Nakumbuka nilikua fom ii,bangi ilikua imekolea kichwani halafu napendwa sana home...
Nlikamatwa asembo paredi,na kete 4 za bangi nimechomeka kwenye soksi.
Wakati nabishana na mwalimu,nikazibugia mdomoni.
Wakawaita wazazi(alikuja mama),alipoambiwa kosa langu.Alilia sana kunitetea mpaka akawaambie wanipe kitabu cha mungu(Qur`aan) nisome ili waamini hata nikiwa home me ni mtu wa dini,Nilisamehewa.
Aliporudi home akatipitiliza mpaka kwenye nyumba tunayokaa,akaingia mpaka chumbani kwangu.
Akakuta kisado kimejaa zinde za ganja,shungi za sigara,paketi za viroba(power no.1).
Alilia sana,sanaaaa