Ulichokipata wewe kwa gharama wengine walikipata Kkwa bei sawa na bure

Ulichokipata wewe kwa gharama wengine walikipata Kkwa bei sawa na bure

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Wakati wewe ulitumia mamilioni ya pesa kufaulu Kidato cha nne, kuna wajuba gharama zao Kwa ujumla tangu Kidato cha Kwanza mpaka cha sita hawafikishi hiyo milioni Moja. Hivyo usiringe Sana Utaonekana mshamba tuu!

Wakati wewe ulitumia mamilioni ya Pesa kupata Pisikali Fulani, kuna Wakulungwa hawatoi hata Mia na wanapata wanawake wazuri kama huyo unayemgharamikia vile watakavyo.

Wakati wewe ulitoa mahari milioni Nne mpaka kumi ili kuoa mwanamke huyo anayekupasua kichwa sasa hivi😉😉 kuna wajuba mahari zao hazifiki hata laki moja na wake zao ni wazuri na wanaishi maisha ya Raha mustarehe.

Wakati wewe ulinunua Gari hilo unalotembelea Kwa gharama kubwa, kuna Wazee WA connection wamenunua Gari hiyo hiyo Kwa bei karibu na nusu bei ya uliyonunulia Gari yako.

Wakati wewe unatumia mamilioni ya Pesa kujilinda dhidi ya wezi na Majambazi na bado unalala Kwa wasiwasi, kuna wakala nje wanalala Kwa Raha mustarehe pasipo hofu yoyote.

Wakati wewe unahangaika upate Jambo Fulani labda ni KAZI au elimu au makazi ili uheshimike, kuna wenzako hata uwe na vyote hivyo bado watakuona mbulula tuu!

Kiufupi,
Maisha yanahitaji Kuridhika, na kutokujipa Stress. Usijitese!
Usi-complicate maisha, fanya Jambo lililo ndani ya uwezo wako. Kanuni inasema usivuke mipaka.

Maisha yanatabia ya kukurudisha kwenye Mpaka wako pale unapovuka mipaka,
Ukihangaika kutumia pesa nyingi ili upate kitu Fulani ambacho sio saizi yako fahamu kuwa Maisha yatakurejesha Kwa aibu katika nafasi yako.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Iringa,
 
siti ya mbele hapa, ila kwa wengine ml kumi ni kama laki na wengine laki ni kama milion kumi

Ni kweli kabisa,
Kanuni inasema "ajikwezaye hushushwa, na ajidhiliye hukwezwa"
Ndio maana matajiri ni nadra Sana kusikia wakijisifu Kwa sababu wanaona ni ushamba kujisifu kitu ambacho kuna watu wametumia nguvu ndogo kukipata ilhali wao wamehangaika usiku na mchana
 
hayo unayasema tu kulingana na hali yako.

Pahali napoishi mmiliki wake ni mvuvi anamiliki mitumbwi mingi tu ya uvuvi.

Kama tunavyofahamu sehemu za uvuvi haswa visiwani hakuna bank so inamlazimu kusafiri na pesa hadi mjini.

Nayeye alikua na hizo falsafa za siwezi kujipa presha ya kuweka ulinzi nyumbani kwangu, sikumoja aliingia mjini muda umekwenda bank zimefungwa alipokonywa M20 nyumbani kwake.

Hadi sasa tunavyozungumza anamiliki bastola na nyumbani kwake kuna mifumo ya ulinzi.

Binafsi japo sina mali ila popote napokua swala la ulinzi wangu na ninavyomiliki ni kipaumbele namba moja
 
Back
Top Bottom