Ulifikishaje Milioni 10 ya kwanza?

We Noma Ni Mpambanaji
 
Safi sana mkuu kwa ufafanuzi mzuri sana tofauti na wengine hawasemi jinsi walivyopata hizo pesa zaidi zaidi wanasema tu kiasi kwa mtu alofunguza uzi kwa lengo anaoshia ku stressika kwa jinsi watu walivyopata pesa na njia hawasemi ila wewe umelezea vizuri na Kuna vitu nimejifunza shukrani mkuu.
 
Ukiona mwanaume hasa kijana kajenga mjini, Narudia KAJENGA NYUMBA YAKE HASWAA na anamiliki assets zingine! Aisee ujue karuka mitego mingi sana, kafumbia macho makalio ya kila aina ya kina dada, tena wazuri na warembo mno, kufumbia macho anasa nyingi n.k!

So mbinu au ideas zile zile zinaweza kutumika ili kufikia malengo uliyojiwekea, Make kadri unavyozidi kupata mapesa ndivyo Lucifer nae anazidisha urafiki na wewe na kukuonyesha miliki zote za dunia hii hata ambazo hukuwahi kuziwazia kabisa..
 
Vizuri sanaaaa embu nipe maujanjaa namie dadaaa
 
Nina ki account cha $ kila mwezi naweka minimum $100. Ikifika mwisho wa mwaka nazitoa zote naamua tu vacation wapi. Sasa hapo wengine wakiona mwisho wa mwaka unasafiri huku na kule wanashangaa!
Binafsi saving kwangu haijawahi kuwa tatizo maana pia naogopa mikopo .

Nina salary ndogo tuu take home haizidi 600k but hapo nasevu half of it .

Sasa nikipata na viposho posho huwa sipingui 2.5-4 ndani ya miezi 6 na nikipata hiyo nanunua investment au nafanya mtaji somewhere.

Ndani ya mwaka naweza fikisha saving ya Kati ya 5ml hadi 6 kwa hiyo hizi naweka kweye assets mwisho wa siku nikijumlisha assets zangu zinavuka hiyo 10 mln.

Kitu cha kukwamisha ni labda nipate mgonjwa wa mda mrefu tofauti na hapo nafikisha,nimejenga kwa staili hii hii na kama nakopa ujue ni kwa friend na si vinginevyo.
 
hii njia bora kabisa kwangu pia

NB;HAKIKISHA UNAJUA MATUMIZI YAKO YA MWEZI NA KUTENGA PESA YA EMERGENCY
Kiufupi watu wanacomlicate maisha,ukiushi kwa kiasi wala hakuna shida ila sasa utaitwa mbinde sijui nani kila jina baya but unapuuzia tuu.

Mimi Nina hadi bajeti ya mademu
 
Anza hata biashara ya barafu usave hata 1000 kwa siku
Sio pesa ndogo hiyo,300k kwa mwezi ni ishu kama huna stable income.

Ila observation yangu nimeona watu wenye vipato vikubwa vya salary lakini mara nyingi wanaishiwa pesa kuliko mwenye mapato ya kawaida,hii inatokana na status
 
Vizuri sanaaaa embu nipe maujanjaa namie dadaaa
Maujanja ni kujitoa tu niliamuamua kukilipua

Nikaanza kwa kupost status natoa mkopo watu wakanicheka ila sikuchoka baada ya mda watu wananifata inbox kuomba mkopo mi nawapa vigezo na masharti tu

Na huwez amini mwezi huo pesa ilichukuliwa yote mpaka sasa sivuki mwezi na pesa ya mwezi uliopita kila mwezi pesa inachukuliwa yote
 
[emoji3516]
YOU GUY DO COPY MY MOTION.

HOW OLD ARE YOU HOMIE??

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
 
Sim banking app nimeifuta kwenye simu yangu, tatizo ni tawi la bank limeangaliana na nyumbani....sasa hapo sijui nafanyaje!

Nimedumbukiza atm choon ila wapi tatizo nikiona mlango wa bank umefunguliwa mate yananitoka[emoji134][emoji134]

Mnanishaurije wakuu? Nifanyeje?
 
Ngoja nikawaulize KCB Bank

7% [emoji848]
 
Maisha haya! Input yako ya ntaji mbona haiendani na output ya faida?

Mimi niliwekeza milion 1.9 na kila siku nikawa natengeneza net profit ya 300k kwa miezi kadhaa!
Biashara gani?
 
Nitaanzaa na Mimi aiseee maaana, kila kukicha gharama za maisha zinapanda. Ujakaa vizuri Kodi unavunja kibubu unalipia Kodi, kugeuka ada ya mtoto nihatarii sanaa
 

Nmecheka.Hamia uswekeni huko uache kuangaliana na Bank.
 
1. Take home ni 1,300,000 baada ya makato yote kazini pamoja na benki wakati wa kutoa

2. Nilishusha maisha tukawa tunaishi nyumba ya kupanga ya chumba kimoja elfu 35000 kwa mwezi, jirani kabisa na kazini, ninatembea kwa miguu saa moja nimeshafika. Mwanzo nilikuwa ninakaa nyumba ya 900,000 kodi ya miezi sita bado na umeme juu.

3. Nikaacha kula bia kila siku, nikawa ninakunywa mbili mwisho wa wiki

4. SIkupanga nyumba ya umeme, nilikopa sola ya Zola ule mtambo mdogo wa kulipia 10000 kwa mwezi

5. Bima, pampers na vyakula special vya mtoto (maana sometimes wanachagua sana vyakula wakiwa wadogo) nikaweka bajeti ya 150,000

6. Ikitokea shida sikuwa ninakopa kwa benki, ninakopa kwa marafiki.

7. Nikawa nina kazi za udeiwaka na udalali mida ya usiku na nje ya Ofisi

Nilipofanya hayo yote niliweza kusevu milioni 10 uliyotaja ndani ya miezi sita ya mwanzo na kuendelea, hapa ninavyoandika hivi nina gari ya kifahari SUV na nina nyumba ya zaidi ya milioni 30 ninayoishi na familia yangu na mama yangu nimemjengea nyumba ya milioni saba huko Kijijini kwetu.

Nimejifunza: FANYA IBADA, punguza bajeti za kifamilia, kama umepanga kaa jirani na Ofisi, ongeza njia za kupata kipato, sevu, wekeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…