Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Kipindi Niko chuo siku za weekend nachomoka mara home kwa mzee, mara kwa bi.mkubwa, mara Kwa washkaji… sasa nikienda weekends kwa wana nakuwa inspired kinoma! Mpaka sometimes likizo Naweza kutumia hadi week mbili kwa washkaji staki tena kwenda maskani, baada ya wanangu kumaliza mmoja akaenda Ulaya mmoja akapata kitengo Mkoa fulani kwa sababu kwao walikuwa na watu upande wa ujombani. Kipindi wana wana-separate mimi Niko home kwa Bi.mkubwa life ikaanza kuwa michosho hamna michongo wala nini na kama unavojua nyumbani dharau na kejeli+ nyodo Hasa kutoka kwa madogo huwa haziishi. Sasa pale home bi.mkubwa alikuwa kaolewa tu inamana sio kwetu kwa “100%” mzee mzima nikawa Uncomfortable siku moja nilivurugwa vibaya mno mapema alfajiri nikasepa kuelekea Magomeni kwa jamaa zangu wengine ambapo ni nyumbani kwao na mwanangu mwingine wa Karibu sana ambaye yuko Mamtoni kitambo tangu tuko O-level ila bahati nzuri ukaribu na urafiki wetu wa kushibana ulikaribisha undugu mpaka nikaweza kukaa kwao bila pingamizi. Kama zali baada ya kukaa pale siku kadhaa rizk ikawa inapatikana na mfukoni sikaukiwi ingawa ugenini ni ugenini tu Sio wote walipenda uwepo wangu pale. Msimamizi wa ile nyumba ambaye alkuwa ni shangazi yake na mwanangu alinipenda sana na kuniamini kutokana na nidhamu na uaminifu kiasi kwamba mpaka kunishirikisha maswala kadhaa ya familia… kimbembe kikaja kuna shangazi yake mwingine wa huyo mwanangu ambaye nilienda kuishi kwao kutokana na ups and down za familia alikuwa anaishi mtoni na yeye sasa akaja bongo kula goodtime na kufatilia michongo yao mingine huku bongo ya ujenzi na biashara zao akanikuta naishi pale na kabla alipata taarifa. Dahh! Yule shangazi hakupenda kabisa uwepo wangu pale na akaagiza niondoke. Kwa sababu mwenye pesa ana kauli yule shangazi wa kwanza msimamizi wa mjengo hakuwa na namna akaniita na kuniweka wazi. Nikiwa kwenye tathmini nikapokea simu kutoka majuu hakuwa mwingine bali ni Mama mzazi wa rafiki yangu na akanitaka nibaki hapo kwa sababu mwana tayari nilimchana kila linaloendelea maishani kwangu kipindi hicho. Siku zilizidi kusogea ingawa maisha yalikuwa mazuri ya amani pale na utulivu lakini maneno ya chini chini yalikuwepo. Shangazi msimamizi wa nyumba anazidi kuwa pressurized kutoka kwa Dada’ake kwamba kijana aondoke hapo sasa ukawa mvutano kati ya mawifi dhidi yangu. Nikaona isiwe kesi nikiwa katika maandalizi ya kusepa mwanangu akanivutia waya akaniambia siku si nyingi nakuja bongo usiondoke kwanza. Mwana akaja na life ikawa inaendelea Kumbe mwanangu alikuja na Neema. Alijua wazi mwanae sina kitu na Niko kwenye situation ngumu ingawa rizq ya pesa za vocha na kubadili mashati inapatikana. Akanipatiaga kitita kirefu cha pesa nakumbuka ilkuwa baada ya mwezi mtukufu na baada ya sikukuu ya eid mnamo mwaka fulani. Nikafanye mafekechee ya kutafuta chimbo maeneo fulani maeneo ya Mikocheni “A” uswahilini ambapo Nlkuwa na mwanangu mwingine anaishi kule lakini alikuwa anafanya kazi dukani. Ikabidi aniunganishe na wana wengine ambao ni ndugu zake tukawa tunakaa ghetto moja. Nikarudi Magomeni na kuaga baada ya kuweka mambo sawa na nikaanza maisha rasmi kama mpangaji. Life ikasonga na siku zikasogea wale wana niliokuwa naishi nao wakapata kazi sehemu tofauti hivyo wakalazimika kuhama… mmoja akaenda Visiwani mmoja hapahapa Dar maeneo ya kawe karibia na Mbezi kamanda nikabaki peke yangu tena ingawa sikupapenda maeneo yale kutokana na mazingira machafu na palikuwa uswahilini nikasubiri kodi iishe… baada ya muda nikapata mchongo ukaniongezea pesa kidogo ikabidi nihame sasa nikahamia Mikocheni “B” ambapo ghetto hata unaweza kumleta demu akagoma kuondoka [emoji1][emoji39][emoji1786] na baada ya wiki chache nikapata kibarua ofisi fulani maeneo ya Mbezi beach. Safari ya maisha ikaanzia hapo ingawa si haba Hohehahe anasongesha siku
Umepambana sana keep pushing
 
Hivi Kuna mtu ana 38yrs anaishi geto?? Aiseee! Umri huo kijana anatakwa awe na familia kwa maana mke na watoto. Sasa utaishije geto mzee mzima?
Mkuu mambo huwa yanagoma, yanayumba, kuna kufilisika, kuuumwa, kuhujumiwa ndg yangu unaamua kurudi nyuma na kujipanga upya.

Maisha ni kitabu kina kurasa nyingi na kila ukurasa una habari zake.
 
Umekazia sana mkuu! [emoji1477][emoji1488]

Nashkuru Mungu niliyajua haya mapema na niliishi ndani ya misingi hiyo… siku zikasogea na Mungu akanionesha njia

Ni nukta muhimu sana za kukazia kwa vijana walio kwenye hatua za kutafuta katika maisha binafsi.
Ahsante mkuu! Nimeona nikazie kwenye Uzi wako maana nimekumbuka mbali sana,umenikumbusha kitu muhimu kwenye historia ya maisha yangu maana hata mimi niliwahi kuishi na watu baki na ndio walionisaidia.

Halafu wanawake na mashemeji niliowakuta kila nilipokuwa nikienda nilikuwa nikiishi nao vizuri sana kwa heshima na adabu.

Tamaa niliziweka pembeni pamoja na mitego yao, hakuna kitu kibaya kama kuingilia mapenzi ya watu. Yaani umekaribishwa kwa watu unaanza kutamani vidada ulivyovikuta na wake au wapenzi wa kaka zako. Hii siyo poa unajitengenezea mazingira magumu.

Mkuu mimi baada ya kufanikiwa kiasi fulani niliwapelekea zawadi japo kidogo lakini kuonyesha moyo wa shukrani. Japo wengine sijui hata wako wapi ,ila niliobahatika kuwaona niliwashukuru kwa wema wao.

Yaani hata kama unaishi nao nyumba za kupanga unawapa heshima zao,wakikuomba msaada wa kazi ambazo unaziweza fanya ilimradi hazikuondolei utu wako na heshima yako.

Mimi ninaamini kama kijana ukiweza kuishi na watu baki vizuri huku ukivumilia madhaifu yao mpaka unafanikiwa na kuamua kuanzisha mji wako huwezi kushindwa kwenye maisha wala kuishi na mke wako.

Maana walimwengu ni shule tosha wadogo zangu, wengi hapa ni wadogo zangu maana nimekuwa ghetto kitambo sana.

Ahsante!!
 
Hivi Kuna mtu ana 38yrs anaishi geto?? Aiseee! Umri huo kijana anatakwa awe na familia kwa maana mke na watoto. Sasa utaishije geto mzee mzima?

Wapo kiongozi… maisha hayana kanuni bali ni kufanya kazi kwa bidii na kujituma ikitokea umepata fursa. Mbona ni wengi tu bado wako kwenye single room na umri umesogea
 
Ahsante mkuu! Nimeona nikazie kwenye Uzi wako maana nimekumbuka mbali sana,umenikumbusha kitu muhimu kwenye historia ya maisha yangu maana hata mimi niliwahi kuishi na watu baki na ndio walionisaidia.

Halafu wanawake na mashemeji niliowakuta kila nilipokuwa nikienda nilikuwa nikiishi nao vizuri sana kwa heshima na adabu.

Tamaa niliziweka pembeni pamoja na mitego yao, hakuna kitu kibaya kama kuingilia mapenzi ya watu. Yaani umekaribishwa kwa watu unaanza kutamani vidada ulivyovikuta na wake au wapenzi wa kaka zako. Hii siyo poa unajitengenezea mazingira magumu.

Mkuu mimi baada ya kufanikiwa kiasi fulani niliwapelekea zawadi japo kidogo lakini kuonyesha moyo wa shukrani. Japo wengine sijui hata wako wapi ,ila niliobahatika kuwaona niliwashukuru kwa wema wao.

Yaani hata kama unaishi nao nyumba za kupanga unawapa heshima zao,wakikuomba msaada wa kazi ambazo unaziweza fanya ilimradi hazikuondolei utu wako na heshima yako.

Mimi ninaamini kama kijana ukiweza kuishi na watu baki vizuri huku ukivumilia madhaifu yao mpaka unafanikiwa na kuamua kuanzisha mji wako huwezi kushindwa kwenye maisha wala kuishi na mke wako.

Maana walimwengu ni shule tosha wadogo zangu, wengi hapa ni wadogo zangu maana nimekuwa ghetto kitambo sana.

Ahsante!!

Busara kubwa sana! Nazidi kupata shule kutoka kwako kiongozi…, nazidi kujifunza [emoji1488]
 
Busara kubwa sana! Nazidi kupata shule kutoka kwako kiongozi…, nazidi kujifunza [emoji1488]
Karibu sana mkuu. Mwanzilishi wa huu uzi tumpe big up maana unasaidia vijana wengi kupata upenyo wa kuanza maisha.

Siku nikipata muda mzuri nitaweka kisa changu jinsi nilivyoanza life na wenzangu mpaka nilipofikia.
 
Ghetto ninaloishi lina mkeka,ndoo ya maji na mifuko yangu ya nguo..napambana nafanya biashara ya kutembeza bidhaa za urembo.wiki hii mambo ni mazuri jumatatu mauzo yalikuwa 37,000 leo 26,000 napambana kutafuta hela pia nasali sana ili mwaka 2023 nije kuwa na ghetto zuri lenye vitu vizuri ndani..

Matumizi yangu hayafiki 5000 kwa siku na mara nyingi ni chini ya 4000 hela ya kula naitoa kwenye biashara hii hii ambayo niliianza jumatano iliyopita hadi jumapili nilipumzika niweza kusave 63,000 hadi leo na nimeshatoa hela ya kwenda kuongeza vitu kesho kariakoo..

Lengo langu niongeze biashara ya pembeni ili inigharamie bill zangu za kila siku.Lengo langu la mwaka ujao niwe na ghetto zuri lenye vitu vizuri ndani vilevile ninunue bodaboda hata ya mtumba iniingizie pesa na vilevile niwekeze kwenye kilimo kama sitafanikiwa katika yote hayo matatu basi at least hayo malengo mawili yatimie.

Uzi huu umenigusa sana hadi nmeamua kuishi mwenyewe kwangu kiukweli sijawahi kuandika post ndefu kuliko hii hapa JF ila kwa hisani ya uzi huu nimeshare jambo langu smartphone yenyewe ninayotumia ni majanga panapo majaaliwa nitaleta mrejesho wa maendeleo ya biashara na picha ghetto langu kwa sasa..

Roger that!
 
Mungu abariki harakati zako mkuu!
 
Umenifurahisha uliposema unasali sana. Ibada ni nzuri inakuondolea msongo wa mawazo na kutokujihusisha kwenye vikundi viovu.

Weka malengo usitumie pesa katika vitu ambavyo hujavipangilia au haviko kwenye malengo yako.Achana na anasa kabisa.

Hakikisha kila pesa unayoitoa kufanya manunuzi au matumizi yako unaiandika kwenye daftari ili utunze kumbukumbu vizuri.

Kabla hujatoka nyumbani, weka kumbukumbu vizuri umeondoka na kiasi gani cha pesa ili ukirudi ujue umepata shilingi ngapi na umetumia kiasi gani.

Jambo la muhimu la kuzingatia. Ukishaanza kupata pesa majukumu yanaanza kukusogelea, jipe majukumu unayoyamudu ambayo yako juu yako achana nayo.

Uwe na kiasi kwenye kutoa misaada, jiulize unayemsaidia, siku ukianguka atakuinua?Jiangalie wewe kwanza wengine baadaye.

Jiepushe na mapenzi, labda kama umri umeshaenda, kumuhudumia mtu,au mimba na kuoa huku hujajipanga inaweza kukuharibia malengo.

Ukiona kipato chako kimeongezeka ongeza kiwango cha elimu kwa fani uipendayo,hii itakupa kujiamini na kuwa na maarifa zaidi. Ni vizuri kusoma ukiwa bado hujakuwa na majukumu mengi.

Usishindane na mtu kwenye vitu vya anasa bali katika maendeleo, na usiwachukie waliofanikiwa na wanaofanikiwa bali jifunze wamefanikiwaje ikiwa wewe bado.

Ni hayo tu machache kwa leo.

Ahsanteni.
 
Nlipost hiii mwaka 2020 na badae December mwaka huo huo nikawa nasepa maskan kwenda kuanza maisha kitaaa bila kuwa na mishe yoyote. Kiukweli nilipiga kazi yoyote iliokuja mbele yangu na hiii ikansaidia kukutana na washikaj mbalimbali ambao ikasaidia kupeana michongo. Hadi Sasa npo get naona hatua zinaenda ila kwa mwendo wa Kobe.
Safi sana,usikate tamaa, keep hustling.
 
Back
Top Bottom