Ulifanya 'Kisanga' gani ambapo Mama yako alikutetea kwa Nguvu zote ili kukuokoa?

Ulifanya 'Kisanga' gani ambapo Mama yako alikutetea kwa Nguvu zote ili kukuokoa?

Enzi hizo nipo chuo ..nilienda home weekend na Baba hua ana kawaida ya kunipa pesa nikifika tu home hata iwe usiku ataniamsha..Basi bana siku moja kaniachia zake pesa kaenda job Kuna kipindi hua kazini kwao wanaenda katikati ya bahari huko Basi atakaa hata week..Sasa namimi si nilijua mshua harudi Hadi week ipite bana..nikavuta sikwenda hostel jpili coz j3 nilikua na miadi na shemeji yenu😊.
J3 bimkubwa kaenda zake kibaruani mida imefika nikaonane na shemeji yenu mara moja Kuna pesa aliniletea na alinihamu kuniona..ni kituo kinachofuata baada ya home nikafunga zangu milango Mimi huyooo..ile nafika tu eneo la tukio naingia tu geti la ile bar nakutana na Baba macho kwa macho..😂😂imagine anajua nishasepa hostel🤣🤣.
Nikasema sirudi nyuma nikamsogelea salamu..akaniuliza vipi hapa ndipo hostel!!?..nilibaki naunyaunya na mbaya zaidi mwamba nae alikaa kwenye Kona ambayo nikipiga jicho naonana nae..lilivyozoba linanipa ishara nipo hapa njoo😣..aisee..najaribu kumkazia macho lakini wapi..si akanyanyuka ilibidi niwasiliane na kwa kichwa atoke pale aende nje..Baba anajifanya anaangalia simu yake Kama haoni..akaniruhusu nisepe.

Jioni Sasa huyu hapa karudi..maswali yakaanza nabaki tu kutumbua macho..Mama anasema nimemuacha nyumbani huyu alitoka muda gani..unamsingizia mtoto..baada ya kuona mabishano mengi kidogo niropoke ..Mama akamuwahi Baba .."nimekumbuka nilimtuma aende akachukue pesa kwa mteja wangu..wewe nawe kwanini hukuniambia Kama ulienda"..hapo Mama kanikazia jicho..hapo ndipo nilipata ahueni na kulala nikaenda hata kula sikula.. nikikumbuka ile siku 😂😂😂😂
 
Sehemu ya kukutania ndo ilikua shida.... Mama alijua kukutetea 😂😂
 
Sehemu ya kukutania ndo ilikua shida.... Mama alijua kukutetea 😂😂
😂😂 Kwakweli
Alinitetea mpaka nikashangaa..Mama angu hakua mtu wa sport sport..hakupenda ujinga mpaka tukampa jina la mjeda mstaafu lakini ile siku😂😂..nilimuaminia
 
😂😂 Kwakweli
Alinitetea mpaka nikashangaa..Mama angu hakua mtu wa sport sport..hakupenda ujinga mpaka tukampa jina la mjeda mstaafu lakini ile siku😂😂..nilimuaminia
Dady alimuona kijana aliyekuita eneo la tukio maana kesi mbona ilimalizwa chap hivo
 
Nilikua nipo Vidato kadhaa, kuna kabinti tulikua tunadate, siku moja tukaenda beach, nipo nambambia mwenyewe, mabusu ya hapa na pale, chezeya kiuno kwa sana asalaleee mdogo wa kiume huyu hapaaa daah binti akamtisha tisha pale asiende kumsemea, walivyofika home dogo kamwaga kila kitu.....

Mida ya saa mbili usiku mama ake binti, dada zake wawili, kaka ake mkubwa na binti mwenyewe hao hadi home, Mama ndio aliwafungulia binti kapigika kichizi, kesi ikaunguruma hapo mnyamwezi nikakataa, Mama acha aanze kunitetea mwanae sina tabia hizo, kaka zangu wakaitwa nao ikawa zogo mimi nimetulia namcheki kipenzi changu alivyoumuliwa uso natamani nimrukie kichwa kaka ake ila ndio hivyo tena nishakataa na binti nae alikataa hakua na mimi, mwisho wa siku wakaondoka, halikuongelewa tena hilo suala hapo ndani nikajua tu nimemuumiza Mama yangu kipenzi ila maBro wenyewe walikua fresh tu afu walikua wananikubali kinyama,

Binti alipelekwa Boarding School na mimi nikajiapiza sita date na binti wa Mtaani, Shule au Kazini, hadi leo naishi na hiyo principle.
Uwongo
 
Dingi yangu ukizingua unakula ngumi mateke,mikato flan ya Bruce Lee,Maza ukizingua anakubonda Kama mke mke mwenzie,ukitoka nduki anakuungia tela aisee...muda wa kipigo hakuna wa kukutetea yaani
🤣 Khee! hatari.
 
Mama yangu hajawahi kunitetea hata dakika Moja
Yeye ndo kwanza alikua ananipiga mboko za kutosha.. nabeba vichechi pale Mezani... kuchelewa kurudi toka shuleni ...
Nikitumwa nachelewa kurudi zile timings anazo nipa michezo mingi sana ..
Ni fimbo tu na mazoezi magumu...
Hallo bila yeye kunikazia Leo nisingekua hapa kama Smart Gang ningekua Mdudu mtu ...
Leo naona madogo wanazingua kisa kazeeka yule Hana tena yale makali yake akiwa na umri wa makamo ...
Lakini nampenda kwani kantengeneza kuja kuwa kiongozi mzuri Leo hii..
Nidhamu ndo kila kitu kila mahali.
 
Sana tu mpaka sikumbuki ni mara ngapi.

Ila ninayo kumbuka nikiwa chekechea nikashindwa maswali ma tano baba akaniita akanipa maswali mengine ya hesabu baadhi nikashindwa aiseee baba alinipigaaa akamwambia mama huyu akifikisha miaka 7 anatakiwa kwenda nairobi kusoma kwa hiyo hakuna cha kumuonea huruma lazima apatie hayo maswali.

Na mama haruhusiwi kunisaidia hata swali moja. Kwenye maswali yake tofauti na yale ya shule nikashindwa mawili weeee alinitoa nje akanifunga mkono kwenye mgomba akasema wasinipe chakula, mama alilia akilalamika mimi ni mdogo🤣 wakaingia ndani kula hapo ni kama saa mbili usiku mama akaiba chakula akanilete weee hiyo vita ilikuwa kali.
Baadae kama saa 4 baba akaja akaniambia ili nitoke pale nimwambie table ya kwanza hadi ya tatu hiyo nilikuwa naiimba kila siku nikaisoma ndo nikatoka.

Aliponitoa akaniambia wewe ni mtoto wangu wa kwanza mimi sikusoma sana nataka usome tena ukifika miaka 7 ukajua kujiogesha utasoma nairobi sawa mwanangu? Ninakupenda sana lazima uwe na akili.
I feel so bad about this
 
Najitahid lakini wapi nilijitaidi kumtetea mtu mzima chuoni kipindi nipo CR alipata disco lakini wakati na mtetea nikalopoka lakini amezidi umbea wenzie wanasoma yeye yupo bise kusaka umbea [emoji23][emoji23][emoji23] dah mpka yule mama aliona aibu af nimekaza jicho
Wewe hufai 🙌🙌🙌
 
Back
Top Bottom