25000q
JF-Expert Member
- Dec 27, 2022
- 4,805
- 3,762
Nilipo ishiwa mtaji baada ya kupakia nyanya kuto geita kwenda mabibi sokoni darWakuu embu tujuzeni ulipitiaje kipindi ukiwa huna hela maisha yamekupiga total knock out and huna kula kulala ya uhakika?
Mie nimejaribu mishe za udalali ila hailipi kabisaa na ni majanga bin vuuu. So how do / did you cope with this situation?
Matenga hayo yanya nilikuwa natumia dalali wangu mala kwa mala Kisha ananitumia hela baada ya kuuza
Ilikuwa ni trh 20 mwezi wa 12 nyaya hizo zilikuwa zinawai hili zikauzwe siku ya sikuu
Dereva alitembea kufika kibaigwa gali likaaribika kibaya zaidi dereva akazima cm akaanza kutengeneza gali lake
trh 22 nikampigia dalali akasema gali aija fika nikimpigia dereva apatikani trh 23 nikaamua kwenda kulipoti polisi wakaamua kutafuta namba hiyo kwa njia ya mtandao wakasema
Kwamala ya mwisho simu yake iliwasiliana kwenye mnala wa kintiku mwisho kibaigwa
Nikaamua kuwa pigia madalali wa kibaigwa na kintingu hili walitafuta gali hilo nikawaeleza lilivyo na namba zake
Madalali wa kibaigwa wakalikuta limepakiwa pembeni mwa barabala huku kibini imeibsmishwa mafundi wako kazini nyuma kwenye kuchanja kuna matenga ya nyanya
Wakampa simu nikamuuliza kulikoni?akasema natengeneza kisha niendelee na safari hiyo trh 24 ikabidi madalali wafaulishe mzigo kwenye gali nyingine kwenda sokoni ifahamike wakati huo nynya zilikuwa na siku 5 tangu zitoke shamba siku 3 ziko Juani juu ya gali
Kufika sokoni siku ya sikuu asubuhi nyaya zote masalo zimeoza yaani uchafu tu hata hela ya kulipia nauli haikupatikana
Ifahamike pesa nilio kuwa nibakinayo mfukoni kama akiba ilitumika kutafuta gali hilo na kuwa tumia madalali kibaigwa
Ilibidi niombe rifuti kutoka runzewe hadi dar nikafika nyumbani sina hata mia
Akili ikafa ghafura milioni yangu 5 ikawa imeyeyuka kimtindo nikaanza kuuza tv hela tunatumia mala simu mala masofa
Sasa nikajikuta sina cha kuuza watoto wanatakiwa kula kwenda shule bahati nzuli silipi kodi maisha yakawa magumu sana
Nikaamua kujiunga na mafundi wa kujenga tukaenda goba nikapewa Sululu na koleo kuchimba msingi tangu asubuhi mpaka saa 12 jioni malipo sh 15000 hela hiyo nilipata lakini mkono ikawa umepasuka hata kula nilishindwa kesho yake sikuludi
Hali ikazidi kuwa mbaya nikawafuta tena mafundi nikakuta kuna kazi ya kubeba zege ndoo ya kilo 20 ninzito usiseme malipo kwa siku 30000 nikakomaa kiume
Wiki 2 nikapata sh kama 250000 baada ya kutoa matumizi
Nikaamua kwenda kukodi tololi Tandale kwa mama 1 anayo mengi ya kukodisha nikaanza kuuza machungwa nanunua Mabibo natembeza miguu akawa inauma sana nikashindwa lakini yalikuwa yana lipa sana kila siku sikosi kuweka sh 20 kama faida
Nikaamua kununua baiskeli anita nikawa na funga vikapu vili mfano wa mizega zega au kama unavyo beba punda mizigo
Nikawa sasa nabeba machungwa mengi na chagua mazuli na mwamvuli wangu naenda kutega kwenye maegesho ya magali madogo
Kama pale makumbusho nauza sana yakibakia naenda pale nwenge sehemu ya mpakani jioni kuna wasafiri wengi pamoja na wanafunzi wa chuo nauza sana saa 3 napeleka basikeli yangu kwa walinzi wa maduka napanda basi nyumbani
Kwa kifupi nilipambana na kazi hiyo kwa msimu 1 tu nikapata 1000,000, ikawa sababu ya kujenga banda la matunda Masaki wakaja libomoa migambo kwenye bomoa bomoa ya mama samia kwa sasa nashukuru nimeludi kwenye kazi yangu ya nynya na vitunguu maji na awamu mwaka huu sio siri kazi nimefanya