NILIONDOKA KWA MLEZI NA KUANZA KULALA GUEST TAKRIBANI MIEZI MIWILI.....
Nakumbuka ni baada tu ya kumaliza form four,nlikua naishi na mlezi tu hivyo kwa kiasi fulani nilikua kila nikitafakari juu ya hatma ya maisha yangu nikawa najiona sina changu pale katika ile nyumba.
Basi, ilikua ni takribani wiki mbili tu tangu nilipo maliza mtihani wangu wa kidato cha nne ndipo morale wa kuhama pale kwa mlezi wangu ulipo kuwa ukizidi.
Hivyo sikua na muda wa kupoteza,nikaingia street kupiga manual works.
Haikuchukua hata week moja nikajitupia kwa wanangu wa Tigo(MCL communication). Kipindi hicho ile promo ya "toa buku urudishiwe buku" na "Facebook bure". Nikapewa CODE ya kusajilia nikiwa kama "FREE LENCER",siku hiyo naanza kazi kumbe ndio siku "Tigo promo" inaanza(hii inahusisha safari katika maeneo mbalimbali).
Basi ndugu,nikaunga nao safari,na huo ndo ukawa mwisho wa kuishi home. Tulipiga kazi almost two months,mwanzo ulikua mgumu kwani sikua na uzoefu,ila baada ya kuzoea tu ile kazi nikawa napiga pesa sana.
Siku zote hizo makazi yetu yalikua ni guest,yani mkichukua double room basi mnalala wanne then mnachanga pesa.
Tulipo rudi sikutaka tena kurudi home kabisa,hapo ndipo maisha ya gheto yalipo anzia.