Nilikua nipo Vidato kadhaa, kuna kabinti tulikua tunadate, siku moja tukaenda beach, nipo nambambia mwenyewe, mabusu ya hapa na pale, chezeya kiuno kwa sana asalaleee mdogo wa kiume huyu hapaaa daah binti akamtisha tisha pale asiende kumsemea, walivyofika home dogo kamwaga kila kitu.
Mida ya saa mbili usiku mama ake binti, dada zake wawili, kaka ake mkubwa na binti mwenyewe hao hadi home, Mama ndio aliwafungulia binti kapigika kichizi, kesi ikaunguruma hapo mnyamwezi nikakataa.
Mama acha aanze kunitetea mwanae sina tabia hizo, kaka zangu wakaitwa nao ikawa zogo mimi nimetulia namcheki kipenzi changu alivyoumuliwa uso natamani nimrukie kichwa kaka ake ila ndio hivyo tena nishakataa na binti nae alikataa hakua na mimi, mwisho wa siku wakaondoka.
Halikuongelewa tena hilo suala hapo ndani nikajua tu nimemuumiza Mama yangu kipenzi ila maBro wenyewe walikua fresh tu afu walikua wananikubali kinyama,
Binti alipelekwa Boarding School na mimi nikajiapiza sita date na binti wa Mtaani, Shule au Kazini, hadi leo naishi na hiyo principle.