Ghetto ninaloishi lina mkeka,ndoo ya maji na mifuko yangu ya nguo..napambana nafanya biashara ya kutembeza bidhaa za urembo.wiki hii mambo ni mazuri jumatatu mauzo yalikuwa 37,000 leo 26,000 napambana kutafuta hela pia nasali sana ili mwaka 2023 nije kuwa na ghetto zuri lenye vitu vizuri ndani..
Matumizi yangu hayafiki 5000 kwa siku na mara nyingi ni chini ya 4000 hela ya kula naitoa kwenye biashara hii hii ambayo niliianza jumatano iliyopita hadi jumapili nilipumzika niweza kusave 63,000 hadi leo na nimeshatoa hela ya kwenda kuongeza vitu kesho kariakoo..
Lengo langu niongeze biashara ya pembeni ili inigharamie bill zangu za kila siku.Lengo langu la mwaka ujao niwe na ghetto zuri lenye vitu vizuri ndani vilevile ninunue bodaboda hata ya mtumba iniingizie pesa na vilevile niwekeze kwenye kilimo kama sitafanikiwa katika yote hayo matatu basi at least hayo malengo mawili yatimie.
Uzi huu umenigusa sana hadi nmeamua kuishi mwenyewe kwangu kiukweli sijawahi kuandika post ndefu kuliko hii hapa JF ila kwa hisani ya uzi huu nimeshare jambo langu smartphone yenyewe ninayotumia ni majanga panapo majaaliwa nitaleta mrejesho wa maendeleo ya biashara na picha ghetto langu kwa sasa..
Roger that!
Umenifurahisha uliposema unasali sana. Ibada ni nzuri inakuondolea msongo wa mawazo na kutokujihusisha kwenye vikundi viovu.
Weka malengo usitumie pesa katika vitu ambavyo hujavipangilia au haviko kwenye malengo yako.Achana na anasa kabisa.
Hakikisha kila pesa unayoitoa kufanya manunuzi au matumizi yako unaiandika kwenye daftari ili utunze kumbukumbu vizuri.
Kabla hujatoka nyumbani, weka kumbukumbu vizuri umeondoka na kiasi gani cha pesa ili ukirudi ujue umepata shilingi ngapi na umetumia kiasi gani.
Jambo la muhimu la kuzingatia. Ukishaanza kupata pesa majukumu yanaanza kukusogelea, jipe majukumu unayoyamudu ambayo yako juu yako achana nayo.
Uwe na kiasi kwenye kutoa misaada, jiulize unayemsaidia, siku ukianguka atakuinua?Jiangalie wewe kwanza wengine baadaye.
Jiepushe na mapenzi, labda kama umri umeshaenda, kumuhudumia mtu,au mimba na kuoa huku hujajipanga inaweza kukuharibia malengo.
Ukiona kipato chako kimeongezeka ongeza kiwango cha elimu kwa fani uipendayo,hii itakupa kujiamini na kuwa na maarifa zaidi. Ni vizuri kusoma ukiwa bado hujakuwa na majukumu mengi.
Usishindane na mtu kwenye vitu vya anasa bali katika maendeleo, na usiwachukie waliofanikiwa na wanaofanikiwa bali jifunze wamefanikiwaje ikiwa wewe bado.
Ni hayo tu machache kwa leo.
Ahsanteni.