Ulifanya 'Kisanga' gani ambapo Mama yako alikutetea kwa Nguvu zote ili kukuokoa?

Ulifanya 'Kisanga' gani ambapo Mama yako alikutetea kwa Nguvu zote ili kukuokoa?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Hapo kwa ** ubao usome 1-1**
[emoji16] Mkuu ni kama Hali flani hv unapata ZERO na familia yote inajua kuwa ni ZERO ila Bi.mkubwa pekee anajua umepata Zero ila anaamini ni One isiyochangamka[emoji1787]. Ile promo aliokuwa ananipa huwezi amini hata mm ilibaki kidogo nikatie rufaa matokeo.
 
Heheh ngoja na mimi niweke kisa changu, miaka kadhaa iliyopita nikiwa form 3, kuna mtoto mmoja wa kisabato alitokea kunielewa,kiukweli ile Pisi ilinielewa sijawahi kuona..yeye alikuwa form 4 ila shule tofauti...
Ungemuoa huyo... Aliyekufanya mtoto wa kiume kupata mhaho
 
[emoji16] Mkuu ni kama Hali flani hv unapata ZERO na familia yote inajua kuwa ni ZERO ila Bi.mkubwa pekee anajua umepata Zero ila anaamini ni One isiyochangamka[emoji1787]. Ile promo aliokuwa ananipa huwezi amini hata mm ilibaki kidogo nikatie rufaa matokeo.
Bi mkubwa alitisha mkuu 🤝🤝🤝🤣🤣🤣🤣
 
Kuna binti nilikuwa namfukuzia wakati nipo primary darasa la sita, sasa akawa anachomoa. Siku moja naenda mtoni ilikuwa jumatano nikamwona peke yake anafua. Nilichofanya nikaiba sabuni tu kabla hajaniona, yeye si mjanja!

Nilipoibuka nikaona anahangaika kutafuta soap yake. Nikampa pole sana, kisha nikamwambia achague jambo moja kati ya mawili;

° anipe penzi kisha mimi nitaenda kumpa mche mzima wa sabuni nyumbani (ni kweli ningeenda kumwibia nyumbani maana zilikuwepo kweli)
° afulie masilu (haya ni majani fulani walikuwa wnafulia wahenga, yanatoa povu kama sabuni)

Akaniambia hafanyi vyote, yaani sipati penzi na hafulii masilu na nikifika nyumbani nina kesi.
Nikamwambia achana na mimi, nikaendelea na michezo yangu hadi usiku.

Usiku ulipofika nikaenda nyumbani nikaiba mzigo wa kuni niliookota jana yake halafu nikautua kwa nguvu kisha nikazana jikoni ili nipate menyu kama kawaida ninavyotoka kazini.
 
Wakati naingia jikoni nikamkuta yule binti, mama yake na dada yake kumbe walishatangulia kutoa mashitaka.
Baada ya kuonekana nina kesi ya kujibu kwa tuhuma mbili. Kwa kuomba penzi na kuiba sabuni ya yule binti maana ilipotea katika mazingira ya kutatanisha tulikuwa wawili tu mtoni.

Aisee pale nyumbani wakawa kama wamebanwa na kicheko kwamba tangu lini mimi nikaiba soap, yaani motheq alinitetea kishenzi coz mimi mambo ya kufua sikuwa na interest nayo kabisa. Huwa nakabidhiwa sabuni lakini naitelekeza bila kufua, zikaoneshwa na za mchana wake na nguo ambazo sijafua nimeziloweka tu.

Ikabaki tuhuma moja ya kutaka kujipatia penzi kwa njia za udanganyifu.

Hiyo nayo sister alinisaidia.

Ila siku ya pili akaniuliza ni kweli mdogo wangu ulifanya haya? Nikakubali akasema usirudie, kuna ukimwi.
 
Siyo kiasi hicho, usela tena wa kidato Cha pili. Sema wahenga wanasema baada ya dhiki faraja.

Kila nikimuangalia binti yangu ambaye sasa amenizidi urefu, Basi nabaki nacheka, nikikumbuka nilivyolala selo😀😀😀😀😀
Ulikua mtundu sana wewe... Duuuh 😳
 
Siyo kiasi hicho, usela tena wa kidato Cha pili. Sema wahenga wanasema baada ya dhiki faraja.

Kila nikimuangalia binti yangu ambaye sasa amenizidi urefu, Basi nabaki nacheka, nikikumbuka nilivyolala selo😀😀😀😀😀
🤣🤣🤣😂😂😂😂 Dah nimecheka kwa sauti aiseeee
 
Back
Top Bottom