Ulifanya kosa gani Shuleni Hadi kengele ya dharura ikagongwa watu wakaja mstarini kwa ajili yako?

Kuna dogo juz tu hapa.alirudishwa shuleni kisa hajavaa soksi.akaambiwe akamuite mzazi wake. Dogo akakumbuka kuwa alishapewaga hela ya soks na mzazi wake ila aliifanyia matumiz mengne ayajuaye. Basi akajiongeza akatoka darasani na kuelekea nje ..watu wakajua kuwa anaenda home..kumbe alipofika nje ya darasa akaiona kengele akataka aibebe akauze kama chuma chakavu..ili apate pesa ya soksi.basi wakati anaitoa pale ilipo ikatoa mlio..madarasa mengne wakashangaa mbona kengele inagonga muda sio stahik kwa jambo lolote...
 
Shule za jeshi ndo mateso hivyo? Poleee sana
 
Mi bana siku ya kwanza naingia mchaka mchaka darasa la kwanza ila kimtaa,
kuna dogo alinikanyaga mguu aisee nilipiga mpaka kazimika nikakimbia.
Nikaambiwa nisirudi shule
Maza mwalimu karekebisha nikarudi shule
dawati langu nilikua na madem mgeni cheupee mtoto w! Mwalimu na asunta Mtoto wa tajiri mkubwa tu pale.
Bana miaka minne tunacheza mpira dogo Rafael anataka kulipiza.
Wale madem mi walikua washkaji tu.
Kaleta biff tena alikua anamtaka mgeni kwa lazima,
Mgeni analalamika na alikua cheupe(mbulu)
Aisee siku nilikamata hicho ki raphael nilipondaponda yaani kalitoka pale kamelowa.
Asunta hata aweki neno, alikua black beauty with brain.
Rafael kaenda kuripoti kwa babaake.
Babaake si akaja shule.
Kanitwanga ngumi vizuri tu,
Sikumjibu.
Dingi karudi kakuta nimevimba.
"Mwanangu vp"
"nimepigwa"
Na nani?fulani
Mzee akanunua ugomvi "twende"
Zilipigwa ngumi siku hiyo alipigwa mtu mpaka kakaa chini.
huo ndio ubabe mpk leo naujua
 
Basi ikapigwa simu nyumbani kwa dogo..kapokea bi mkubwa ...akaulizwa kuhusu mwanae kutokuwa na soksi. Bi akasema alishapewaga pesa na baba ake..dingi aliporud akapewa taarifa..ikabid aende shuleni kuuliza.. JE KENGELE ITAGONGWA TENA.. NA JE DOGO ANGESEPA NA KENGELE INGEGONGWAJE!?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi nilikuwa mtoro shuleni wakati wa chakula Naenda kula kwa binamu yangu alikuwa karibu na shule, maana shule ilikuwa boarding.Wakati Narudia njia ya uchchoro nikakutana headmaster!Kengere inagongwa na kuzomewa,penda kula hili.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Umenikumbusha kisa cha mwamba 1, tuliesoma nae, jamaa alizingua akapewa karatasi ajieleze, akashusha bonge la mtongozo kwa madam(mkuu wa shule)

Kilichofuata ikapigwa kengele, jamaa alikula fimbo za kutosha, alipoona kazidiwa alitoka nduki, sijawahi kucheka ktk maisha yangu kama nilivocheka siku ile.
 
Jamani mimi kuna tukio nililifanya miaka ya zamani nikiwa darasa la nne(4) japo sio shuleni ni tukio lilitokea nyumbani. Hadi leo hii nikikumbuka hicho kisa kama nipo na mzee karibu huwa naishiwa kabisa furaha.

Kwanza kwangu ni zaidi ya aibu na hilo tukio lilipelekea nikachukia kipaji changu, tangu hiyo siku sijawahi tena kumsikia mzazi akiniuliza nimesoma nini huko shuleni. Ni kuitisha tu karatasi za mitihani tena kwa unyonge, amakweli "what goes around comes around!! Na mimi nahangaishwa na vijana.
 
Mimi na wenzangu tuliweka upupu ofisi ya walimu. Siku hiyo walijikuna sitasahau enzi hizo.
 
Darasa la tatu mwalimu mkuu wakati huo,alikuwa anateua ma moniter na monitress mwenyewe,mimi niliteuliwa mwanyoni mwa muhula wa kwanza,kufikia mwezi wa sita,darasa likanishinda,kila nikiandika wapiga kelele wakienda kuchapwa basi njiani kurudi home nakula kisago, ikafkia hatua kila wakianza kupga kelele nikiwataka wanyamaze "acheni kelele" hawatulii naanza kulia, hali hii nikaenda nayo ikanichosha,nikajitosa hadi kwa mkuu wa shule,nikamwambia "mwalimu naomba unitoe umonita nimechoka" teacha kimya kimya akachukua kiboko akanitandika barabara viboko 6 na kuniamuru nirudi class, jion yake saa 10 wakati wa kwenda home kengere lilipogongwa akatanganza mstarini kuwa kuanzia leo xxxx si monita tena. Mpaka leo sjapata karma ya uongozi tena dadeki zangu.
 
Darasa la tatu mwalimu mkuu wakati huo,alikuwa anateua ma moniter na monitress mwenyewe,mimi niliteuliwa mwanyoni mwa muhula wa kwanza,kufikia mwezi wa sita,darasa likanishinda,kila nikiandika wapiga kelele wakienda kuchapwa basi njiani kurudi home nakula kisago, ikafkia hatua kila wakianza kupga kelele nikiwataka wanyamaze "acheni kelele" hawatulii naanza kulia, hali hii nikaenda nayo ikanichosha,nikajitosa hadi kwa mkuu wa shule,nikamwambia "mwalimu naomba unitoe umonita nimechoka" teacha kimya kimya akachukua kiboko akanitandika barabara viboko 6 na kuniamuru nirudi class, jion yake saa 10 wakati wa kwenda home kengere lilipogongwa akatanganza mstarini kuwa kuanzia leo xxxx si monita tena. Mpaka leo sjapata karma ya uongozi tena dadeki zangu.
 
Wewe jamaa wewe kutoka mikoa ya Mara au Mwanza ulitisha,hata kujiridhisha tu kuwa madame yupo hakuna?
Ndugu yangu, jana yake ndio tulikuwa na madam class na sikuona kama alikuwa na dalili yoyote ya ugonjwa tena nakumbuka vizuri ilikuwa ni siku ya jumatano.

Alhamisi ndio mambo yakaharibika, tena toka siku hiyo niliisha ichukia siku ya alhamisi hata niwe na mipango yangu ya pesa huwa siifanyi kwenye hii siku hata kusafiri tu huwa nakuwa mzito ikitokea nimelazimika kusafiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…