Ulifanyaje kipindi huna hela, yaani maisha yamekupiga total knock out?

Watu watakwambia beba zege, choma viazi, osha gari.

Hakuna atakayekwambia njoo mtaa C ukifika kuna mshkaji F mwambie umekuja kubeba zege/ choma viazi/ kuosha gari.

Hii ndiyo tofauti ya members wa mitandao ya kibongo na ile ya nje ya bongo. Hata mtu akisema njia aliyopitia anasema nilipambana mno ila hasemi ni kwa namna gani.

Mkuu, una marafiki/ ndugu hawa ndiyo wanatakiwa wakukumbuke wakisikia michongo. Wanakuamini? Wanajua uwezo wako ingawa upo benchi?

Ingawa sikua nimeajiriwa kabla ya wenzangu ila walijua kua jamaa ishu za sales ataweza. Mmoja aliposikia ishu nikatafutwa nikaenda, now here is the issue, kwa kawaida mimi ni mkimya mno halafu nikagewa hiyo ishu so ikabidi niadopt.

Hichi unachofanya wewe nilishafanya tena humuhumu na ninakuhakikishia una 0.091% za kupata mtu wa kukupa suluhu humu. Wengi humu ni stori nyingi.
 
Kitu kingine nimesahau.

Watu wanaziongezea chumvi CV zao vibaya mno. Wewe unaweza sema hapa nilifanya field miezi miwili huu uzoefu nisiuonyeshe halafu kuna mwenzako kafanya mwezi, anauonyesha na anaupamba.

Mwengine anaandika vitu hajawahi kufanya but the catch is you have to look the part na udefend hiko unachosema unakijua. Mfano wewe unajua kutumia computer ila hujui kutumia excel labda lakini kwenye CV unasema uko vizuri kwenye excel.

Fungua profile linkedin, ijaze details za msingi. Anza kuwafuata HR inbox, ni wala hongo so utajua unaanzia wapi.
 
Issue nipo Moshi, huku hakunaga hizo bolt bin uber, huku ni bajaj mostly na hata kisela kisela ni ngumu kugusa chombo cha mtu, unaweza kung'utwa mpaka usahau kuwa una njaaa.
Pole sana kwa mkoa wa kilimanjaro wajwnja ni wengi sana hapo Town.......kama unaweza hama mkoa hrbu jaribu kuhama kajaribu na sehemu nyingine ukute bahati yako haipo hapo
 
Nenda kwa watu wanaofanya biashara ya catering ,uombe kaz ya ku serve ,utapata na msosi bure,kwa wale wanaopikia nyumban ndo wazuri,
 
Sema niliomba kazi za Takukuru ila nahisi kigezo cha umri ndo kimenipiga knock out directly maana nagonga 30 mwaka huu.
Watu wanaingia humo above that age mzee. Nchi ngumu hii kama huna refa. Yani una sifa sote kabisa, ila unaachwa. Mtoto mmoja wa kamishna sifa hana ila baba anambeba na kitengo kizuri anapata kazi....acha kabisa mkuu
 
MANYEMA PALE SOKONI MZEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE AU WAPI ??? VIPI KUNA MISHE GANI HUKOO MANYEMA ????
Kuulizia kuwa manyema kunamishe gani ni umezingua. Ilitakiwa umcheki bhana pm mwasiliane muonane then along the way ukifika manyema mwenyewe utaangalia au kuelekezwa maana jamaa ameonesha kutaka kukuonesha njia.. Ila wewe unaleta ujuaji.
Sokoni, Unajua kuna mishe gani.
 
Great inspiration.
Sio wale wengine stori zao zinaruka kama CD ya james bond.
 
INAFIKIA ILE HATUA UNASIKILIZIA FUTARI MSIKITI WA JIRANI
HATA KAMA SIO MUISLAMU BIN VUUUU
PINDI LIFE LIMEKUKAMATA NA UKA KAMATIKA YAAANI HUNA HATA MIA MBOVU YA KUNUNULIA MHOGO WA KUPOZA NJAA



GHAFLA BIN TAABAN MWEZI WA RAMADHANI UNAKUWA MSAADA WAKO HAHAHA


LIFE HILIIIIIIIIIIIIIIIII
 
HEYEEEE HEYEEEEE MAISHA NI KUCHANGAMKAAA ASEEEEE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…