Ulifanyaje ulipoachika?

Ulifanyaje ulipoachika?

Dah yaani hapa natoka kuachika Kwa sababu ambazo naziona sio za msingi kabisa, nimempa 100k akafanye ishu zake nyingine bila hata kuniomba.

Hata Asante hakusema, juzi ananiomba Tena shilling laki Moja ambayo Haina maelezo yoyote [emoji848] She was like... Umm babe naomba shilingi laki Moja[emoji33][emoji33] meseji ikaishia hapo.

Nami sikujibu chochote nione reaction Yake mpaka zilipoanza lawama kwamba nimekua bahili siku hizi[emoji51][emoji51]
Nikawambia yes mimi ni bahili so what, akadai tuachane.

Nami nikaona poa tu maana Amna mambo apa zaidi ya kuchunwa tu[emoji51] sijataka kuhoji kuhusu ile pesa nilomtumia bila kuomba. Nipo nipo tu kichwa kime hang[emoji56][emoji56][emoji56]

Kumbe kuachwa ndo inakua hivi[emoji33][emoji33] Ila naona kama nimetua ka mzigo Fulani hivi, kuachana na hii Toyota brevis [emoji23] ila Kuna mda naanza kumuwazia Tena.

Ebu nipeni mbinu nifanyeje ku overcome ishu kama hii
mzabzab
Mzee wa kupambania

Eti To yeye mtu anaekutumia pesa bila kuomba ni bahili[emoji848]
Shunie Antonnia Depal Chakorii ebu kuweni na huruma na pesa zetu wandugu
Mada nyingi za hivi siyo za wana ndoa
 
Kaka..Nimecheka hapa ofcn hadi wenzangu wamenishangaa....mbavu zangu, kwanini nacheka? mm yalinikuta makubwa..enzi za ujana 2000s, nilipata kidemu flani kizuri sana kinaitwa Sofia, hali yangu kiuchumi kweli nilikuwa hoi bin taabani, mtoto tukapendana sana tu, kweli nikasahau shida zangu angalau kwa muda, kula yangu kama kumchinja Kobe "timing" kwahiyo kunasiku anapiga tafu, kumbe bwana upande wapili kuna jamaa anamnyandua Sofia, huku nakule si nikagundua, hasira ya wivu nikalianzisha, tulikuwa tuna kaa Geto tuko mtu 4 room 1, nikatembeza bakora, binti kanipiga biti la hatari kadai hataki tena urafiki, nikaitisha kikao na washkaji haraka sana, eti nadai nilichokiita gharama zangu.. huyo mgoni wangu jina Luka.. alikuwa kibaka kwahiyo yeye pesa si tatizo kubwa, kikao kikanguruma Sofia akaulizwa unamtaka nani kati yahawa wawili... akadai anampenda LUKA.. wakuu kwanza nilipoteza uwezo wa kuona, kusikia, kujitambua nilishindwa kujibu chochote kaayangu kimya ikachukuliwa nimekubali hoja, ... nikatakiwa niwasilishe madai.. nikadai 50,000/- LUKA kavuta 100,000/- aiseee.... hili tukio lilinitesa muda mrefu, kumbe hata gharama zote za kikaoi kiwemo chakula na posho za wajumbe alilipa LUKA. kumbe hata zile fedha alizokuwa ananihonga Sofia alikuwa anapewa na LUKA. (LUKA the Great)
Ulikua great marioo in town
 
Back
Top Bottom