Mzee kwanza pole kwa hizo stress,,,kitu unachotakiwa kwanza tuliza kichwa chako..kisha amin unaweza fanya jambo bado..
Swala la kazi hapo hasa za kuajiriwa weka pending kwanza.... watu weng wamelemaa wakiamini kazi itakuja tu...
We ni mwanaume aka mwamba,baharia etc...sasa sie wamba tuko hivi..Macho yote huwa tunaweka mtaani na kuangalia tunaweza piga mbishe gani...Ww ukiona kuna hela sehem flan basi jichanganye naww ukapige hela..kikubwa kazi iwe halali...
Pili usiache kujifunza kitu kipya chochote kinachoweza kukupa hela..mzee jifunze mambo ni mengi sana yana hela..tumia google na youtube vizur utajifunza mambo meng utapata hela...
Mfano ngoja nikupe list ya vitu kadhaa nilivyojifunza kupitia mitandao na ndo vinavyonipa hela mimi...
1.Kuflash simu,hapa naongelea maswala ya kutoa frp, flashing, repair network,ku unlock network lock hizi na kesi kibao tu...mzee unakuta nimekaa tu naletewa simu
2.maswala ya computer maintenance,sjui kupiga window,mara drivers ku update,mara kuweka program ,mara kuweka ram,mara kufunga hdd na kesi nying tu nafanya...
3.Manunuzi ya mtandaon, AliExpres na eBay huko...nilijfunza kununua vitu huko kwa bei rahis naaagiza nakuja bongo napush faida kubwa sana...lakin pia naagizia watu bidhaa huko,navizia msimu wa offa nanunua order kwa bei chee napata cha juu na bado nalipwa hela ya kuagiza bidhaa...mfano leo nimepta offa simu mteja alilipia 380 majuzi,mim nikasubr anniversary sales ya leo AliExpres nikapata hiyo simu kwa laki 3 kamili...80 ikawa faida..sijaila hiyo faida..namm nikaweka order ya vitu vidogo vidogo mpaka 80 yote ikaisha..hivyo vitu vikija naviuza kiulaini napata backup ya mkwanja
Yani nna issue kibao nmejifunza..hizo ni samples tu..zingine ni kubwa mpka kuandika uchawi..[emoji1787]
So mwana tuliza akili anza kupamban jifunze mambo mapya,jichanganye kwenye pesa we ingia..saidia hata fundi poa tu..