Daah wakuu acha niwape story.
2014 niliamishwa shule na mama na kunipeleka shule ingne wilayani kumbuka mwanzo nlikuwa naskuli city center kbsaa sasa hii ni baada ya mama kuona uhuni umenijaa sana apa mjini.
Sasa bhana iyo shule nlioenda walikuwa wanasoma somo la Agriculture na mimi sikuwahi lisoma kbsaa na apo school nliamia j"4 so wanafunz wenzangu wakawa wananiambia wewe kesho ni test ya agriculture na mwalimu huwaga hajui cha mgeni wala nini we soma, me nkakaza shingo bhana si j5 ikafka na ticha wa agric akaja asee alikuwa anaogopeka shule nzima yaani yule mwamba alikuwa anagonga viboko hatari.
Yaan alipoingia tuu class akasema wote lazeni vichwa kwenye dawati, then akaandika maswali ubaoni, after akasema chaneni karatasi mna dakika 10 tuu za kujibu haya maswali, maswali nayakumbuka mpaka leo yalikuwa hivi
1. a) What is weed?
b) What is weeding?
2. Merits and Demerist of weed
3. Methods of controlling weed
4. Mention 5 common weed
Sasa bhana wenzangu wakawa bize na kujibu maswali, uku mimi nikipekua pekua daftari langu jipya likiwa halina neono lolote ndani zaid tu ya jina kwenye cover, Si teacher akaniona akajua naigia kwa kupekua daftari akaja mpaka nilipo na kusema-:
Teacher: Simama juu na weka kila kitu chako kwenye dawati ad mda wa test utapoisha hakuna kuandika chochote,
Me: Mwalimu mimi ni mgeni nimeamia jana na nlipotoka hili somo halipo
Teacher:Nimekwambia simama juu sitaki kujua we ni mgeni na umefundishwa agriculture au vipi we subiri si iyo karatasi yako umeandika jina?
Me: ndiyo
Basi bhana nilovyomjibu ye akaendelea zake kuzunguka zunguka darasani akikagua wanafunzi wasiigie na mda ulipoisha akakusanya karatasi zake na kuzisahihisha. na alipomaliza akatugawa kutokana na score apa sasa ndo show inaanza.
Teacher: Kama umepata 0-40 pita mbele, 41-59 kaeni kati kati, 60-79, kushoto na 80-100 kaeni kulia. Kama una 0-40 viboko ni 9, 41-59 viboko ni 6, na 60-79 ni vitatu.
Akaanza kuwanyoosha wa fimbo 3 tatu, wakafata wa 6, then tukaja sisi wa viboko 9, maana mimi sikufanya swali lolote hivyo niliscore 0(zero), me nkabaki zangu wa mwisho ili nimuelekeze mimi ni mgeni na hili somo sijawahi kulisoma, kumbe bhana mtu kashanitamani aloooh apo ndo kazi ikaanza yaani tulibishana sana, kila akisema shika vidole mimi nagoma sishiki wala kuinama, asee aliongea kwa hasira na kwa kelele sanaa
NIMESEMA INAMA SHIKA VIDOLE.. Asee alianza kunipiga fimbo kila mahali ndipo nikaamua na mimi kujitetea alooo mtu alikula ngumu mixer mateke yaani tulipigana haswa na kiukweli nlimzidi ad shart lake likachanika na suruali yake ilichafuka mno kwa kiwi ya kiatu changu.
Teacher kuona ishakuwa ivyo akatoa simu akampigia second master na walimu wengne wakaja bhana class wakamuona alivyo na mimi pia wakaniona hali nilyonayo yaani nlikuwa nishaamua liwalo na liwe ila apa sikubali anichape yaani bora nichwapwe na walimu wote ila so yeye, bhas bhana second akamwambia nenda kabadilishe shart na suruali wakati tunaangalia namna ya kumuonya ama kumfukuza huyu mwanafunzi, basi bhana walimu wakatoka na mimi na KENGELE YA EMERGENCE ikapigwa.
Siwezi sema nini kiliendelea ila huyo mwalimu alikuja kuwa karibu na mimi mno na somo lake la AGRICULTURE Nilipenda sana na nililitendea haki ad akawa aninitolea mifano chanya.
NOTE: Mwalimu huyo leo hii ni afisa Ugavi mkoa flani, na ata nikiwa chuo tulikuwa tukiwasiliana sana na alinikutanisha na marafiki zake hivyo alikuja kuwa msaaada kwangu. Na agriculture ni somo zuri sana kuwahi kusoma kati ya masomo yangu yote naweza sema hivyo.