Kwanza nitoe shukrani sana kwa mkuu
Walec kwa kufikiria kuanzisha uzi huu ambao umekuwa ni motivational kwa vijana wengi tena saanaa hakika hii ni akili kubwa hongera na pia nikushkuru maana hata mimi ni mmojawapo wa wale walionufaika na uzi huu matata sana .Hakika uzi huu utaishi milele 'na milele mkuu,
Huu uzi umekuwa inspirational kwangu 'na umenifanya nikasepa hom 'na kuanza maisha mapya tena kwa haraka saana bilabila kutizama nyuma kikubwa kilicho nipelekea kufanya maamuzi magumu ilikuwa n mishe za foleni kufungua mahotpot kila siku halafu mshua naye anakupa makavu kiaina japo hakwambiii ila utajiongeza tu mwenyewe
Namshukuru mungu nilianza japo kigumu sometime unahustle hadi kijiakili cha kurudisha mpira kwa kipa kinakuja lakini ukifkiria ushajikusanya mazaga kibao ukirudi itakuwa shangwe kwa wanga mtaani 'na hapo ndipo unapozidisha hustle ili uendeleze jahazi ulilolianza 'na kuepuka aibu .
Ila ukweli ni kwamba sasa nina amani tena sanaa 'na akili pia imekuwa ninawaza mbaali sanaa tofauti 'na nyumbani .
Ikumbukwe kwamba nyumbani nimeaacha room mbili za wazi lengo sio kukimbia ila lengo ni KUJITAMBUA KAMA MTOTO WA KIUME NA BABA WA FAMILIA FULANI BAADAYE maana ukizoea nyumbani kinachofuata ni kuja kugombania mali za urithi 'na wadogo zako
Ushauri: vijana tusiogope kuanza 'na kuhamia ghetto maisha ya gheto sio sawa 'na nyumban kila kitu free akili inalemaa