Ulifikishaje Milioni 10 ya kwanza?

Ulifikishaje Milioni 10 ya kwanza?

Kwanza hongera sana kwa kazi uliyopata ni jambo la kumshukuru Mungu walau una sehemu ya kupata ujira wako!

Kuhusu suala lako, pia naomba nikupongeze kwa kuwa na malengo chanya. Tukirudi kwenye suala lako la msingi ningependa kukwambia yafuatayo:

1) Jitengenezee utaratibu wa kuweka akiba na uwe na nidhamu.
Hapa nataka kusema nini? Kwamba chagua bank ya aina yoyote enenda kafungue saving account [zipo aina mbali mbali za saving account - utachagua itakayo kufaa].

Then after, chagua kiasi chochote ambacho kila mwezi utakuwa unakipeleka kwenye account akiba yako. Mfano kama unapokea 1.5m, hakika kila mwezi ni lazima 500,000 uipeleke kwenye account. [Hii iwe mandatory]

Mfano unaweza kwenda pale KCB Bank ukafungua ile saving inayotoa 7% interest per annum.

Sambamba na kufungua lazima nidhamu ya pesa ishike mkondo wake, bila nidhamu itakuwa ni ngumu sana kufikisha malengo yako [Hakikisha kila mwezi unapeleka hiyo pesa na isipungue hata sent labda uzidishe!

2) Tafuta biashara ndogo ndogo ufanye ili zikuongezee kipato, ujue kutegemea only one source of income ni tatizo! Hii biashara utakayoanzisha ndo itakupa pesa ya kula na itakusaudia usipate tamaa yq kwenda kuchokinoa kwenye saving account yako!

3) Punguza matumizi yasiyokuwa ya lazima, hili kitakusaidia sana kufanikisha point no. 01

Mungu akubariki katika utekelezaji wako, Amina[emoji1317]
 
Back
Top Bottom