Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Nmeanza kukaa geto nna takribani mwaka na robo, sikuondoka na mia ya mzazi, nna fridge, kitanda, dstv, TV na kila chombo, kodi nalipa 150K, nshanunua na Gari, nmenunua kiwanja, na nategemea mwezi wa 5 nianze ujenzi ila mniombee maana mpaka sahivi nna balance ya 4M na kiwanja nmenunua 10M+ ilna sina mkopo sehem yoyote, na bado niko under 23, tuombeane wakuu
Hongera sana mkuu.
 
Maisha ya geto rahaaa sanaaaa
20210223_234209.jpg
 
Mimi ilikuwa tofauti kidogo..
Mimi nilipanga miaka kadhaa iliyopita nyuma, kitu Cha kwanza wakati naanza maisha nilinunua kapeti, mapazia na Tenga pa nguo chafu, baadae nikanunua subwoofer sea piano old model zile za mziki mnene wakati huo nalala chini kwenye kapeti nikiwa natandika blanketi chini. Baad ya mwezi nikavuta feni na kitanda niliona nilinunua godoro kwanza nitakuwa mvivu wa kununua kitanda kwa hiyo Bora ninunue kitanda ambacho kikikaa ndani kitanipa uchungu wa kununua godoro..
Baada ya mwaka nikajichanga changa nikavuta flat screen 32 inch, mwezi uliofuata nikanunua sofa , mwezi wa 3 nikanunua godoro 10 inch Sasa rasmi..nikajaa vyombo, Gesi nyingi mkubwa na plate ya majiko mawili..
Vyote hivyo ilinichukua miaka 2 na nusu na Sasa hivi Nimepanga vyumba viwili, na vyote nilinunua dukani vikiwa vipya kasoro bufa maana lile la mwanzo used, nilinilia pesa kinoma kila week linaharibika mwishowe kwa HASIRA nikaamua kuligawa tu.. Sasa ikija gheto kwangu Ni hatari hutamani kuchomoka yaani kiyoyozi tu ndo kinakosekana hapa[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom