nilijitahidi hata kutokuwaambia nyumbani, nashukuru Mungu naishi mwenyewe kwa kujitegemea, nimenunua vitu vyangu nadunda zangu

Hongera [emoji3]

Kwaiyo ukawa unaulza chini for how long

Sent from my SM-G9550 using Tapatalk
 
Hongera [emoji3]

Kwaiyo ukawa unaulza chini for how long

Sent from my SM-G9550 using Tapatalk
Kwa miezi kadhaa aisee I wanted to learn life hafu watu walikuwa wanashangaa kwanini nyumba yako hii chukua chumba uwe na vitu kiruu kumbe ni mipango tu nowdays geto langu limedamshi hatari loh.
Kumbe naweza ishi vyovyote na nisife

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa miezi kadhaa aisee I wanted to learn life hafu watu walikuwa wanashangaa kwanini nyumba yako hii chukua chumba uwe na vitu kiruu kumbe ni mipango tu nowdays geto langu limedamshi hatari loh.
Kumbe naweza ishi vyovyote na nisife

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee umetisha sana mama[emoji119]

Sent from my SM-G9550 using Tapatalk
 
Muhun sio lazma awe na tabia za ajabu...hata mtu smart kwangu mi namuita muhun tu....skuiz wahun ndio watu makin mkuu...relax

Sent from my SM-G9550 using Tapatalk
Kijana naona geto linakuharibu.
 
Back
Top Bottom