Ulifikishaje Milioni 10 ya kwanza?

Daaah huwazii vyeti tena mkuu. Hongera sana
 
Nilianzisha biashara ya kufundisha watu jinsi ya kufaulu mitihani ya vyuo vya Marekani mwaka 2015. Miezi 3 baadae tulipata deal tukapata 16m na 4.5 m kati yake ilikuwa faida tukagawana na partner wangu so nikapata 2.25m.

Then Nikaanzisha biashara ya consultation kuhusu kumanage uzito mwaka 2016. Mpaka 2017 katikati nilikuwa na 10m saved tayari.
 
Utakua una tatizo la kutokua na mipango ya muda mrefu, yani ww ukipata héla basi utakachokutana nacho ndicho unachonunua, kwahio unawaza kua mtu anaetaka kununua sandals ndio atunze héla kwa miezi 6 plus? Labda kama nizile sandals za firauni[emoji16][emoji16], mtu mwenye malengo endelevu lazima awe na akiba endelevu , ukibakiza hio akiba ya buku/buku 2 unaenda nunulia Nini? au utakamilishia lengo gani?
 

Nina mipango mingi ndio maana siwezi kuweka hela ikae tu,hela inazungushwa wewe,fedha inaingizwa kwenye mzunguko ili ijizalishe.
 

mi nimejiunga mchezo wa laki tano for the first time mtu anapokea m6 tupo 12 na naonaa hii ni njia rahisi ya kusave manake kijumbe akikusimamiaa lazima utatoaa tu
 
VICOBA = Village Commercial Bank...
Nakushauri bora pesa yako ukainvest sehemu au uingie partnership au ununulie ata shares kama una knowledge na hivyo vitu kuliko uko Kwenye VICOBA na masaccos,uko ujanja mwingi watu wanacheza na % tu..

Vicoba havina asilimiaa ni vikoba vya watu wanaojuaa mtaani sidhan kama ni vya bank
 
Lazima uwe tajiri ila weka mbali sana mademu wanaturudisha wanaume. Komaa na mkeo kama umeoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…