Ulifanya kosa gani Shuleni Hadi kengele ya dharura ikagongwa watu wakaja mstarini kwa ajili yako?

Ulifanya kosa gani Shuleni Hadi kengele ya dharura ikagongwa watu wakaja mstarini kwa ajili yako?

Kuna dogo juz tu hapa.alirudishwa shuleni kisa hajavaa soksi.akaambiwe akamuite mzazi wake. Dogo akakumbuka kuwa alishapewaga hela ya soks na mzazi wake ila aliifanyia matumiz mengne ayajuaye. Basi akajiongeza akatoka darasani na kuelekea nje ..watu wakajua kuwa anaenda home..kumbe alipofika nje ya darasa akaiona kengele akataka aibebe akauze kama chuma chakavu..ili apate pesa ya soksi.basi wakati anaitoa pale ilipo ikatoa mlio..madarasa mengne wakashangaa mbona kengele inagonga muda sio stahik kwa jambo lolote...
 
Nilisoma shule ya jesh jina kapuni so kulikuwa na askar mmoja ana mwili mkubwa na c. Unajua walimu huwa kwa wanafunz wana majina yao ya utan so tulikuwa tunamuita jambo kubwa ingawa mwenyew hakufaham na kama alifaham alikosa ushahd so cku iyo aliniagza nikawaambie wanafunz wenzng kuwa ikfika saa 8 wasiondoke kuna matangazo ebwana nikaenda nikawatangazia so kuna ticha mmoja nae ni soja akaniuliza mwlim gan kakutuma utoe hilo tangazo c nikaropoka yule JAMBOKUBWA akaniambia jambokubwa kwa mshangao akanipeleka ofcn matcha wengne walvyosikia ule mkasa wakacheka afu jambokubwa mwenyew yupo hapo alimaind then alikuwa captain yaan nyota 3 akawaita wanafunz wote nao walivyotangaziwa ule mkasa c wakacheka wakaambiwa kwanza wagalegale kweny matope wakala stick advance wote afu ikaja zamu yangu nilikula stick mabao mabut had alipotokea mkubwa wake kanal ndo akamuamuru aache apo nishalowa vbaya mno asee acngetokea yule kanal cjui ingekuwaje
Shule za jeshi ndo mateso hivyo? Poleee sana
 
Mi bana siku ya kwanza naingia mchaka mchaka darasa la kwanza ila kimtaa,
kuna dogo alinikanyaga mguu aisee nilipiga mpaka kazimika nikakimbia.
Nikaambiwa nisirudi shule
Maza mwalimu karekebisha nikarudi shule
dawati langu nilikua na madem mgeni cheupee mtoto w! Mwalimu na asunta Mtoto wa tajiri mkubwa tu pale.
Bana miaka minne tunacheza mpira dogo Rafael anataka kulipiza.
Wale madem mi walikua washkaji tu.
Kaleta biff tena alikua anamtaka mgeni kwa lazima,
Mgeni analalamika na alikua cheupe(mbulu)
Aisee siku nilikamata hicho ki raphael nilipondaponda yaani kalitoka pale kamelowa.
Asunta hata aweki neno, alikua black beauty with brain.
Rafael kaenda kuripoti kwa babaake.
Babaake si akaja shule.
Kanitwanga ngumi vizuri tu,
Sikumjibu.
Dingi karudi kakuta nimevimba.
"Mwanangu vp"
"nimepigwa"
Na nani?fulani
Mzee akanunua ugomvi "twende"
Zilipigwa ngumi siku hiyo alipigwa mtu mpaka kakaa chini.
huo ndio ubabe mpk leo naujua
 
Basi ikapigwa simu nyumbani kwa dogo..kapokea bi mkubwa ...akaulizwa kuhusu mwanae kutokuwa na soksi. Bi akasema alishapewaga pesa na baba ake..dingi aliporud akapewa taarifa..ikabid aende shuleni kuuliza.. JE KENGELE ITAGONGWA TENA.. NA JE DOGO ANGESEPA NA KENGELE INGEGONGWAJE!?
 
Kunakipindi nilikua nasoma shule ya msingi kulikua kuna mama anapika mihogo nje ya shule, kwakua shule ilikua na uzio kwahyo kwenda kununua ni kipengele.

Mimi nlikua na fahamika vzur kwa kutoboa fensi, kwahyo nilikua napewa hela na darasa zima naenda kuwaletea mihogo wakati wa mapumziko..

Siku moja nikaingia tamaa ile hela ya wanafunzi nikanunulia saa kali ya mkononi..

Nkarudi darasani huku ninalia wanauliza mihogo iko wapi nkawaambia mwalimu Apolo amenishika nikiwa napita kwenye fensi akaniambia niile mihogo yote na fimbo za kutosha nimekula.

Sasa ubaya nikwamba kuna mtoto wa mwalimu akakazirika akaenda ofisini akamwambia mamake anaomba hela maana mwalimu apolo amemwambia Ayos ale mihogo yetu.

Kumbe mwalimu apolo akuwepo siku hiyo yaani nilikuja kuchukuliwa msobemsobe yani sita sahau milele lile tukio.. mpaka leo stakagi kabisa kuvaa saa naichukia yani nkama nina aleji na saa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi nilikuwa mtoro shuleni wakati wa chakula Naenda kula kwa binamu yangu alikuwa karibu na shule, maana shule ilikuwa boarding.Wakati Narudia njia ya uchchoro nikakutana headmaster!Kengere inagongwa na kuzomewa,penda kula hili.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hahaaa!!!

Nilisomaga shule moja ya kulipia, ile shule ilikua primary & secondary. (Zote boarding)

Primary walikua wanalipa ada za maana, hata msosi wao ulikua wa maana, mixer mikate na blueband, chai ya maziwa, mayai etc,

Sie wa secondary ada ilikua kawaida tu, so hata huduma zetu ni kawaida kama kayumba tu lakini wote tulikua compound moja na shule zote mmiliki ni mmoja.

Na kama unavyojua shule za boarding kitengo cha misosi, kila siku ni ugali mchana, ugali usiku, mboga ni maharagwe mwanzo mwenga. Wali ilikua ni alhamis mchana(ukikosa hapo ni mpaka next week )

Nilikua na kampani ya washkaji zangu, jumla tulikua wanne, kama masihara sijui ata tulianzaje tukawa na mchezo wa kuzamia jiko la primary, tunaiba maandazi na maziwa.

Ikifika usiku(mida ya prepo) sie tunachomoka mmoja mmoja darasani tena kwa ishara, tunaenda kukutana kwa mkapa(jikoni)

Kuna kidirisha kidogo wanachotumia kugawia msosi, sasa kile kidirisha kilikua hakifungi, kinarudishiwa tu(ni vile vya nondo)

Sie ndio tukawa tunapenya pale tunaingia jikoni, tunakuuuula maandazi weee na kunywa maziwa kama mapanya, then hao tunarudi darasani tukiwa tunafuta midomo tu, huku tunawacheka kisiri siri wenzetu waliokula ugali maharagwe.

Mwanzo ilikua wanazama watatu, mmoja anabaki akisoma ramani, kuangalia kama mlinzi anakuja ama la, so mkitoka mnamletea na yeye maandazi na ikitokea mlinzi anakuja, jamaa anawastua mnajikausha mle jikoni kimyaaa, mlinzi akija anapita pita tu then anaondoka nyie mnaanza mashambulizi upya.

Baada ya kuzoea mchezo ule ikaja kuonekana kwamba mtu anaebaki nje kuangalia soo, hafaidi vizuri, maana mkitoka mnamletea maandazi tu, maziwa hapati, hivyo tukaamua kuwa kila mtu ni lazima azamie(hakuna cha kubaki kucheki soo) Mistake no 1

Tulivyokubuhu na mchezo ule, tukaanza kuzamia na mabegi na chupa. Tukiingia ni uharibifu wa maana.

Maandazi yalikua yanawekwa kwenye ndoo, kwa hiyo ukizama ndani, unafungua zipu ya begi lako kisha unalivalisha kwenye mdomo wa ndoo, kisha unanyanyua juu chini(kama wnavyofanya wauza nyanya na vitunguu kwenye visado njiani), mzigo wooote unaingia kwenye begi, maziwa mnamimina kwenye chupa, then haoooo mnasepa. Ilifika point kuna mshkaji wa nje alikua anakuja kununua maandazi kwetu na yeye anaenda kuuza.

Mie binafsi ilikua nikiingia cha kwanza napiga vikombe viwili vya maziwa fresh bariiidiiii (kupoza koo)kisha ndio naanza mashambulizi.

Siku hiyo kumbe kuna mtego umewekwa bwana, tumezama vizuuri tu, mie kama kawaida huyooo kwenye vikombe [emoji478] nikachukua kimoja kisha huyoo kwenye friji(ni giza lakini ramani yooote naijua) nimepiga funda la kwanza fresh ile napiga la pili nashangaa mwanga mkali balaa unanimulika usoni (I was like am I dreaming!!!??? red handed na kikombe cha maziwa tena jiko la primary daaah) tochi nne zinamulika from different angles.

Ndo ikawa hivyo tena, kengele ikagongwa usiku ule ule(9:30pm) wanafunzi woote shule nzima wakaambiwa wanatakiwa kwenda eneo la jikoni kuna dharula, kufika jikoni wanatukuta wazee wa kazi tupo ndani ya jiko.

Shule nzima mwanangu wanatuzomea tu, halafu nilikua nina penzi jipya na kishombe shombe flani so ilikua noma sana yani.

Wale washenz walisubiri shule nzima imefika ndio wakatutoa mle jikoni.

Ila mwisho wa siku maisha mengine yaliendelea.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Umenikumbusha kisa cha mwamba 1, tuliesoma nae, jamaa alizingua akapewa karatasi ajieleze, akashusha bonge la mtongozo kwa madam(mkuu wa shule)

Kilichofuata ikapigwa kengele, jamaa alikula fimbo za kutosha, alipoona kazidiwa alitoka nduki, sijawahi kucheka ktk maisha yangu kama nilivocheka siku ile.
 
Jamani mimi kuna tukio nililifanya miaka ya zamani nikiwa darasa la nne(4) japo sio shuleni ni tukio lilitokea nyumbani. Hadi leo hii nikikumbuka hicho kisa kama nipo na mzee karibu huwa naishiwa kabisa furaha.

Kwanza kwangu ni zaidi ya aibu na hilo tukio lilipelekea nikachukia kipaji changu, tangu hiyo siku sijawahi tena kumsikia mzazi akiniuliza nimesoma nini huko shuleni. Ni kuitisha tu karatasi za mitihani tena kwa unyonge, amakweli "what goes around comes around!! Na mimi nahangaishwa na vijana.
 
Mimi na wenzangu tuliweka upupu ofisi ya walimu. Siku hiyo walijikuna sitasahau enzi hizo.
 
Darasa la tatu mwalimu mkuu wakati huo,alikuwa anateua ma moniter na monitress mwenyewe,mimi niliteuliwa mwanyoni mwa muhula wa kwanza,kufikia mwezi wa sita,darasa likanishinda,kila nikiandika wapiga kelele wakienda kuchapwa basi njiani kurudi home nakula kisago, ikafkia hatua kila wakianza kupga kelele nikiwataka wanyamaze "acheni kelele" hawatulii naanza kulia, hali hii nikaenda nayo ikanichosha,nikajitosa hadi kwa mkuu wa shule,nikamwambia "mwalimu naomba unitoe umonita nimechoka" teacha kimya kimya akachukua kiboko akanitandika barabara viboko 6 na kuniamuru nirudi class, jion yake saa 10 wakati wa kwenda home kengere lilipogongwa akatanganza mstarini kuwa kuanzia leo xxxx si monita tena. Mpaka leo sjapata karma ya uongozi tena dadeki zangu.
 
Darasa la tatu mwalimu mkuu wakati huo,alikuwa anateua ma moniter na monitress mwenyewe,mimi niliteuliwa mwanyoni mwa muhula wa kwanza,kufikia mwezi wa sita,darasa likanishinda,kila nikiandika wapiga kelele wakienda kuchapwa basi njiani kurudi home nakula kisago, ikafkia hatua kila wakianza kupga kelele nikiwataka wanyamaze "acheni kelele" hawatulii naanza kulia, hali hii nikaenda nayo ikanichosha,nikajitosa hadi kwa mkuu wa shule,nikamwambia "mwalimu naomba unitoe umonita nimechoka" teacha kimya kimya akachukua kiboko akanitandika barabara viboko 6 na kuniamuru nirudi class, jion yake saa 10 wakati wa kwenda home kengere lilipogongwa akatanganza mstarini kuwa kuanzia leo xxxx si monita tena. Mpaka leo sjapata karma ya uongozi tena dadeki zangu.
 
Wewe jamaa wewe kutoka mikoa ya Mara au Mwanza ulitisha,hata kujiridhisha tu kuwa madame yupo hakuna?
Ndugu yangu, jana yake ndio tulikuwa na madam class na sikuona kama alikuwa na dalili yoyote ya ugonjwa tena nakumbuka vizuri ilikuwa ni siku ya jumatano.

Alhamisi ndio mambo yakaharibika, tena toka siku hiyo niliisha ichukia siku ya alhamisi hata niwe na mipango yangu ya pesa huwa siifanyi kwenye hii siku hata kusafiri tu huwa nakuwa mzito ikitokea nimelazimika kusafiri.
 
Back
Top Bottom