Mimi personally sijawahi ila nakumbuka kuna rafiki yangu alilea mtoto hadi kafika miaka 5 ndipo akapata wasiwasi kutokana na mwenendo wa mwanamke kuwa na kiburi na kufumania mawasiliano ya simu ikabidi azuge amchukue mtoto wakatembee akaenda nae hospital na kupima vinasaba ndipo ikaonekana sio mtoto wake kwa 98% hawana vinasaba vya kufanana.
Kijana alikuja na karatasi hadi kwa bibi mzaa mama wa mtoto yaani mkwe au mama wa mwanamke. Akaja muonyesha ajionee. Binti anapigiwa simu anaanza kuwaka kwann anampeleka mtoto hospital bila ridhaa yake.
Akaitwa kwenye kikao hakutokea anakwepa. Jamaa aliondoka ila dah nilifeel yale maumivu namna alikuwa anajikaza asilie huku macho yamefura kwa hasira na huzuni. Akikumbushia miaka yote hii amehangaika kukata bima, kulipa ada, kuja kumtembelea mtoto kila weekend, kumtoa out kumpeleka sehemu za watoto acheze na wenzake.
Mbaya zaidi tukiwa kwenye hiki kikao mtoto akaingia kutoka shule ameona gari ya baba yake akaja kasi na kumrukia baba yake kama kawaida yake jamaa akajitahidi tu kucheka ili mtoto asijisikie vibaya.
Dah ile moment iliniuma sana hadi leo nikikumbuka huwa kuna huzuni kali sana inanivaa. Mtoto nasikia anamuuliza bibi yake baba atakuja kunichukua twende kutembea kule kwa bibi (akimaanisha bibi mzaa baba yake). Na mtoto anajua kupiga simu kuna siku alichukua simu ya bibi yake akapiga sana namba ya baba yake hadi akapokea wakaongea. Jamaa hiyo kitu inamuuma sana aisee.
Watoto wakike huu ushetani wa uzinifu huwa unazaa sumu kali sana kwenye jamii na madhara yake ni makubwa, mnakuja kuweka laana kwenye koo zenu na watoto wenu.
Shenzi sana. Dah [emoji25]