Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Big up man mi changamoto kibao nimepitia na mpk leo cjapata ahueni otherwise uzima upo may be kesho things might be ok
So kupitia mimi hope mtajifunza vijana wenzangu kuwa endapo utalitumia vizuri basi hakika maisha yak yatabadilika.pia la mwisho ni kumtafuta mwenza mwenye maono ila uiangukia kwa kwa hawa makahaba wa mjini utaishia kuhangaika mwisho wa siku unarudi nyumbani ukiwa na miaka 40,bila kufanya lolote
Jerrybanks
 
dah siiti getto saivi napaheshimu sana!!
ilikua baada ya kumaliza chuo.. niliumiza kichwa sana ntafanyaje nikae home.. hapana nitadharaulika sana.. kuna mshkaji mmoja nilisoma nae premary alikua mwanza anapiga mishe zake za boda boda.. nikaongea nae jamaa fresh.. nikatoka home bila kuwaanbia naenda mwanza.. ilibd niwadanganye maana wasingeruhusu niondoke bila hela... nilikaa kwa mshakaji mpk kesho ananiheshim sana.. nilikua nalala kwenye sofa.. usiku jamaa anakuja kalewa kinoma.. anankuta macho inabidi nitoke amgonge dem wake.. 😂😂😂 (nimepigwa exile sana).. ikawa kidogo tabu kupata kazi ya taaluma yangu.. nikaamua kushika chaki.. nikafundisha fizikia na hesabu.. nikawa nalipwa vizur.. mshahara wa kwanza tuu.. nikahama na kununua kitanda. mshahara wa pili nikaanza kununua vitu vingne.. nilikua na jeuri sana.. maana nilikua sinunui kitu cha kawaida.. yaan najibana miezi mitatu.. then naenda nunua bonge la kabatii.. nikilileta geto nasema sinunui tena kabati maisha yangu yote.. lbd anunue mwanamke.. saiv nikimkaribisha dem geto lazm aulize umeoa!?? 😂😂😂😂😂 nimejifunza mengi sana.. hapa ni nyumbani si geto tena!!
Asante sana...NIMEPATA SOMO ZURI
 
🤣 Nashukuru sana huu uzi, ulinihamasisha nikajipinda, nimechukua kitanda, godoro na kabati vya kuvutia nimehama home, sasa endeleeni kutuma madini zaidi nizidi kuhamasika .... shida ninayopata huku ni vyakula vya kununua havina ubora pia upweke
Anza kupika tu mkuu, nunua vyombo japo ni ghali lakini inasaidia hasa ukimiss chakula kizuri ukipendacho
 
Kabla ya kuanza kukaa geto nakumbuka 2012 naingia DAR sina ndugu nimjuae,rafiki,wala jirani nimekuja nataka kuwa na maisha yangu...mkononi nina begi la nguo tu sina Cheti hata cha drs la 7...nimetua Ubungo tu nikawaza leo naenda kulala wapi?

Mfukoni nakumbuka nilikua na 14000 alafu nilikua na simu yangu ya bLACKberry bold,begi zito ntaenda nalo wapi nkawa najiuliza? nikawa nimetoka nnje ya stand ya ubungo nakuja mdg mdg na hii road ya shekilango huku naburuza begi langu usiku huo.

Nikaja mdogo mdogo hadi nikafika manzese Tip Top kufika pale nikapata wazo la kwenda kulala kwanza guest alafu kesho yake pakikucha ntajua cha kufanya..nikavuka road nikaenda ndani ndani huko kutafuta guest ya bei rahisi nikabahatika pata guest sh 7000 nikaingia nikaoga nikabadilisha nguo nikawa nawaza sasa..mkononi nina 7000 tu imebaki.

Akili ikanijia..usiku huo huo nikaamka nikatoka nnje ilikua mida ya saa 7 inaenda 8 usiku nikamkuta mlinzi mbabu anakunywa kahawa basi nikamuita,nikamuuliza "samahani babu,nimetoka safari nina nguo chafu nahitaji mtu wa kuzifua napata wapi maana kesho asubuhi natakiwa kuondoka"..yule babau akaniuliza kwahiyo unataka zifuliwe usiku huu uondoke nazo kesho? nikamwambia hapana nitaziacha nitarudi jioni.

Akanambia hata yeye anaweza kuzifua zitoe tuzihesabu na kuziona...basi nikamtolea tukahesabu nikamwachia,hapo nguo wala hazikua chafu nilitaka tu kupata mtu wakubaki na begi langu la nguo..baada yakukubaliana nikampa kisha nikarudi kulala sasa vizuri..palipokucha kazi yya kutafuta kazi ikaaanza.

Nakumbuka nilienda MOSHI HOTEL ipo pale tip top jikoni nikamkuta mzee mmoja nikamwomba kazi,akaniangalia kisha akanambia hapa kazi za wanaume hamna kuna kazi za wanawake tu kama kuosha vyombo na kufanya usafi,unaweza fanya? nikamwambia Baba mimi nafanya kazi yyte naomba kazi..akanambia pita ndani nakumbuka nilikua nimevaa tracksuit nyekundu ya manchester juu mpk chini na raba zangu..nikaingia ndani nikaonyeshwa karo la vyombo lina vyombo masahani na masufuria..

Nikaanza kuosha sahani zinazotoka kwa wateja kazi ikaendelea hadi muda wa kufunga,nikasugua masufuria makubwa mpk yakatakata,nikapiga deki jiko ki ufupi jiko lili meremeta hiyo siku..maana sio kwa kupanga Kule..baada ya kila kitu yule baba alonipa kazi alikua kashaondoka wafanyakazi tunalipwa na keshia mshika daftari na hela so akanambia nimeambiwa nikupe 4000..Nikapokea nikamshukuru akanambia Poa kesho uwahi mapema basi,nikamjibu sawa.

So nikaondoka usiku huo ilikua mida ya saa 7 hv sina pakulala..nikawa nawaza leo naenda wapi kulala! bahati nzuri nikiwa nazunguka mitaa ile ile kuna pub moja iNaitwa LAMBO HUWA kuna wadada wanajiuzaga hapo so wanakesha 24hrs nikaingia mle ndani nikawa nashangaa pool table,na kuangalia vituko vya mle ndani...

Usingizi ukawa unanishika nikawa natamani sana kulala,nikiwa pale nimesimama nasinzia alikuja BAUNSA akanambia oyaaa hatulali humu nenda kalale kwenuuu,kama ushamaliza kinywaji sepa zako...hapo hapo nikaskia DJ akitangaza "BAUNSA TUSAIDIENI KUTOA NNJE WATU WASIO NA VINYWAJI" BASI baunsa akanambia toka nnje..nikamwambia Mi nasubiri game liishe nicheze pool table,akanambia Chukua kinywaji basi....nikamwambia nletee PEPSI basi akanletea pepsi..wanauza 1000.

Nikawa na pepsi yangu,sasa kwakua nina kinywaji nikatafuta kiti na meza nikakaaa na PEPSI yangu,nikawa siiinywi maana ikiisha unafukuzwa nnje au ununue ingine,basi nkaiweka mezani mimi nkawa nasinzia...ivyo ivyo kufika mida yya saa 10 hivi nikanywa pepsi yangu nikatoka nnje nikarudi kule kazini.

Nikafika nikaingia jikoni nikaanza kukoleza moto na kuweka kila kitu mkao yani...saa 11 wakati boss wa jikoni analeta nyama za supu na kongoro,utumbo anakuta nishakoleza Moto nishachemsha maji nipo naota Moto,akaniuliza DOGO VIPI unaipenda kazi yako eeeeh? SAFI SANA.

Basi tukaosha utumbo tukabandika kwa mara yya kwanza saa 12 na nusu supu ilikua ishaiva SIFA ZOTE kwangu yani..basi maisha yangu yakaendelea hivyo usiku nikitoka kazini naenda LAMBO nanunua soda ya buku nakaa mezani nalala hapo hapo ikifika saa 10 nainywa soda natoka naenda kazini...

Nikifika kazini pale naingia kwenye vyoo vya wateja naoga nafua nguo yangu naikamua naikung'uta naivaaa hyo hyo alafu naenda nakoleza moto chap chap nakaa NAOTA basi nilifanya kazi pale sana hadi siku moja yule boss akanishtukia kuwa sina mahali pakulala akaniuliza unakaa wapi? nikamwambia sina pakukaa nikamuelezea kwa ufupi.

AKanambia nitaongea na meneja wa hii hotel utakua unalala na wafanya usafi wa hapa so utakua unakaa hapa hapa,basi alifanya hivyo nikawa nakaa pale pale hotelini nikawa siendi tena LAMBO,maisha yaliendelea hadi nilipopata vicent vya Kupanga GETO ambapo nakumbuka kwa mara ya kwanza kupanga nilipanga chumba cha 15,000 Maisha yaliendelea vizuri nikapata experiance ya vitu vingi.

kwa sasa naishi kwangu naishi maisha ya Ndoto zangu japo bado nazidi kupambana...

Naosha sufuria kupita maelezo yani mdada ukija kwangu ukagusa sufuria zangu kijinga jinga ukaziacha,nazirudia upya

Napika vyakula hadi wadada nikiwapkiaga wananambia we kaka Umejulia wapi kupika vyakula hivi? jibu ni SIRI YANGU.

Nilikujaga kurudia lile BEGI LANGU la nguo nililoachaga kwa BABU japo alinambiaga nimpe 30,000 na kwakua nilikua nayo wala sikuona shida nilimpaga na nikachukua nguo zangu..maisha yakaendelea.
ulipitia changamoto kubwa lakini matunda yake naimani umeyaona, umeniinspire na mie kuwa na moyo mgumu
 
2015 nillikuwa najaa na jamaa yangu uku napiga msuri qt.

Badae tuka shodwana na jamaa so nikitafuta chumba nikaamia nikiwa nausufuria mbili tuu Sina hata godoro nillikuwa na jiko langu dogo la mchina maisha yalienda kama Kawa nikapambana ad Leo mambo Safi japo bado nipo geto Lakin
 
2015 nillikuwa najaa na jamaa yangu uku napiga msuri qt
Badae tuka shodwana na jamaa so nikitafuta chumba nikaamia nikiwa nausufuria mbili tuu Sina hata godoro nillikuwa na jiko langu dogo la mchina maisha yalienda kama Kawa nikapambana ad Leo mambo Safi japo bado nipo geto Lakin
Jamaa yako yukwap mkuu?

Umetisha lakin sio kwa mwanzo huo mkuu[emoji16]
 
Daaahh uu uzi ulinihamasisha niingie magetoni, saiv naishi gheto nna kama miez 5 hivi ila pako pOa voz tuko wapangaji wote ni mabachela tu. ila ndo vile vitu vingi sina c unajua mwanzo mgumu
Screenshot_20190802-145522.jpeg
 
Back
Top Bottom